Hata nyinyi bado mnafanya mambo kienyeji.
Ukifuata vizuri system ya Vicoba dhamana ni akiba yako pamoja na wadhamini ndani ya kikundi kama ni Wawili its okey.
Vicoba hausiki na mambo ya kuchukuwa vitu vya mtu Nyumbani, mnachanganya haya mambo na kujitungia taratibu badala ya kufuata muongozo wa Vicoba.
Labda ili unielewe vizuri Mimi nikiwa na shida Nina watu wa aina mbili ambao wananiamini, wa kwanza atanikopesha kwa riba bila dhamana yoyote, na wa Pili ananikopesha cash bila riba wala dhamana yoyote, sasa jiulize upo kwenye Vicoba ukope kwa dhamana hiyo Vicoba ina faida gani au ya kazi gani?
Nilichokigunduwa Mimi kwenye Uzi huu inawezekana kabisa kinachoendelea mtaani kwa sehemu kubwa siyo Vicoba Bali ni remix ya upatu, kausha damu na Vicoba na hapo ndio kwenye confusion jamii kubwa haielewi kinachoendelea.
Mimi nikipata muda wa kujitolea bure kuwafundisha watu wa vikundi village community bank ni nini ni lazima wafike mbali na wote lazima wawe na bima za afya na kikundi lazima kiwe na asset za kuingiza faida na Kikoba huwa hakivunjwi kugawana pesa ila unaruhusiwa kujitowa na mchanganuo wa pesa utazopewa uko wazi kwa muongozo wa Vicoba.
Kwa kifupi nawashauri wenye Vicoba waviendeshe kwa mfumo wa Vicoba Endelevu, na kama kwa mwaka mgao wa pesa uwe wa hisa na uwekezaji.