Labda nikuulize mleta mada..
Baba yako unampenda? Je, haijawahi kupita siku, siku mbili, hata tatu au zaidi hujampigia simu? Je, uliposhindwa kumpigia simu, alikulalamikia kwamba humpendi? Je, kupiga/kutokupiga simu ndio kipimo cha mapenzi? Vipi kabla simu hazijaingia, watu walikua wanawasiliana kila siku? Je, walikua hawapendani? Hivi kiuhalisia kuna haja ya mtu kukupigia simu kila saa ndio eti ujue anakupenda??
Huu ulimbukeni wa kudhani kwamba mapenzi ni kupigiana simu ni utoto.. mimi naweza kukupigia simu na kutuma msg kila dakika na nikawa sikupe ndi vilevile. Wanaume wana mambo mengi ya kufanya kupambana na maisha, kutafuta pesa nk ili uishi maisha mazuri.. sio kukaa kupiga piga simu kila dakika..! Aftaroo ukipigiwa simu kila saa mnaanza kutuona kama mazuzu.