Najua hamtanielewa ila mwenzangu.
Wonderful na akina
atoto watanisaidia hapa kuwatoeni huko.
Kipindi hiki cha uchaguzi hakika nimegundua wanaume mnapenda vya bure sana. Baada ya uchaguzi kuisha mmekuwa ni watu wa kulalamika.
Kulalamika kwenyewe mnalalamika elimu bure,milo mitatu bure, hadi kufika hatua mnasema kuoa itakuwa ngumu,mimba kukataliwa zitaongezeka,Wanaume ni mmelogwa ama? Ni nini hiki mnashadadia vitu vya bure?.
Halafu bila aibu unajiita kamanda, unajua maana ya kamanda?.
Ulipokuwa unazaa watoto wako hukujua itafika siku watahitaji kusoma,hukujua iko siku utataka kuoa then ujipange?
Mungu katubariki Tanzania kuna opportunity za kumwaga,mwanaume unashindwa kuchangamkia fursa?.
Tuna ardhi nzuri mwanaume unashindwa kujikita kwenye kilimo mashamba yenyewe kijijini kukodi kwa mwaka hadi kwa buku kumi unapata?!
Tangu juzi mmekuwa ni watu wa kuandika vitu visivyo na kichwa wala miguu kwenye mitandao kulialia wakati wanawake wako busy kuchakarika na biashara zao.
Mwanaume mzima kweli unalialia? Unasahau uliambiwa utakula kwa jasho?.
Kuna mwingine akasema nahama Tanzania kweli? kisa umekosa vya bure sasa ndo unapata akili ya kuhama nchi wakati hapo mwanzo hata siku moja hukuwahi kucheki nchi gani ya nje ina opportunity ukachakarike huko?.
Serious Wanaume mmekera sana kipindi hiki cha uchaguzi.Mi nilitegemea mabadiliko ambayo yangewasikitisha kuyakosa ni Sera za Act wazalendo sasa mnasikitika milo mitatu? elimu bure?, afya bure,
HEBU WANAUME FANYENI KAZI.