Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Kama unahitaji hela ya kufanyia kitu haraka nafikiri hii ni njia salama kwa wasioamini Riba
Unachukua unafanyia wazo lako halafu unaendelea na mengine
Ila nasema tu kama una shida ya haraka ni salama zaidi haina riba
Hebu elezea vizur mkuu ni mnazikusanya halaf mnakopeshana? Maana ukisema mnakua mnachangiana ni mzunguko wa mwezi had mwezi sasa hela yakufanyia kitu haraka inakuaje hapo au mfano mpo sita na wewe ni wa sita si unasubiri hadi ufikiwe? sasa kusubiri ufikiwe si ungezitunza mwenyewe tu kwa nidham. Kuliko risk za huko maana wabongo tunajuana, Au mimi naelewaje?
 
Nawaza Hapa,

1. Hivi mwanaume unapata wapi ujasili kucheza kikoba Kama wanawake? Lengo lako Ni Nini hasa? Unajiskiaje kwa mfano.

2. Tena wengine utashangaa kabisa, anakuaga hadharani mwanaume mwenzie kua Anaenda kwenye kikoba! Unabaki unamwangalia Mara mbili mbili humpatii picha.

3. Hivi wanaume wanaocheza vikoba, nao upitia Changamoto kama hizi wanazopitia dada zetu na mama zetu ktk kusaka pesa za marejesho ya vikoba kila baada ya siku kadhaa za wiki au mwezi?
View attachment 2742195
Wewe endelea kumsikiliza oscar,huyu jamaa kwanza kwa mim namchulia km mlopokaji,kila nikikuta kaweka kibwagizo chake waga najifikilia Sana juu ya reasoning yake,wewe fanya chochote unachoamini kitakufanya ufikie malengo bila kuvunja Sheria za nchi
 
Vicoba ni nini?

Vicoba ni Village community bank.

Kwahiyo ukielewa maana ya Vicoba hakuna tatizo lolote kwa mwanaume kushiriki.
Bado maana peke yake haitoshelezi kumfaa mwanaume acheze kikoba.

Kwanini mwanaume ucheze Kikoba?

Unashurutika hadi kulipa faini ukichelewa, hela ya faini ambayo hata haiwekwi kwenye akaunti yako nawe unaona fresh?
 
Nawaza Hapa,

1. Hivi mwanaume unapata wapi ujasili kucheza kikoba Kama wanawake? Lengo lako Ni Nini hasa? Unajiskiaje kwa mfano.

2. Tena wengine utashangaa kabisa, anakuaga hadharani mwanaume mwenzie kua Anaenda kwenye kikoba! Unabaki unamwangalia Mara mbili mbili humpatii picha.

3. Hivi wanaume wanaocheza vikoba, nao upitia Changamoto kama hizi wanazopitia dada zetu na mama zetu ktk kusaka pesa za marejesho ya vikoba kila baada ya siku kadhaa za wiki au mwezi?
View attachment 2742195
Wengi ni upinde
 
kuna wanawake wanadharau wanaume wacheza vicoba
Wanawake wanadharau wanaume wasiokuwa na pesa.

Miaka ya 90's Jiji la Dar ndio lilianza kupokea vijana wa kimakonde kutoka mikoa ya kisini na ndio wakaasisi jina la Wamachinga.

Nakumbuka Wamachinga wa mwanzo kwa sisi Watoto wa Dar tuliwaona kama mafala Fulani kwa biashara walizofanya kumbe walipiga sana pesa na Watoto wazuri mtaani wakawa wanawapenda wao kwa sababu wana pesa sisi tuna sound za uzawa tu kumbe ujinga mtupu.

Inawezekana wengi hawana elimu ya village community bank au hata hao washiriki huenda baadhi yao hawana uelewa wa namna ya uendeshaji wa Vicoba, kuna vicoba aina mbili Vicoba Endelevu na Vicoba vya kuvunja.
 
Sijawahi kufikiri kama ndugu Deep Pond nawe una fikra kama hizi. Village Community Bank (VICOBA) ina tatizo gani? Au ulimaanisha upatu? Vicoba viko karibu nchi zote za SADC & EAC na imeonyesha mafanikio makubwa. Tatizo kwa hapa nchini utakuta havijasajiliwa na havina utaratibu unaoeleweka. Arusha Club SACCOS ilianziaga chini sana kwa marafiki tu kuanzisha umoja wao ila kwa sasa ipo level nyingine ikijumuisha matajiri wengi wa Arusha. Bado serikali inatakiwa itoe elimu kuhusu mambo ya fedha kwa wananchi. Itawasaidia kina Oscar Oscar na Deep Pond kutambua kuwa VICOBA havina jinsia. Umaskini hautaisha au kupungua kwa fikra kama hizi za Oscar Oscar na Deep Pond.
 
Back
Top Bottom