Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Shunie umetoa somo zuri, kama mtu hajaelewa ndio basi tena. 2017 hadi 2020 nilifaidi hiyo kitu kupitia wife, sikuwahi kwenda, sikujua hata nani ni nani huko, wife alikuwa na majina mawili, kukopa kwa riba nafuu kabisa, unakuwa mtu wa tight budget manake unajua kila mwezi/wiki lazima rejesho na hisa utoe.

Ila kikivunjwa, wife akikuletea maokoto ndio unaiona faida yake.
 
Vicoba nilikua navidharau,ila mwaka Jana vimeniiokoa Sana, shukrani kwa wife.
Mwaka huu nimenunua gunia 10 za mahindi kupitia vicoba, Kuna mtu alikuwa anauza na sikuwa na fedha.
Vicoba wakasababisha fasta.
Nilichojifunza mwaka huu ni kutosikiliza au kuchukua ushauri kutoka kwa online strangers ambao hata yakikukuta hawatakwepo kukusaidia.
 
Huyu mzee wangu yupo vizuri mno ndiyo maana hata nikikutana naye kwenye majukwaa ya michezo naogopaga hata kujibizana naye kwa kejeli maana aliyekuzidi kakuzidi.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Yah kabsa Anakujibu kw Facts had unakosa Upinzani wa kuendelea mwshoe unahamia kumbishia mwngne
 
Hata nyinyi bado mnafanya mambo kienyeji.

Ukifuata vizuri system ya Vicoba dhamana ni akiba yako pamoja na wadhamini ndani ya kikundi kama ni Wawili its okey.

Vicoba hausiki na mambo ya kuchukuwa vitu vya mtu Nyumbani, mnachanganya haya mambo na kujitungia taratibu badala ya kufuata muongozo wa Vicoba.

Labda ili unielewe vizuri Mimi nikiwa na shida Nina watu wa aina mbili ambao wananiamini, wa kwanza atanikopesha kwa riba bila dhamana yoyote, na wa Pili ananikopesha cash bila riba wala dhamana yoyote, sasa jiulize upo kwenye Vicoba ukope kwa dhamana hiyo Vicoba ina faida gani au ya kazi gani?

Nilichokigunduwa Mimi kwenye Uzi huu inawezekana kabisa kinachoendelea mtaani kwa sehemu kubwa siyo Vicoba Bali ni remix ya upatu, kausha damu na Vicoba na hapo ndio kwenye confusion jamii kubwa haielewi kinachoendelea.

Mimi nikipata muda wa kujitolea bure kuwafundisha watu wa vikundi village community bank ni nini ni lazima wafike mbali na wote lazima wawe na bima za afya na kikundi lazima kiwe na asset za kuingiza faida na Kikoba huwa hakivunjwi kugawana pesa ila unaruhusiwa kujitowa na mchanganuo wa pesa utazopewa uko wazi kwa muongozo wa Vicoba.

Kwa kifupi nawashauri wenye Vicoba waviendeshe kwa mfumo wa Vicoba Endelevu, na kama kwa mwaka mgao wa pesa uwe wa hisa na uwekezaji.
 
Kama wanapata manufaa kwann wasicheze. Ukute anaewasema vibaya na yeye hana kitu anafanya zaidi yupo kwa shemeji analelewa na ugali wa bure
 
Una jambo Dr Matola, PhD holder. Utafika mbali mkuu[emoji1787][emoji1787]
Elimu nzuri mnawapa watu, wasije kuishia kusema ooh hiki cha kike, hiki cha kiume, hiki hakifai...
 
Mimi mwanaume na mwakani tunavunja kikoba chetu,nina akiba ya kupata kiwanja huko nikipata tu nanunua kiwanja kikubwaaaa.
 
Hawa matrafiki wa mjini wanacheza vikoba kwa week anapokea mtu million 3 hizo hela wanawakamua hawa boda boda na hizi gari za mjini
 
Vicoba Kama vicoba ni vizuri Kwa wanaojitambua.

Ila Kibongobongo mwanaume kushiriki vicoba naona haijakaa poa, maana ukiachana na masuala ya akiba pia Kuna umbea Sana Kwa wahusika.

Kwaiyo sidhani Kama ni sahihi Kwa jinsia me.
Hakuna mtu aliyeendelea kwa vikoba kwasababu 90% zile zinakuwa sio pesa za halali ni pesa za dhulma wengi wanapata katika njia isiyofaa
 
Kuna mmoja juzi kaniambia yuko kwenye chama nikajua chadema wako mjini kumbe ndo vikoba
 
Hawa matrafiki wa mjini wanacheza vikoba kwa week anapokea mtu million 3 hizo hela wanawakamua hawa boda boda na hizi gari za mjini
Hao traffic wanacheza upatu siyo Vicoba.

Upatu unaweza kuendesha hata kwa group tu la WhatsApp, Vicoba ni physical activities.
 
Hao traffic wanacheza upatu siyo Vicoba.

Upatu unaweza kuendesha hata kwa group tu la WhatsApp, Vicoba ni physical activities.
Mkuu Unaweza kupata muda ukaweka chapisho moja la ABC ya hivi vikoba .. ili itusaidie tujue wapi tushike halafu tukamua wenyewe, ikikupendeza wa kibali chako inawasiliishwa
 
kupanga ni kuchagua,

Kuna mdada anacheza kikoba kwa niaba ya mumewe,mumewe ni afisa,,,,,,,aisee


One day yes[emoji1317]
mawardat, mwanamke mwenyewe ndo wewe,kwamaana siyo kwa unyenyekevu huo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…