Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Moja...Wake zetu na mademu zetu wakikutana kwenye vicoba wanaliwa sana na wakopeshaji , wasiwasi ni kwamba je, na wanaume wanaliwa au wanafanyaje huko?


Pili...Vicoba vinapandikiza umbea sana kwa wanaume ndiyo maana sasa hivi huwezi tofautisha wanaume wa kwenye vicoba na wanawake wa vibarazani.


MWANAUME KUCHEZA VICOBA NI TABIA ZA KIKE
 
Mimi nacheza VIKOBA kwani kuna shida gani. Tunajifanya jeuri tu za kipumbavu. Yaani Kwa sababu za ajabu niache VIKOBA nakopa Kwa asilimia tano, niende benki nikakope kwa asilimia kumi na tano. Tuheshimu ushirika ni muhimu sana.
 
Uko vizuri mkuu watu wana mitazamo hasi tu ya VIKOBA. Mimi na watumishi wenzangu tisa tulikaa tukawaza tukaona hatutoboi na mikopo ya benki, mtu unakopa 20mil unalipa 30mil. Tukaona hapana, tukajiunga tukaweka, tukasajili kikundi ustawi wa jamii na tukaweka lengo la kukusanya 12 mil Kwa mwaka wa kwanza. Hivi ninavyoongea mwaka wa tano tunaelekea 100 mil. Hakuna kwenda benki tena.
 
JF nzima wew ni mmoja kati ya Watu ambao huwa Anamjibu Mtu/kumuelekeza kwa Facts,

Nakuheshimu sana Bro Kazi nzuri Dr Matola PhD
 
Naomba kujua mkuu.. hii ina tofauti gani na kufungua fixed akaunti alafu uwe unaweka hela wewe mwenyewe tu then unaenda kuwithdraw baada ya muda uliopanga?
 
Naomba kujua mkuu.. hii ina tofauti gani na kufungua fixed akaunti alafu uwe unaweka hela wewe mwenyewe tu then unaenda kuwithdraw baada ya muda uliopanga?

Naomba kujua mkuu.. hii ina tofauti gani na kufungua fixed akaunti alafu uwe unaweka hela wewe mwenyewe tu then unaenda kuwithdraw baada ya muda uliopanga?
Haina tofauti kubwa ila fixed unawekeza kwa mkataba tuseme miaka 2 au 3 na unapata faida kidogo
Sasa mimi hiyo faida ndio siitaki na credit cards ninazo ila kwa mfano nikilipia huduma ya gari kama petrol au shopping zangu kabla ya riba tu yaani mwisho wa mwezi nalipa haraka

Natumia credit card kwa sababu ina guaranteed kama nikilipia kwa matapeli
Hii ninayotumia kwa kuchanganya na wenzangu ni wakati nahitaji hela ndefu kwa mara moja ambapo naweza kupewa mtu wa pili au wa 3 na kufanya jambo haraka

Riba ndio naikimbia hapo sio kingine ingawa kuna Bank hapa zinafuata sharia
 
Ngoja nitarejea vizuri nikae darasan.. halafu kumbe ni tofauti na upatu
 
Hongereni sana wakuu. Watu wanachanganya tu mambo kwa uelewa wao mdogo. Hivi vikundi vya upatu ni shida. Mikopo ya benki na hizi Microfinance ni sumu ya maendeleo. Mimi nilikopeshwa na Microfinance 15m kwa riba 20% kwa muda wa miezi 6 karibia nikimbie nchi. Biashara iliyumba kidogo mambo yakawa magumu kuanzia rejesho la 4. Dada yangu ndo aliniokoa kwa kunipa mchongo wa Vicoba. Ilinisaidia sana kumalizana na majamaa.
 
Hapo kwenye bold🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…