Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Sijawahi kufikiri kama ndugu Deep Pond nawe una fikra kama hizi. Village Community Bank (VICOBA) ina tatizo gani? Au ulimaanisha upatu? Vicoba viko karibu nchi zote za SADC & EAC na imeonyesha mafanikio makubwa. Tatizo kwa hapa nchini utakuta havijasajiliwa na havina utaratibu unaoeleweka. Arusha Club SACCOS ilianziaga chini sana kwa marafiki tu kuanzisha umoja wao ila kwa sasa ipo level nyingine ikijumuisha matajiri wengi wa Arusha. Bado serikali inatakiwa itoe elimu kuhusu mambo ya fedha kwa wananchi. Itawasaidia kina Oscar Oscar na Deep Pond kutambua kuwa VICOBA havina jinsia. Umaskini hautaisha au kupungua kwa fikra kama hizi za Oscar Oscar na Deep Pond
A
Faida ya vicoba anaiona mtu asiyejua kuhifadhi / kuwa na matumizi ya hovyo ya fedha, tofauti na hapa hakuna faida.
 
Shunie umetoa somo zuri, kama mtu hajaelewa ndio basi tena. 2017 hadi 2020 nilifaidi hiyo kitu kupitia wife, sikuwahi kwenda, sikujua hata nani ni nani huko, wife alikuwa na majina mawili, kukopa kwa riba nafuu kabisa, unakuwa mtu wa tight budget manake unajua kila mwezi/wiki lazima rejesho na hisa utoe.

Ila kikivunjwa, wife akikuletea maokoto ndio unaiona faida yake.
Na kwenye kuvunja hapo wanaume ndio huwa wanachanganyikiwa na kuomba wake zao wawachezee
 
Uko vizuri mkuu watu wana mitazamo hasi tu ya VIKOBA. Mimi na watumishi wenzangu tisa tulikaa tukawaza tukaona hatutoboi na mikopo ya benki, mtu unakopa 20mil unalipa 30mil. Tukaona hapana, tukajiunga tukaweka, tukasajili kikundi ustawi wa jamii na tukaweka lengo la kukusanya 12 mil Kwa mwaka wa kwanza. Hivi ninavyoongea mwaka wa tano tunaelekea 100 mil. Hakuna kwenda benki tena.
Safi sana mkuu, hii imekaa poa sana aisee.
 
Uko vizuri mkuu watu wana mitazamo hasi tu ya VIKOBA. Mimi na watumishi wenzangu tisa tulikaa tukawaza tukaona hatutoboi na mikopo ya benki, mtu unakopa 20mil unalipa 30mil. Tukaona hapana, tukajiunga tukaweka, tukasajili kikundi ustawi wa jamii na tukaweka lengo la kukusanya 12 mil Kwa mwaka wa kwanza. Hivi ninavyoongea mwaka wa tano tunaelekea 100 mil. Hakuna kwenda benki tena.
12M X 5 years = 60 M

ila ni kweli 60M ni kuelekea 100M
Hongereni sana ila pitieni katiba yenu vyema ya Ushirika wenu maana kadri fedha zinavyoongezeka Shetani wa Tamaa na migogoro anaanza vikao kazi

njia pekee ya kumdhibiti ni kuimarisha STK ( 'Sheria, taratibu na kanuni) za umoja wenu
 
Kwamba unakua mwanaume afu unaogopa kujitunzia pesa mpk zikakae vikoba[emoji28]
Kwahiyo uko bank ela zako unazitunza wewe mwenyewe?..Labda kama ulitaka kuzungumzia Upatu,ila vicoba ni bank ya vikundi kwa level ya kijiji.Na ina taratibu zake zauendeshaji,wewe sema kibongo bongo hatuzingatii sana hizo taratibu ndo maana unaona ni kitu cha hadhi ya chini au cha wanawake.Tunaona ni mambo ya wanawake kwasababu wanawake ni rahis kusocialize kwenye mijumuiko kuliko wanaume,ila haina shida yoyote mwanaume kua uko.
 
Back
Top Bottom