Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Wanaume kuweni makini sana kuoa wanawake waliotoka Vyuoni

Ni vizuri na busara sana kuwa na akiba ya maneno. Usiwaone hao wanaochukua hayo maamuzi kuwa ni wajinga! Bado tu hujabananishwa!

Unaingia mzima mzima unajitoa unahudumia, unasomesha mpaka wewe unajisahau halafu mkeo anakuja kuanza kukudharau na kuchezewa na majamaa waziwazi. Kama huna kifua au support system nzuri linaweza kutokea la kutokea.
Ntakaa kinyonge ila sio kujiua aisee, nmepitia changamoto nyng sana na nimevuka sembuse kuachwa?
 
Tuepuke kuoa mwanamke mwenye X....Tena ukute Ex mwenyewe waliachana sababu jamaa hajajipata au kwa kuwa umetokea mwenzangu na Mimi una vihela vyako umeahidi kuhudumia vizuri....Kuna bro wetu ishawahi mtokea hii,yule dada waliachanaga na ex wake kwa kuwa dada ake alikuwa anampa presha adate na mwanaume mwenye pesa waikomboe familia so kweli demu akampata bro baada ya Dem kujipata vizuri akawa anakodi hotel anaenda kukutana na ex wake😭
 
Kwanza naomba nitoe pole kwa familia ya mtoa mada kwa haya mazito yaliyoikumba familia kwakweli watu wema wamekuwa wakiangamia sana kwa kutokujua nn wanalolifanya na hii imesababushwa na wengi wetu kukosa subira ,maono na kushindwa kuomba ushauri kwa ndugu,marafiki au majirani ili kupata msaada wa kile unachokifanya kwa wakati huo,
Wengi wetu tumekuwa na maoni ya muda mfupi sana bila kujua haya ni maisha yako na mtu unayehisi ni mpenzi wako ndo utaenda kuishi nae ........hivyo basi ukifanya kosa tegemea majuto maisha yako yote.
Vijana wenzangu wakati umefika pale unapohisi kwamba uyu ni mtu sahihi....tujitahidi kushirikisha vijana wenzetu/ ndugu/marafiki hii itasaidia kupata kilicho Bora zaidi na kupunguza vifo kwa vijana vinavyosababishwa na stress.
 
Kijana unataka kuoa tafuta darasa la saba sogea sogea mpaka form four or six weka ndani kula maisha,usicheze na hao wacheza porn kwa kigezo cha kusaidiana maisha siku akipata kazi
Mimi nakuelewa sana Mkuu

Kuna jamaa yangu ni Daktari kabisa alioa Mhasibu msomi wa chuo kikuu wakazaa mtoto mmoja na tumemchangia kabisa kwny shughuli yake...juzi akaoa binti mdogo aliyeishia Fm IV

Ukimuuliza kulikoni? Anasema ameamua kumuoa Mwanamke anayemsikiliza na sasahivi ana amani tele

Kuna Wanawake wasomi hawafai kabisa kiukweli though sio wote
 
Kitu ambacho wanaume wengi hamkijui ni Tabia za mwanamke ambae Anajitafuta au ana hali ngumu kimaisha huwa ni kama simba jike mwenye njaa kali so chochote kitakachotokea mbele yake kama kimenona anapita nacho, Maisha ya Binti alietoka Chuoni hana kazi wala Pesa huwa ni kama Wife Material full adabu na utii

Ndio hawa wanawake wa vyuoni au waliomaliza na ajira hawana, simaanishi kuwa hawana haki ya kupata wenza ila uwe makini sana kuwasoma kabla ya kuwaowa, Hao wakishaolewa huwa wanaendelea kuhaso kutafuta ajira sasa usiombee atume maombi alafu ukute upo nae Dar alafu uskie kapangiwa kituo cha kazi Dodoma huko or Mwanza au apate kazi ya maana ukiwa nae hapo ndio utaanza kujua tabia zake halisi

Mwaka 2017 nilimpotezaga kaka yangu, alikipenda kibinti kikiwa mwaka wa pili chuoni akawa anakihudumia,hadi kinamaliza Chuo akakiowa bwana ila kwenye uchumba tu ugomvi ulikuwa hauishi maana kulikuwa na Tetesi yule binti alikuwa na mpenzi wake wa zamani kwa siri ila kilichompeleka pale kwa Bro ni pesa

Kaka akaowa kibishi, Ndoa iko Mwaka wa kwanza tu, Binti akala shavu Kigoma huko shirika linalodeal na wakimbizi pesa nje nje, Ndoa ndio ilipoanza kuwa ndoano hapo maana ilikuwa ni Marufuku kaka kumfuata yule Binti kigoma hadi arudi yeye Dar hao ni wanandoa yani

Za chini chini wambea wakamtonya Kaka kuwa yuke Binti huwa anamsafirisha yule Mwanaume wake wazamani hadi kigoma anafikia kwake mara kwa mara na anamrudisha Dar tena kwa Ndege, Na ndio maana Binti hakutaka kaka Awe anaenda kigoma

Kaka mwaka 2016 mwishoni akanywa sumu ila aliponyea kufa yote ni kama alipata sonona ,akawa hana mtu wa kumwambia, Baada ya lile tukio ndio akaipa Familia ukweli sasa, familia ikaweka kikao yule Binti akaitwa ila akasema yupo Bize Kigoma huko yote jeuri ya pesa na pumzi

Ikabidi sisi kama familia sasa tuongeze ukaribu uliopitiliza, ili ile hali iondoke tukawa tunakaa kwake kwa zamu yote kumpa kampani maana tulishaona Dalili mbaya na ndio tulikuwa tunamtegemea yani wadogo zake ametusomesha na kutupigania sana, Wifi tukawa tukimpigia simu hata kupokea hapokei

Mwaka 2017 mwezi wa Sita akaanza kuugua vitu visivyoeleweka mara Presha mara anadondoka kazini, Alipopelekwa Hospitali kwa uchunguzi ikaonekana Mishipa yake ya moyo imeanza kutanuka tukaambiwa anatakiwa arelax na aache kuwa mtu wa Mawazo , ila kila tukijaribu ikawa mtihani, 2017 mwishoni akafariki alidondoka tu bafuni kumkimbiza Hospitali tayari akawa ameshaondoka hili pigo siwezi kulisahau

Baada ya hili tukio kutokea Baba nae hadi leo hajawahi kuwa sawa kabisa, ila aliwaita watoto wake wote wa kiume kitu nachokumbuka alisema oweni wanawake wenye elimu za kawaida msije kusumbuana huko mbele, na akasema tumewasomesha kwa garama kubwa na sasa mna kazi zenu yeyote atakaeleta tena Mwanamke hapa kama ana Elimu ya juu basi huyo Mwanamke naye ni Sharti awe na pesa na kazi kabla hamjafahamiana yaani kiwaunganishe upendo sio Pesa mlizokuwa nazo

Akasema kuwa ukiniletea hapa Mwanamke Mwenye elimu ya juu na hana kazi wala pesa basi mkatafute baba mwjngine ampokee huyo mwanamke kama mnae la sivyo aishie huko huko, yaani Baba ni kama alivurugwa na ile hali

Ila wansemaga Dam ya mtu ni kama nzito or inaweza kukulilia ila sijui kama ni kweli but yule Binti mwaka 2022 Tabora huko, alipataga ajali mbaya sana Gari aliyokuwa anaendesha ikagongana na lori miguu yote ikabanwa mean ikasagika akakatwa miguu yote kwa sasa ni mlemavu kabisa hana miguu.
Wa bongo mnasumbuliwa Sana na ngono, yaani unaogopa binti wa chuo! Unaogopa kukimbiwa na mchumba!
Sasa wewe unaweza kukabiliana na mishe za ku tafuta pesa ndefu(sio za kununua ka IsT na ku Jenga nyumba ya vyumba vitano), namaanisha ku tafuta mkwanja mrefu utoe ajira, kwa, ndugu na jamaa, kama watu 60+,
Ndio maana mjini vichaa wengi, wengi wanavurugwa na mapenzi!
Bro wanawake ni wengi Sana, hata huko vyuoni wapo wazuri tu,
Hata kitaani wale walioishia LA, Sana wapo vicheche, wanatamani simu na chips kuku, na lift, I speaks from experience, nimewala wengi Sana,
 
nimejalibu kusoma hii story yako na kuvaa viatu vya baba ako mzazi...binafsi alipitia maumivu makali sana na imeniuma sana poleni sana ,mchumba hasomeshwi na mke pia sizani kama ni sahihi kusomeshwa... pesa ya kumsomesha mke ni bora mfungue biashara....
Msomeshe mfungulie biashara kama ni mama watoto wako hata akikuacha atakula na wanao
 
Tatizo mnaoa wake za watu kwa kuwavuta na ulimbo(pesa)..

Pole kwa binti, ila mabinti wakianza kukufanyia visa huwa hawarudi nyuma utasanda tu.
Sometimes kuchepuka ni muhimu, kaka yenu mngemsogezea mali safi nae awe anajichapia mdo mdo, sasa mnaenda nyie wadogo zake afanye nini na nyie??
 
Back
Top Bottom