Mzigua90
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 38,342
- 88,625
Juzi kuna shosti yangu limemkuta jambo. NYUMBA aliyokua anakaa alishawahi kuishi mwanaume Fulani na familia yake. Sasa siku ya tukio wakati yuko ndani akasikia MTU anagonga geti lake kwa nguvu sana. Kwenda kufungua anakutana na mwanamke yuko na kitoto kichanga cha kama miezi minne.
Ile anafungua tu yule mwanamke akamwambia yani ilibaki dakika moja nikuachie huyu mtoto hapa nje ya geti niondoke zangu. Ikabidi shosti aulize kwani mbona sielewi. Akamwambia huelewi nini. Niitie mumeo Nina maongezi nae. Nae akazidi kushangaa maana ile NYUMBA anaishi mwenyewe na Mara chache hata mwanae anakuwepo. Mwanaume aliezaa nae hawana mahusiano ya kusema anaweza kuwa kama mume au boyfriend wake.
Sasa akawa anamtuliza anamwambia Dada utakuta umekosea NYUMBA. Anakazana kabisa ni hapa hapa kwa Jose. Wewe si ndo mke wa Jose? Sasa mumeo kanizalisha matumizi haleti nimeamua kuwaletea mtoto mumlee. Sasa like zogo likawavuta watu ndo kumtuliza yule Dada kuongea nae yule Dada ndo kugundua alipoenda sipo kwa muhusika.
Maana yake ni kwamba alishakua tayari kwenda kuvunja ndoa ya yule baba mtoto bila kujali mwenzie ana mke. Pata picha huyo baba alimficha mkewe kuhusu kuzaa nje halafu ghafla anakuja kutupiwa kichanga cha miezi mine akilee na mkewe.