Kabakabana
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 5,550
- 1,165
- Thread starter
- #141
Kisa chako si cha ajabu kufanywa na baadhi ya wanaume na hata baadhi ya wanawake. Lakini kuuliza "Wanaume mna tatizo gani?" ni kuwachanganya wanaume na hata wanawake wote katika kapu moja.
Katika kuzungumzia "urafiki baina ya wanaume na wanawake", wengi hapa walikuja na wazo kuwa "kitu hicho hakiwezekani", wanaamini ama mnakuwa wapenzi au kila mmoja kivyakevyake; [jambo ambalo mimi ninapingana nalo]. Urafiki baina ya mwanamume na mwanamke unawezekana, cha muhimu ni kuweka mipaka tangu mwanzo, jambo ambalo wewe ulifanya kwenye 1. nyekundu la kumpa nambari ya simu lakini ukakosea zaidi kwenye 2. nyekundu kwa kumfanya rafiki mtu ambaye ulijua kuwa alikuwa hakutaki kama rafiki tu.
Na hiyo 3. nyekundu bado nina mashaka kuwa "rafiki yako" kwa maana ya rafiki anafika hadi anaolewa ukiwa hujui bwana arusu ni nani. Lakini hayo yote ni maangalizo tu, ninachotaka kukushauri, kama walivyo kushauri wengine, kwa heshima ya huyo "shoga yako", achana kabisa kabisana huyo fataki na hata na shoga yako. Kuwa kwako karibu na shoga yako ni sawa na kuwa karibu na huyo jamaa.
wewe ni mtu wa kwanza kwa kunielewa,nakushukuru sana.
Mimi nilikuwa busy na mbali kwa muda, kwahiyo hata sikuwaza mambo ya kuuliza bwana harusi ni nani.