Wanaufufuo na watu wote mnakaribishwa kesho tujumuke kwa ajili ya bwana Mungu wetu

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,283
Reaction score
23,443
Ndugu zangu wapendwa huu ndiyo wakati wa kuwa imara zaidi kuliko wakati wowote. Simama na mathayo 10:28 HATISHWI MTU

Kumbukeni hili msije kusahau hata siku moja! Mungu yupo pamoja nasi wakati wote, Yeye mwenyewe Alisema DUNIANI MNAYO DHIKI LAKINI JIPENI MOYO, MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU (Yohana 16:33)

Usikubali Hofu ikuzuie kumfuata Yesu!

Hakuna vita vipya Yesu aliushinda ulimwengu vita vyote Vilipiganwa pale msalabani Alitangaza wazi kwa watu wote wenye kuamini katika Kristo kuwa IMEKWISHA!

Wao wanatutisha leo, wanazuia tusimwabudu leo lakini kumbukeni MSHINDI alishatangaza Ushindi kabla yao!

Kumbukeni neno lake ukimkana kristo leo naye siku ya mwisho atamkana mtu huyo.

Hata watesi wetu wamepanga kujumuika nasi kesho kumsifu bwana!

Heri ninyi watapowachukia kwa ajili ya mwana wa adamu...furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ipo juu mbiguni (luka 6:22-23)

Majeshi majeshi tukutane kesho mapema
 
Kwani ni lazima mkutane na kusali pale ubungo?
Hamwezi kupanga eneo jingine mkisubiri mustakabali wa gwajima na serikali Kisha kanisa likifunguliwa mnatejea eneo lenu?

Kwa Nia njema tu nauliza
 
Kanisa ni la Mungu na si mwanadamu!
Mungu akikwambia uende ukaihubiri injili mahala flani hutakiwi kwenda ambako hujaelekezwa.

Matendo 5:59 ...Ni heri kumtii Mungu kuliko Wanadamu

Kwasasa Sauti ya Mungu inasema tutasali hapo, Mungu akisema tukasali kwingine Tutakwenda
 
Oh kwahiyo mmelekezwa msali palepale?waumini wote si ndio?
Na mbona gwajima haji pale anasali chumbani kwake?
Nyie ndo mnaishia kupigwa virungu na polisi mnatupwa korokoroni ye anakuwaga wapi?
Ye kaelekezwa abaki huko si ndio?
Sawa
 
Natamani nikuulize KWANINI WAMEFUNGA KANISA? Lakini nafahamubhuna majibu ngoja nikujibu maswali yako;

Ukiwa huna roho mtakatifu huwezi kuelewa!
YESU MWENYEWE ALIJIFICHA soma Yohana 11:53-54 inasema: Basi tangu siku walipofanya shauri kwamba Wamuuwe, Kwahiyo Yesu hakutembea tena WAZIWAZI kati ya wayahudi.

Vivyo PAULO mtume alitoroka ndani ya kikapu, vivyo hivyo hata kwa ELIA

Kuna wakati wa bwana kusema na kuna wakati wa kujificha, na wakakati wa kurarua
 
Kwani ni lazima mkutane na kusali pale ubungo?
Hamwezi kupanga eneo jingine mkisubiri mustakabali wa gwajima na serikali Kisha kanisa likifunguliwa mnatejea eneo lenu?

Kwa Nia njema tu nauliza
Kwanini wakasali kwingine nasi hapo ubungo? Ebu waeleze hapo kuna shida gani ambako kwingine hakuna?
 
Natamani nikuulize KWANINI WAMEFUNGA KANISA? Lakini nafahamubhuna majibu ngoja nikujibu maswali yako;

Ukiwa huna roho mtakatifu huwezi kuelewa!
YESU MWENYEWE ALIJIFICHA soma Yohana 11:53-54 inasema: Basi tangu siku walipofanya shauri kwamba Wamuuwe, Kwahiyo Yesu hakutembea tena WAZIWAZI kati ya wayahudi.

Vivyo PAULO mtume alitoroka ndani ya kikapu, vivyo hivyo hata kwa ELIA

Kuna wakati wa bwana kusema na kuna wakati wa kujificha, na wakakati wa kurarua
Kamatieni hapohapo hadi kieleweke
 
Hawezi kujibu hilo swali akiwa na akili timamu subirini akilewa ndipo atawajibu kama mlevi
Kukashifu hakukuongezei kitu Wala hakukusaidii chochote.mi ni mmojawapo wa wapinga uovu na kufutiwa usajili na Hilo kanisa ni kitu nsichounga mkono.
Na najua sababu gani ilofanya wawafanyie hivo

But Nia yangu ni "usalama wao"
Shida mmejaa mihemko
 
Back
Top Bottom