Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bila ya shaka miguu yake ipo busy Kigoma, Duh wahuni nyie hamkumpa jini lakini🤣🤣🤣Alikuja tena uso mweupe ila kwa sasa ni mlemavu hana miguu miwili yalimkuta makubwa Dam ya mtu nzito sana
Elimu kubwa ni kuanzia ngapiNa hadi leo Baba aliwaasa kaka zangu na wadogo zangu wa kiume akasema oa mwanamke mwenye elimu ya kawaida wanawake wenye elimu kubwa ndoa kudumu mtihani aisee niliamini
😂😂😂😂😂😂😂....daaah we jamaamke wangu alinambia nimsomeshee eti nimpeleke chuo akasome nlicheka mpka nkapaliwa...
Bado yupo busy kigoma au ?Alikuja tena uso mweupe ila kwa sasa ni mlemavu hana miguu miwili yalimkuta makubwa Dam ya mtu nzito sana
1. Je kwa muda alokaa naye hakumpiga mimba???Alikuja tena uso mweupe ila kwa sasa ni mlemavu hana miguu miwili yalimkuta makubwa Dam ya mtu nzito sana
Kilimtokea kitu gani?Alikuja tena uso mweupe ila kwa sasa ni mlemavu hana miguu miwili yalimkuta makubwa Dam ya mtu nzito sana
Alipat ajali akakatika miguu yote 2Bado yupo busy kigoma au ?
Nimeshamjua isee hii dunia ni ndogo sana.Alikuja tena uso mweupe ila kwa sasa ni mlemavu hana miguu miwili yalimkuta makubwa Dam ya mtu nzito sana
Kumbe ndg yangu ww ni JIKE/KE? Wow...😍Ni kweli kabisa, mimi kuna mwanamme kanizidi miezi 7, kamaliza chuo anajitafuta na shughuli za hapa na pale, tupo wapenzi nashangaa ananisalimia, namuona kama tapeli tu, kwasababu hapo akipata kazi lazima aende kazini kwake, na najua hakuna ndoa ya mbali.
Umesahau kuswitch akaunti mkuu 😂Ni kweli kabisa, mimi kuna mwanamme kanizidi miezi 7, kamaliza chuo anajitafuta na shughuli za hapa na pale, tupo wapenzi nashangaa ananisalimia, namuona kama tapeli tu, kwasababu hapo akipata kazi lazima aende kazini kwake, na najua hakuna ndoa ya mbali.
Karma 👏👏👏❤️❤️❤️Alikuja tena uso mweupe ila kwa sasa ni mlemavu hana miguu miwili yalimkuta makubwa Dam ya mtu nzito sana
Tatizo ni huyo dada kupata deal la kazi mapemaa! Unadhani angekula msoto wa mtaa angeweka hii jeurii?Ndio shida ya kudharau red flags,,,kaka yako toka awali alishaona hapa kuna mushkeli lkn akakaza fuvu kwamba akisha muoa atakuwa amesolve tatizo na hapo ndipo shida ilipoanzia
Always kuwa makini sana na small details
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bila ya shaka miguu yake ipo busy Kigoma, Duh wahuni nyie hamkumpa jini lakini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Huyo kaka yako boya sana,pole lknKitu ambacho wanaume wengi hamkijui ni Tabia za mwanamke ambae Anajitafuta au ana hali ngumu kimaisha huwa ni kama simba jike mwenye njaa kali so chochote kitakachotokea mbele yake kama kimenona anapita nacho, Maisha ya Binti alietoka Chuoni hana kazi wala Pesa huwa ni kama Wife Material full adabu na utii
Ndio hawa wanawake wa vyuoni au waliomaliza na ajira hawana, simaanishi kuwa hawana haki ya kupata wenza ila uwe makini sana kuwasoma kabla ya kuwaowa, Hao wakishaolewa huwa wanaendelea kuhaso kutafuta ajira sasa usiombee atume maombi alafu ukute upo Dar uskie kapangiwa Dodoma huko or Mwanza au apate kazi ya maana ukiwa nae hapo ndio utaanza kujua tabia zake halisi
Mwaka 2017 nilimpotezaga kaka yangu, alikipenda kibinti kikiwa mwaka wa pili chuoni akawa anakihudumia,hadi kinamaliza Chuo akakiowa bwana ila kwenye uchumba tu ugomvi ulikuwa hauishi maana kulikuwa na Tetesi yule binti alikuwa na mpenzi wake wa zamani kwa siri ila kilichompeleka pale kwa Bro ni pesa
Kaka akaowa kibishi, Ndoa iko Mwaka wa kwanza tu, Binti akala shavu Kigoma huko shirika linalodeal na wakimbizi pesa nje nje, Ndoa ndio ilipoanza kuwa ndoano hapo maana ilikuwa ni Marufuku kaka kumfuata yule Binti kigoma hadi arudi yeye Dar hao ni wanandoa yani
Za chini chini wambea wakamtonya Kaka kuwa yuke Binti huwa anamsafirisha yule Mwanaume wake wazamani hadi kigoma anafikia kwake mara kwa mara na anamrudisha Dar tena kwa Ndege, Na ndio maana Binti hakutaka kaka Awe anaenda kigoma
Kaka mwaka 2016 mwishoni akanywa sumu ila aliponyea kufa yote ni kama alipata sonona ,akawa hana mtu wa kumwambia, Baada ya lile tukio ndio akaipa Familia ukweli sasa, familia ikaweka kikao yule Binti akaitwa ila akasema yupo Bize Kigoma huko yote jeuri ya pesa na pumzi
Ikabidi sisi kama familia sasa tuongeze ukaribu uliopitiliza, ili ile hali iondoke tukawa tunakaa kwake kwa zamu yote kumpa kampani maana tulishaona Dalili mbaya na ndio tulikuwa tunamtegemea yani wadogo zake ametusomesha na kutupigania sana, Wifi tukawa tukimpigia simu hata kupokea hapokei
Mwaka 2017 mwezi wa Sita akaanza kuugua vitu visivyoeleweka mara Presha mara anadondoka kazini, Alipopelekwa Hospitali kwa uchunguzi ikaonekana Mishipa yake ya moyo imeanza kutanuka tukaambiwa anatakiwa arelax na aache kuwa mtu wa Mawazo , ila kila tukijaribu ikawa mtihani, 2017 mwishoni akafariki alidondoka tu bafuni kumkimbiza Hospitali tayari akawa ameshaondoka hili pigo siwezi kulisahau
Baada ya hili tukio kutokea Baba nae hadi leo hajawahi kuwa sawa kabisa, ila aliwaita watoto wake wote wa kiume kitu nachokumbuka alisema oweni wanawake wenye elimu za kawaida msije kusumbuana huko mbele, na akasema tumewasomesha kwa garama kubwa na sasa mna kazi zenu yeyote atakaeleta tena Mwanamke hapa kama ana Elimu ya juu basi huyo Mwanamke naye ni Sharti awe na pesa na kazi kabla hamjafahamiana yaani kiwaunganishe upendo sio Pesa mlizokuwa nazo
Akasema kuwa ukiniletea hapa Mwanamke Mwenye elimu ya juu na hana kazi wala pesa basi mkatafute baba mwjngine ampokee huyo mwanamke kama mnae la sivyo aishie huko huko, yaani Baba ni kama alivurugwa na ile hali