Hapo kila mtu atasema dada afuate ndoa kwa msukumo wa kwamba ndoa ni kitu adimu na akikosa hapo kwamba anaweza kusumbuka kupata tena mtu wa kumuoa.
Hili ni tatizo la jamii sasa. Vijana wengi wanakimbia ndoa hata kama wanaimudu sababu jamii imewashape watoto wa kike kuamini ndoa ni sehemu ya kupata kama vile mchezaji wa mpira anaposaini mkataba mnono wa pesa nene.
Sasa ukitazama vijana wengi hali ya uchumi kwao si nzuri miaka hii kumkuta kijana wa miaka 30 ana miliki tu subwoofer flash yenye miziki ya gosper na godoro tu anaishi chumba cha hana hata kiwanja anakula kwa mama ntilie imeshakuwa kawaida.
Mabinti hawawataki hawa vijana si kwasababu si waowaji bali ni ile hofu ya kutotaka kutafuta na mwanaume huwa wanasema wanaume watakuja kuwanyanyasa huko mbeleni na kuwanyang'anya kila kitu walichotafuta pamoja na kutafuta mwanamke mwingine na kuwatelekeza na watoto [emoji23][emoji23][emoji23] cha ajabu wao wanataka wakutane na mwanaume awe na kila kitu waende wakapate nae watoto kisha wamuombee afe warithi mali na kuzitawala kwa amani. [emoji23][emoji23][emoji23]
Huu ni ubinafsi ambao jamii ime instill ndani ya akili za watoto wa kike especially hawa wa kizazi cha miaka ya kuanzia 1980 kuja leo. Tazama sasa wanavyoteseka sasa na kuharibu zaidi ya vile walivyowazia kuwa wangeharibu. Wapo tayari kuolewa na mtu anaezaa zaa hovyo na mabinti na hawajibiki kujenga familia imara ili mradi wanaona wanavyotaka kwa huyu mwanaume, awe na gari, ameajiriwa serikalini, awe anatoa pesa ya shida ndogo ndogo, asaidie familia ya Mwanamke etc. Huu ndio upumbavu wanaoshawishiana kuukubali.
Hawa vijana wanaoishi wenyewe na hawajaoa wakishaanza kujitafutia na kutengeneza kipato, kuna umri wakifika ni ngumu sana kuja kuwashawishi kujenga tena familia maana pesa wamepata, wameshamiliki assets kama viwanja, nyumba, gari, na pesa benki, wewe mwanamke unakwenda kufanya nini sasa kwenye maisha ya huyu mtu na anajua umekuja kukwarua pesa zake utumie kutatua shida zako?
Sasa kama hamtaki kuolewa why mnahangaika kuzaa si mnataka kuishi kisela basi muendelee achaneni na kupata watoto na hamjui ndoa inafanyaje kazi. Kama hauna huruma wa kujali kumuinua, kumsapoti, kumfariji, kuhasisha, kusikiliza na kushirikiana na mwanaume kujenga maisha kuwa number one fan wake achana na kupata watoto wala kulilia kuolewa na ukijua hii kazi hauwezi maana ukiianza haina kupumzika.
Jambo jingine nawapa siri wadada. Kama unabisha fanyia utafiti. Hizi ni golden formulas za maisha ya mahusiano ukizishika utafanikiwa sana kimahusiano usipozishika siku ukisoma tena hii comment utajilaumu sana.
1. Katika vita ya mahusiano, mwanaume hupambana kwa msukumo wa asili yake, mwanamke hupambana kwa msukumo wa hisia zinamwambia nini kwa wakati huo. Hence In every game you play in relationships you are bound to fail. Be very careful and serious how u make decisions.
2. Ukiona kwenye uhusiano wewe ndie unatakiwa ufanye maamuzi au msukumo ndipo vitu vitokee jua haupo kwenye mahusiano upo na mtu ambaye anasubiria kuanza mahusiano na wewe sie muhusika. Kwasababu mahusiano mwanaume huwa ndie ana run vitu wewe mwanamke unareciprocate kwake efforts zake. Ukiona unajiona unapatia sana na wewe ndie director katika huo uhusiano then jua upo umeshafeli kabla ya kujua umefeli. Kama unabisha endelea utakuja elewa hizi kanuni siku ukishakichezea.
Unapona upo na mwanaume kila anachofanya kila kuinua au kukuletea maamkizi fulani then tayari upo katika mahusiano. Kama unabisha kumbuka kuna wanaume ulishakutana nao na ulifeel kitu ukiwa nao ila ukachagua kwa utashi wako binafsi kuwa una mambo muhimu ya kuyapa kipaumbele kwa muda huo sababu haukuwa umewaona muhimu hadi wakaamua kukuachia na maisha yako ila leo hii wameoa na wanafamilia ila wewe hadi leo bado unajitafuta uchawi kuwa ulilogwa na nani hadi sasa hauna familia na utulivu ni zero.
Ni kwasababu ulidharau hizi kanuni mbili hapo juu.
Sent using
Jamii Forums mobile app