Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Tatizo ni kupishana tu kwa mitazamo, mwanamke anaweza kushika mimba kwa sababu kadhaa
1. Imani kuolewa na huyo mtu
2.kuzaa mtoto mzuri kulingana na appearence za wazazi
3.mali
4.kuvutiwa na ukoo
5.uzembe tu
6. Au plan zingine tu

Kwa mwanaume yeye sababu ni moja tu kubebesha mimba kama kuonesha umwamba hatakama hataki kulea mtoto ila kile kitendo tu cha kumzalisha mtoto wa mtu ni fahari kwao ingawa ni upuuzi tu

In short ni upuuzi tu
jaman
 
Tatizo ni kupishana tu kwa mitazamo, mwanamke anaweza kushika mimba kwa sababu kadhaa
1. Imani kuolewa na huyo mtu
2.kuzaa mtoto mzuri kulingana na appearence za wazazi
3.mali
4.kuvutiwa na ukoo
5.uzembe tu
6. Au plan zingine tu

Kwa mwanaume yeye sababu ni moja tu kubebesha mimba kama kuonesha umwamba hatakama hataki kulea mtoto ila kile kitendo tu cha kumzalisha mtoto wa mtu ni fahari kwao ingawa ni upuuzi tu

In short ni upuuzi tu
Hayo yote ni kwa sababu ya jamii isiyo na ukombozi wa kifikra
 
Kuna kikundi kinakuja kupingana na mtoa mada,
Kudos mtoa mada sms sent
Kuna wanawake u-single mother wanautafuta kwa nguvu
1. Mtoto anazaliwa, wewe mama ndiyo unakuwa wa kwanza kumpa jina mtoto, baba akitoa jina unakataa. Hapo u-single mother unakuhusu
2. Una mwanaume zaidi ya mmoja, hapo ikitokea mimba lazima usingle mother ukuhusu.
N.B
Kuna wanawaume walikuwa na nia nzuri tu ila kutokana na ujinga wa mwanamke wamebaki pekee yao.
 
kuna haja kama taifa kuanzisha somo jipya la uzazi tena kwa viboko na adhabu kali mashuleni.
Unafikiri hawajui? Basi tu wadau wanaamua kupotezea. Mfano kwa njia ya kalenda, ME hamuulizi ke kuhusu hiyo kalenda, anapeleka moto mzima mzimaa, na KE muda huo hajali tena liwalo na liwe acha apelekewe moto mzima mzima aenjoy the moment... Matokeo yake ndo hayo sasa. Mtego ni utamu. Na unakuta muda huo wadau hawako tayari kuingia kwenye ndoa. Jambo zito hili watu wa jinsia zote mbili hizo elimu wanazo mkuu. Na njia nyingine za uzazi wa mpango watu wa jinsia zote wanazijua vizuri tu.

Mtego ni utamu na kuwa irresponsible kwa pande zote mbili. Hata uwachape viboko mkuu utaumiza mikono yako tu. Kuna mdau humu huwa anasema "Tatizo binadamu ni wabisi sana".

Watu wamepinda mkuu...
 
Ho
Inakwaza na kufedhesha sana kwasasa kuona kuna ongezeko kubwa la watoto ambao hawajulikani baba zao ni akina nani na hata kama baba wanajulikana basi hawapo katika maisha ya mtoto.

Big up kwa akina baba ambao wanapambania kuwatunza na kuwalea watoto wao wa damu na kuwajibika kama baba na kutowatenga hawa watoto.

Kimsingi baba ni mtu muhimu sana katika maisha ya mtoto na baba anapokosekana katika maisha ya mtoto ni rahisi sana kwa mtoto kupoteza direction ya Maisha utu uzimani.

Mtoto wa kiume unakutana na mdada haujui history yake haumfahamu anaishi kwa mwenendo gani kisa tu kakuruhusu kumpelekea moto unaachia mbegu zako kwenye mji wake wa uzazi ukijua wazi matokeo yake ni yapi.

Hivi huwazii mtoto wako anapozaliwa huyo ndie atakuwa mama yake na wewe ndie baba yake na ndio mwanzo wa familia? Why sasa unaanzisha kitu kikubwa namna hiyo katika hali ya kizembe sana.

Hauoni kuwa unakuja kumpa maisha ya mateso na maumivu huyo mtoto ambaye alitakiwa kukuzwa kwenye maisha ya upendo wa baba na mama na yeye aje kuwa raia mwema?

Je, umemuwazia huyo mwanamke namna atateseka na mtoto huyo usiku pekee yake mchana pekee yake, hapo inakupa fahari gani kama mwanaume kuona damu yako ipo huko na wewe upo huku usijali inaishi maisha ya namna gani?

Kama kwako ni muhimu kuchuja nafaka, si upige hata nyeto au uzingatie ngono salama ambayo haitaleta mtoto ambaye hautakuwa hiyari kumlea kwa upendo?

Hivi unatakiwa uwe na akili ya namna gani hadi kukimbia mtoto wako mwenyewe ambaye hata ukimtazama unajiona kabisa wewe yule pale katika mwili na damu?

Hebu ifike muda tuanze kuambiana ukweli, hawa watoto tunaweza wapata katika mazingira salama na tukawalea. Kama mwanamke ni mkorofi hushindwi kuchukua mtoto wako ukapeleka kwa bibi yake yaani mama yako au ukatafuta mwanamke akusaidie kulea hata beki tatu wapo kibao ambao utamuacha pale room kwako akae na mtoto na wewe umpatie mshahara na akusaidie kuishi na mtoto wako vizuri tu hadi atakapofika umri wa kuanza kujisimamia.

Trust me, mtoto yupo salama zaidi akikua mazingira ya shida pembeni ya baba yake kulikoni akiishi maisha ya shida pembeni ya mama yake ambapo ni rahisi kuharibika tabia na kuwa tatizo ukubwani.

Siku zote linapokuja swala la kulea mtoto huwa wanaume kuna ile tabia ya kujitisha kuwa mtoto atateseka akilelewa na watu baki, huu ni upotoshaji mkubwa sana. Ipo mifano hai ya wanaume waliolea watoto wao wenyewe bila mama wa mtoto kwa msaada wa mfanyakazi na familia yake hadi mtoto kawa mtu mzima, si watoto wa kiume tu hata wa kike.

Inawezekana na nirahisi sana zaidi ya unavyofikiria. Mimi nimeshalea wajomba wawili kwa msaada wa bibi yao na dada wa kazi baada ya kuona upumbavu wa mama zao unavyowagharimu watoto. Ndio maana nauchukia sana usingle mother sababu naelewa madhara na mateso yake kwa watoto wasio na hatia.

Inaanza na wewe kuwajibika na sio kuwategemea hawa mabinti wa sasa ambao hawawajibiki na maamuzi yao. Kama wewe hautatoa mbegu zako kwa mtu ambaye hautaanza nae familia masingle mother watatokea wapi na watoto watapatikana vipi?

Hebu wanaume tuchague kuwajibika na sio kuwa vilaza ambao kwa makusudi tunachagua kushirikiana na wanawake irresponsible kuleta watoto duniani na kuwatesa bila hatia. Hebu tuanze kuwa na maono ya wapi tunapeleka uzao wetu ili tusipoteze mbegu zetu zikaotea mibani.

Utafurahi siku unakutana na binti yako amekuwa mdangaji, kahaba, ana ma'tattoo amekuwa mtu wa hovyo kama akina Giggy money, au Amber Rutty?

Au unakutana na mtoto wako wa kiume amekuwa kituko, kasuka marasta au kaweka dreads, matattoo mwili mzima, kavaa mlegezo, anakimbiza bodaboda halafu wewe ni mtu na heshima zako unapita, unaweza kumrekebisha tena samaki aliyekauka? Ni kazi rahisi sana kujenga kizazi bora kupitia malezi bora ya watoto kuliko kurekebisha taifa na jamii iliyoharibika kwa gharama na program za kuwarekebisha watu wazima ambao wamekomaa kiakili na wameshapinda.

Acheni kuzaa watoto ambao hamna mpango wa kuwalea na kuwatunza kwa upendo kifamilia mnatutesea watoto wasio na hatia na kuleta laana ambazo hazikuwa na nafasi kwenye jamii yetu. Watoto waliopo kwa sasa iwe ni funzo tubadilik
Hao wanawake mara nyingi huwa wanataka wenyewe. Si tulishakubaliana kuwa wanawake huzaa pale wanapotaka na hakuna mtoto wa bahati mbaya kwa kizazi cha kidijitali. Wanawake wengi wanazaa na wanaume wakiwa wanajua kabisa kuwa Hakuna future ila wanazaa kwa sababu
1. Mwanaume handsome
2. Akizaa atapata maokoto zaidi
3. Anataka mwenyewe kuwa single maza (Rejea clip ya kondakta wa taifa)
4. Umri umeenda
5. Akimzalia atakuoa. Nk

Mkuu dunia ya leo siamini tena kama kuna mwanamke anapata mimba bahati mbaya. Labda wale wa vijijini watumia viswaswadu ambao hata JF hawapo
 
Hapana bhna mapenzi yana nguvu

Kumbuka mwanaume anaweza mtamani mwanamke na mwanamke akazama kwenye penzi akiamini kuwa ndiye mume kumbe mwanaume yupo kutimiza haja zake

Na kuna wanaume wana wadanganya wanawake wakibeba mimba atamuoa akibeba tu anachimba zake

Hapo kosa la nan?
Hahaha, aisee hao wa kudanganya ivyo wamevurugwa 😂 😂
 
Uko sahihi mleta Uzi........ila Wanawake wenyewe wanataka kuwa single mother,japo si wote.Binafsi kuna binti niliwahi kuwa naye kwenye mahudiano, nikaona hapa sasa ngoja nioe, kwasababu tulikuwa tumefahamiana vema,baada ya kumwambia nataka kuja kwenu, akasema yeye kwenye maisha hajawahi kuwaza kuolewa,atazaa na kulea watoto mwenyewe hataki kubanwa banwa,nikapiga chini......akazaa na mume wa mtu iringa huko, ghafla akaanza kunipigia na kuomba ushauri kwangu na kukiri hakuwa na maamuzi sahihi kwasababu ni ngumu sana, mtoto alipokuwa kuna mwamba akaingia line akampeleka kwao,jamaa amemzalisha tena na hana habari naye tena japo alitarajia amuoe......kila siku anapiga Simu nimshauri 😀😀.

Pamoja nasisi kuacha mbegu ovyo,ila dada zetu nao baadhi hawaelewi nini wanataka
 
Back
Top Bottom