Acha kulalanika hovyo, sababu ni ninyi wanawake wenyewe mlioolewa. Mfana mimi binafsi, nikikurupuka ile kumi na mija kamiki, dadaa keshaamka na kuanza usafi, maji ya kuoga kashanitengea wife kalala, nimirudi jioni akiniona tu anatenga maji ya kuoga, wife pengine yupo jikoni au pengine pasipo na umuhimu kunizidi, chakula kikiwa tayari dadaa akinitengea na kunikaribisha juu, wife yeye huita tu mtoto, chukua chakula mpelekee babaa, nikimaliza kula, dada anatoa vyombo fasta na kuniletea maji ya kunywa na kunawa, wife yupo tu. Sasa najiuluza je huyu dadaa ndio akitakiwa kuwa wife? Mahaba yanajijenga mdogomdogo, hata kama ni kabaya lakini ile care yake inanivutia, inabidi nimlipe fadhila tu basi afurahi na yeye.