majoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 2,595
- 4,775
Nimefanya utafit mdogo tu humu nimegundua wanaume mnalalamika sana kuhusu wanawake kuwaomba pesa, kuwapiga mizinga, kutotosheka na mnachowapa na mengine kibao. Jamani eee hebu acheni kulalamika kwa kuwa hayo mmeyataka wenyewe. Unatafuta mwanamke ili uwe unamwaga grisi chafu hapo na unataka akuhurumie asikuombe chochote! Haiwezekani hata kidogo. Wewe kama unajiona unahitaji mwanamke kwa nini huoi? kwa nini usimchukuwe jumla? muweke ndani maisha yaendeleee....Lakini hii biashara ya malalamiko yasiyo ya msingi humu tumeichoka! Acha wawapige mizinga hadi mtie akili na kutafuta ufumbuzi ambao ni wa kubeba jumla. Hamjifunzi wa baba zenu? hamuoni wametulia na mama zenu?
Tofauti na hivyo mtaishia kulishwa malimbwata, kudharauliwa, kupoteza muda kuwaza maumivu ya kutendwa badala ya kuwaza na kupanga maisha. Ukweli ni kwamba simhurumii hata kidogo mwanamume anayepigwa mizinga! Pigweni tuuuuuuu.... good day kwa wapigwa mizinga wote