Wanaume njooni hapa, Unapotafuta mke, Ni sahihi kumueleza binti unataka kumuoa unapomtongoza kwa Mara ya kwanza?

Joao de Matos

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2022
Posts
334
Reaction score
268
Habari wanajamii forum.

Nimekuwa na maswali mengi kuhusu Unapotafuta mke. Na inapofika hatua ya kumpenda binti flani na kumueleza hisia zako za kutaka kuwa nae, hivi Ni sahihi kumueleza Moja kwa moja kuwa unataka kumuoa?

Maana kuna vitu najiuliza, kwamba wakati mwingine inaweza kuwa njia rahisi ya kupata mtu ambaye anania na ndoa kabisa.

Au wakati mwingine unaweza kupata mtu ambaye yeye kwanza anahitaji ndoa tuu na SI kukupenda wewe Kama wewe , yeye Ni hitaji lake Ni ndoa tuu. Na watu wa namna hi wanaweza kukuonyesha mapenzi fake ilimaradi umuoe tuu.

Na kuna kipindi ninaona si vyema kumueleza Moja kwa moja nia yako , Ni vyema ukaingia naye kwanza kwenye mahusiano ya urafiki kwanza.

Sasa ni sahihi kumueleza Moja kwa moja nia yako kumuoa au uingie tuu urafiki ya kawaida kwanza.

Nawasilisha: Uzi tayari
 
Habari wanajamii forum.
Nimekuwa na maswali mengi kuhusu Unapotafuta mke.
Na inapofika hatua ya kumpenda binti flani na kumueleza hisia zako za kutaka kuwa nae, hivi Ni sahihi kumueleza Moja kwa moja kuwa unataka kumuoa?
Chunguzaneni kwanza halafu ndio uangalie kama anafaa kuoa au laah, ndoa sio jambo la kukurupuka
 
ROBERT HERIEL once said,...
 
Yaaaani unamaanisha unaanza kumtongoza na neno natafuta mke wa kuoa? Kama jibu lako ni ndiyo usifanye hivyo. Kwa uelewa wangu mwanaume anayetongoza na kuanza na gia nataka kukuoa namtathimini kuwa labda ameona Mimi Nina njaa na ndoa Sana, hivyo anatumia njia hiyo ili anikule asepe. Utanioaje ndani ya week moja na Wala hatujuani? Kuweni kwenye mahusiano kwanza, ukimuona anafaa kuwa mke basi kaa naye chini umwambie mipango yako ya kuwa mke na mme.
 
Hapana.

Wanawake tunapenda sana ndoa. Na wengi wetu wapo desperate sana kuonekana wameolewa kwa sababu zao wenyewe.

Na ukizingatia ratio ya wanawake kwa wanaume inaongezeka itakuwa rahisi sana kwa bi dada kuficha kucha zake ili aonekane mwema na anaestahili kuwa mke.

Akishaingia ndani sasa. 🀭🀭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…