Wanaume njooni hapa, Unapotafuta mke, Ni sahihi kumueleza binti unataka kumuoa unapomtongoza kwa Mara ya kwanza?

Wanaume njooni hapa, Unapotafuta mke, Ni sahihi kumueleza binti unataka kumuoa unapomtongoza kwa Mara ya kwanza?

Joao de Matos

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
334
Reaction score
268
Habari wanajamii forum.

Nimekuwa na maswali mengi kuhusu Unapotafuta mke. Na inapofika hatua ya kumpenda binti flani na kumueleza hisia zako za kutaka kuwa nae, hivi Ni sahihi kumueleza Moja kwa moja kuwa unataka kumuoa?

Maana kuna vitu najiuliza, kwamba wakati mwingine inaweza kuwa njia rahisi ya kupata mtu ambaye anania na ndoa kabisa.

Au wakati mwingine unaweza kupata mtu ambaye yeye kwanza anahitaji ndoa tuu na SI kukupenda wewe Kama wewe , yeye Ni hitaji lake Ni ndoa tuu. Na watu wa namna hi wanaweza kukuonyesha mapenzi fake ilimaradi umuoe tuu.

Na kuna kipindi ninaona si vyema kumueleza Moja kwa moja nia yako , Ni vyema ukaingia naye kwanza kwenye mahusiano ya urafiki kwanza.

Sasa ni sahihi kumueleza Moja kwa moja nia yako kumuoa au uingie tuu urafiki ya kawaida kwanza.

Nawasilisha: Uzi tayari
 
Habari wanajamii forum.
Nimekuwa na maswali mengi kuhusu Unapotafuta mke.
Na inapofika hatua ya kumpenda binti flani na kumueleza hisia zako za kutaka kuwa nae, hivi Ni sahihi kumueleza Moja kwa moja kuwa unataka kumuoa?
Chunguzaneni kwanza halafu ndio uangalie kama anafaa kuoa au laah, ndoa sio jambo la kukurupuka
 
ROBERT HERIEL once said,...
SITAKUOA KWA SABABU NINAKUPENDA, BALI KWA SABABU UNASTAHILI KUOLEWA NA MIMI.

Anaandika, Robert Heriel.

Naweza kukupenda lakini nisikuoe Kama haustahili. Ninauwezo wa kuutiisha moyo wangu ufanye kile akili yangu itakavyo. Kupenda ni tendo lisilo la hiyari, lakini kuendelea Kupenda ulichokipenda ni maamuzi ya mtu binafsi. Moyo unaweza kupenda lakini ukauzuia na ukatili. Ukiweza kuuamrisha moyo basi umeyaweza Mapenzi.

Naweza kumuoa Yule ambaye nilikuwa simpendi ikiwa anastahili kuolewa na Mimi. Ninaouwezo wa kuuamrisha moyo upende kile ulichokuwa haupendi na ukapenda.

Taikon na watu wa Aina yangu, tunaoa wanaostahili na hatuoi Kwa kufuata hisia na matamanio ya mioyo yetu.
VIGEZO kwetu ndio muhimu, anayestahili kuolewa nami nitamuoa. Siwezi kukuoa kisa umependelewa na moyo wangu wakati hauna vigezo. Hilo kamwe halitokaa litokee.

Binti Mzuri, anatabia njema, anamcha Mungu, ananipenda, anajitutumua na kuhakikisha ninakuwa Mume wake, anakuwa upande wangu na kunisapoti kila nikifanyacho, alafu ati nimuache binti huyo kisa moyo haumtaki, labda sio Mimi.

Alafu ati nihangaike na kabinti mshenzi ambako kapokapo,
Hakana tabia njema,
Hakanipendi ati mpaka nikafuate fuate na kujikomba komba Kama Paka,
Ati Mimi ndiye nijitutumue wakati kenyewe hakanihitaji, Dooh! Labda sio Mimi Taikon.

Vijana nisikieni Mimi Taikon, Ukitaka uyaweze mapenzi, basi mpe moyo wako mtu anayestahili kupewa na sio ufuate mihemko na hisia zako.

Mapenzi ni Kama mechi ya ushindani, wewe ndio Refa, kamwe usimpendelee mtu ambaye hastahili. Hata kama moyo wako ulikuwa upande Fulani. Mwenye vigezo vya kuwa Mke mpatie maisha yako.

Ukomavu ni pamoja na kujua namna ya kujidhibiti, kutenda haki, kuyapa maisha yako kile yanachostahili na sio kile utakacho.

Asiyekuhitaji usimhitaji. Hata kama moyo wako unakudanganya unamhitaji,
Asiyekupenda usimpende, hata kama moyo wako unakudanganya unampenda,
Moyo ni mdanganyifu, usikuingize mkenge.

Ukiweza kutumia kanuni hiyo itakusaidia baadaye,
Hakuna mwanamke atakayekupelekesha,
Hutokuwa mtumwa wa mtu,
Siku mwanamke akizingua unauwezo wa kumuacha kwani amepoteza vigezo na haukumpendelea, lakini kama ulimpendelea kwa kufuata moyo wako nakuhakikishia utakunya mavi.

Yaani uache mwanamke anayekupenda, na kujitoa kwako kisa moyo wako😀😀. Tumia Akili.
Ndio baadaye unakuja kulia Lia Kama Mpumbavu kazi kusumbua watu.

Nitakuoa Kwa sababu unastahili kuwa Mke wangu. Kisha nitauamrisha Moyo wangu Ukupende na utafanya hivyo.

Sipokei amri kutoka moyoni, Bali Mimi ndiye Natoa amri ya nini moyo upende.

Sipokei amri kutoka katika Nafsi yangu ya nini niamini Bali Mimi ndiye naiamrisha Nafsi yangu kile ninachotaka iamini.

Hivyo ndivyo namna ya kuishi maisha ya furaha na Amani.

VIGEZO na Masharti kuzingatiwa!
Ukishatimiza vigezo na masharti ndio Taikon atakupenda, na sio nikupende kisa nimekuona tuu umzuri, sijui unashepu, sijui unatembea kwa madoido. Never!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Yaaaani unamaanisha unaanza kumtongoza na neno natafuta mke wa kuoa? Kama jibu lako ni ndiyo usifanye hivyo. Kwa uelewa wangu mwanaume anayetongoza na kuanza na gia nataka kukuoa namtathimini kuwa labda ameona Mimi Nina njaa na ndoa Sana, hivyo anatumia njia hiyo ili anikule asepe. Utanioaje ndani ya week moja na Wala hatujuani? Kuweni kwenye mahusiano kwanza, ukimuona anafaa kuwa mke basi kaa naye chini umwambie mipango yako ya kuwa mke na mme.
 
Hapana.

Wanawake tunapenda sana ndoa. Na wengi wetu wapo desperate sana kuonekana wameolewa kwa sababu zao wenyewe.

Na ukizingatia ratio ya wanawake kwa wanaume inaongezeka itakuwa rahisi sana kwa bi dada kuficha kucha zake ili aonekane mwema na anaestahili kuwa mke.

Akishaingia ndani sasa. 🤭🤭
 
Back
Top Bottom