Wanaume oeni yatima, hamtojutia

Wanaume oeni yatima, hamtojutia

Hao nao wanapewa viburi na mashangazi na mamdogo zao labda kama unazungumzia yatima aliyeokotwa akiwa mdogo sana ndugu wengine hawajulikani,nayajua acha niishie hapa
 
Sio kila yatima anakua hivyo Mimi sitaki kusimulia, kwanza unazungumzia yatima yupi anaeishi na Mama yake au aliefiwa na wazazi wote Mama na Baba?

Maana yatima au binti anaeishi na Mama yake alafu Baba kafari au wanakwambia tu Baba hajulikani jaribu kufuatilia tabia za Mama usije ukaoa bomu la dakika,
Yatima maana yake ni mtoto aliyefiwa na wazazi wake wote wawili. Kama baba au mama yupo huyo siyo yatima. Na kama wazazi wako hai lakini hawamhudumii mtoto naye siyo yatima.
 
Ukienda kuoa angalia nani mwenye kauli kwenye familia kati ya Baba na Mama, ukiona Mama ndio mwenye kauli kijana jiandae kisaikolojia hapo jiandae kuburuzwa maana huyo binti kakopi familia yake inavyoendeshwa kimama Mama, ukikuta mwenye kauli ni Baba Oa fasta tena usiulize mahari mara 2 na usiweke hata deni maliza ingawa wanasema mahari haimalizwi

Haya mambo hayana formula rafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka mitatu iliyopita nilioa mwanamke kutoka familia ambayo alikuwa na wazazi wote, kwa kweli ndoa ilikuwa pasua kichwa , mwanamke akajaza vitimbi

Siku moja nikamwambia mjomba wangu kuhusu hali mbaya ya ndoa yangu, akanishauri achana na huyo mwanamke tafuta mwanamke ambaye ni yatima, ambaye maisha yake ya uyatima aliyaishi akiwa kati ya miaka 0 na 23, oa huyo utakuja kunishukuru sana

Ni kweli kabisa nimetoa shukrani kwa mjomba kwa ushauri aliyonipa ni miaka 2 imepita sasa na hajawahi kuleta mgogoro na mjomba alioa yatima anaishi kwa amani sana na mimi nakushauri tafuta yatima oa, ndoa yako itakuwa salama sana, na wanawake wa hivi wananidhamu, upendo, huruma, na wanyenyekevu ila ukimuudhi ni rahisi kububujikwa na machozi na nzuri zaidi mme wake ndiyo humfanya kama baba yake mzazi ambaye alimuacha akiwa mdogo
Hongera kuwa kama mimi japo mimi sijaoa yatima ila ninaishi maisha mazuri na yenye furaha tele na mke wangu
 
Ni kweli kabisa nimetoa shukrani kwa mjomba kwa ushauri aliyonipa ni miaka 2 imepita sasa na hajawahi kuleta mgogoro na mjomba alioa yatima anaishi kwa amani sana na mimi nakushauri tafuta yatima oa, ndoa yako itakuwa salama sana, na wanawake wa hivi wananidhamu,
Hongera ila nao huwa wanaruka ukuta nina ushahidi mwingi tu
 
Mungu ana nafasi maalum katika moyo Wake kwa yatima na wasio na baba (Kumbukumbu la Torati 24:20; Yeremia 49:11; Yakobo 1:27). Zaburi 27:10
Zaburi ya 68: 5 inasema, "Baba ya yatima, mtetezi wa wajane, ndiye Mungu katika makao yake matakatifu.
 
Siku mkiujua mzizi wa tatizo tutakuwa tumesolve 60% ya matatizo yote ya mahusiano.

Tabia ya ukubwani ni reflection ya tabia/mazingira mtu aliyokulia utotoni, kwa kuelewa au kutokuelewa ndiyo yanayomfanya mtu awe alivyo ukubwani. Na inaenda mbali zaidi, namna ambavyo mhusika ameelewa changamoto zake na kuamua kuzifanyia kazi.

Mwingine kwa kukosa familia utotoni anapokuwa mkubwa anathamini sana familia, ni kitu anachoweza kukifia, na familia bora inaanzia na ndoa bora. Kwa upande mwingine, mtu aliyekosa familia udogoni na pengine akalelewa kwa manyanyaso anaweza kuwa na roho ngumu/mbaya sana ukubwani, au akawa wa baridi (cold hearted) ambao ni watu hatari sana. The reason watu wanasumbuana sana katika mahusiano yoyote yale iwe ndoa, urafiki, ujirani, makazini etc ni sababu tunadeal na mashetani yaliyojivika ngozi za binadamu.

Kwahiyo mkuu circumstances yako haitoshi kudraw conclusion na kuitumia kutolea ushauri.
 
90% ya wanawake huwa viburi wanapokua na plan B kwenye maisha. Ndio maana wenye akili huoa wasio na elimu, kazi, pesa, wanaotokea maisha magumu nk ili waweze kuishi nao vyema. Kwahio leo tunaongeza na yatima kwenye list. Angalizo tusiwanyanyase ni dhmbi tuishi nao kwa amani maana wanawake wanye sifa hizo huwa wanyenyekevu sana
 
Miaka mitatu iliyopita nilioa mwanamke kutoka familia ambayo alikuwa na wazazi wote, kwa kweli ndoa ilikuwa pasua kichwa , mwanamke akajaza vitimbi

Siku moja nikamwambia mjomba wangu kuhusu hali mbaya ya ndoa yangu, akanishauri achana na huyo mwanamke tafuta mwanamke ambaye ni yatima, ambaye maisha yake ya uyatima aliyaishi akiwa kati ya miaka 0 na 23, oa huyo utakuja kunishukuru sana

Ni kweli kabisa nimetoa shukrani kwa mjomba kwa ushauri aliyonipa ni miaka 2 imepita sasa na hajawahi kuleta mgogoro na mjomba alioa yatima anaishi kwa amani sana na mimi nakushauri tafuta yatima oa, ndoa yako itakuwa salama sana, na wanawake wa hivi wananidhamu, upendo, huruma, na wanyenyekevu ila ukimuudhi ni rahisi kububujikwa na machozi na nzuri zaidi mme wake ndiyo humfanya kama baba yake mzazi ambaye alimuacha akiwa mdogo
We muombe Mungu azid kuwapa amani baraka na upendo chief ndoa haina formula. Mi naamin ukitaka mke bora muombe Mungu tu hakika atakupa hitaji la moyo wako. Kumbuka mali na urithi mtu ataupata kwa babae bali mke bora hutoka kwa Bwana. Hii kitu ni serious ishu aisee.
 
Back
Top Bottom