Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Ushawahi jiuliza siku nitoke vipi? Au kila siku unavaa style moja ya mavazi hadi watu washakuzoea? Sasa kuna hizi dress code tano (5) siku unaweza kuzijaribu.
1. Kuchomekea jeans na shati mikono mirefu.
Hii inakua casual outfit, mfano unaenda kazini au mtoko wa kawaida. Tafuta shati la mikono mirefu, draft au mistari mistari, na jeans lako slim fit, isiwe oversized au ya kubana sana, chini vaa casual shoes.
Kutegemea hali ya hewa unaweza kuongezea na coat.
Hii inawapendeza wanaume wa lika zote, kuanzia vijana, makamo hadi wazee.
Kikubwa ni uchaguzi wa jeans sahihi, na shati liwe simple achana na lenye marangi rangi au maneno ya brands.
2. "Shirt over T-shirt"
Hii nayo nzuri ya weekend. Kwa vijana wa kwenye early au late 20s na 30s.
Tafuta t-shirt inayokufit vizuri, nyeupe au light color yoyote, kisha kwa nje unavaa shati bila kufunga vifungo. Shati la draft au mistari linakupendeza zaidi, na kama possible liwe zito la cotton.
Hii combo inapendeza na jeans ukivalia kwa chini, na angalia pia matching ya rangi ya shati na t-shirt.
Ukivaa hivi tembea kwa confidence na jotahidi sana usibebe bag (backpack) linaharibu muonekano.
3. Traki na T-shirt na raba
Hii ni kwa mitoko ya vijana hadi wazee, ila special occasions kama vile beach, umeenda Taifa kucheki mpira, au weekend flani.
Hapa utavaa track isiokubana sana wala isiwe oversized sana, juu vaa tshirt na raba (au sendo kama utapendelea).
Oversized kama hii sio tamu sana ila kama utaipenda sawa ila kwangu No.
Ukiwa beach kama mwili unaruhusu, unaweza kuvaa na vest, ila usivae mtaani au kutoka nje ya kwako. Utakera watu.
4. Jackets: Denim Jeans au Bomber?
Kama hali ya hewa inaruhusu, jaribu kua na moja wapo ya aya makoti. Yanaenda na nguo za aina nyingi sana.
Mfano, Denim Jeans jacket zinaenda na t-shirt na jeans za rangi mbalimbali, ila usivae full jeans. No.
Bomber jackets aka Flight jackets pia zinaweza kukufanya upendeze.
Kwenye majacket, angalia halia ya hewa na nguo autakayovaa kwa ndani na chini. Usijitese na makoti wakati kuna hali ya hewa ya jua kali.
5. Jaribu kuvaa saa.
Hapa ata nisiongee sana, ila uwe angalau na saa pair mbili au tatu. Chronograph ya mikanda ya chuma na ya ngozi, na smartwatch au kimulimuli kimoja. Tosha.
NB:
Usiangalie wa online ndio ukaiga walivovaa, tunatofautiana maumbo, urefu na rangi. Utatoka kama zombie.
Ukivaa vaa kiume, mtu akikuona tu anajua yule ni mwanaume.
Usioverdress, usivae nguo nyingiii na zisio na maana.
Na mwisho, ukiamua kuvaa like crazy, uwe crazy kwelikweli, ila kwenye special occasions.