Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naboresha kidogo!! Yatima ni lazima awe ni mtoto mwenye umri chini ya 18yrs Amefiwa na mzazi mmoja au wote wawili. Akiwa 18yrs and above huyo sio yatima labda aitwe mkiwa.Yatima ni yule aliefiwa na mzazi awe mmoja au wote kwa pamoja, uliza swali lingine
There is point ktk hii mada na haya maelezo yako.Unaweza oa yatima aliyepitia maisha magumu akawa na roho mbaya na kisasi ndani ukimkosea kukuloga au kukuua kwa sumu jambo jepesi. Unaweza muoa hajawahi pendwa na hajui upendo ni nini, unaweza muoa kakukubali kisa ana shida.
Ila most of the time yatima ni wake wazuri na wafanyakazi wazuri. Bibi yangu mmoja ni mkorofi kama nini hakai na wafanyakazi dukani kwake ila ilitokea akampata mdada ni yatima alidumu nae sana. Na huyo yatima alipanga kwa mama mdogo nikaenda kuwatembelea nikamkuta. Kukekule alikuwa mtulivu kuliko wapangaji wote.
Nina classmate rafiki yangu sana wazazi wake walikufa kaolewa na mwanajeshi. Yule jamaa aliyemuoa kajenga haraka baada ya kuoa, mke wake anadai hana kwao wasipojenga hawajui kesho. Na shughuli za ujasiriamali nyingi. Wale wanajeshi wengine wanalewa tu, jamaa mwenyewe mkewe kamkuta na map.umbu na visabufa miaka kibao kazini hana kitu.
Mke yatima wa tangu utotoni hana wa kumpa jeuri kwao, hana upendo wa kifamilia zaidi ya mume na watoto wake, hana kimbilio akiharibu ndoa yake. Ni rahisi kupenda wakwe zake na huyu mara nyingi aliomba Mungu apate mume mwema maana ndio betting pekee aliyobakiza duniani.
Probably hana mpango wa kukuacha na ukitaka kumuacha ni bora ufe.
Uko sahihi kwa maana ya kitabuni. Ila kumbuka jamii tofauti tofauti huwa zina maana zake kulingana na jamii hizo. Kwa mfano ktk jamii zetu sisi mtu akifiwa na baba uyatima wake ni mkubwa kuliko kufiwa na mama. Mtu akifiwa na mazazi mmoja bado ni yatima hata akifikisha miaka 18. Tena hata ktk vikao vya familia utasikia hao watoto waacheni kabisaa ni yatima hao. Na hapo mmeenda na wake zetu. Kwanza mkikutana ktk vikao kuna ndugu wanalia kwa kukumbuka vifo vya dada zao au kaka zao ambao nyinyi ndo walikuwa wazazi wenu
[emoji16]Kosa hela alafu uje urudie kusoma ulicho andika hapa kwa sauti..
Mkuu,Siku mkiujua mzizi wa tatizo tutakuwa tumesolve 60% ya matatizo yote ya mahusiano.
Tabia ya ukubwani ni reflection ya tabia/mazingira mtu aliyokulia utotoni, kwa kuelewa au kutokuelewa ndiyo yanayomfanya mtu awe alivyo ukubwani. Na inaenda mbali zaidi, namna ambavyo mhusika ameelewa changamoto zake na kuamua kuzifanyia kazi.
Mwingine kwa kukosa familia utotoni anapokuwa mkubwa anathamini sana familia, ni kitu anachoweza kukifia, na familia bora inaanzia na ndoa bora. Kwa upande mwingine, mtu aliyekosa familia udogoni na pengine akalelewa kwa manyanyaso anaweza kuwa na roho ngumu/mbaya sana ukubwani, au akawa wa baridi (cold hearted) ambao ni watu hatari sana. The reason watu wanasumbuana sana katika mahusiano yoyote yale iwe ndoa, urafiki, ujirani, makazini etc ni sababu tunadeal na mashetani yaliyojivika ngozi za binadamu.
Kwahiyo mkuu circumstances yako haitoshi kudraw conclusion na kuitumia kutolea ushauri.
Sawa,, tunasubiri wiki ijayo mtuambie tena mnataka kuoa wa kina nani😑😑
Mtajua hamjui, kituo cha kwanza "Msimbazi Centre"Ko saiv mnatutaka mayatima😀😀😀
Mbombo ngafu
Professional teacher (japo sifundishi) , kazi yangu ya kwanza nimeanzia kwenye NGO ya maswala ya Elimu na kijamii.Mkuu,
Umesomea maswala ya kijamii?
ukioa yatima ujue wewe ndio baba yake na mama yake, ukifanya jambo akahisi unamwonea huwa wanakasirika kwa muda mrefu sana..... wanalia lia sana hawa!Miaka mitatu iliyopita nilioa mwanamke kutoka familia ambayo alikuwa na wazazi wote, kwa kweli ndoa ilikuwa pasua kichwa, mwanamke akajaza vitimbi
Siku moja nikamwambia mjomba wangu kuhusu hali mbaya ya ndoa yangu, akanishauri achana na huyo mwanamke tafuta mwanamke ambaye ni yatima, ambaye maisha yake ya uyatima aliyaishi akiwa kati ya miaka 0 na 23, oa huyo utakuja kunishukuru sana.
Ni kweli kabisa nimetoa shukrani kwa mjomba kwa ushauri aliyonipa ni miaka 2 imepita sasa na hajawahi kuleta mgogoro na mjomba alioa yatima anaishi kwa amani sana na mimi nakushauri tafuta yatima oa, ndoa yako itakuwa salama sana.
Na wanawake wa hivi wananidhamu, upendo, huruma, na wanyenyekevu ila ukimuudhi ni rahisi kububujikwa na machozi na nzuri zaidi mme wake ndiyo humfanya kama baba yake mzazi ambaye alimuacha akiwa mdogo.
Safi sana, unaitendea taaluma yako haki kabisa 👊Professional teacher (japo sifundishi) , kazi yangu ya kwanza nimeanzia kwenye NGO ya maswala ya Elimu na kijamii.
Huko ndiko nilipopata experience yangu ya masuala ya kijamii. 🤝
mwwnye mama siyo yatimaSio kila yatima anakua hivyo Mimi sitaki kusimulia, kwanza unazungumzia yatima yupi anaeishi na Mama yake au aliefiwa na wazazi wote Mama na Baba?
Maana yatima au binti anaeishi na Mama yake alafu Baba kafari au wanakwambia tu Baba hajulikani jaribu kufuatilia tabia za Mama usije ukaoa bomu la dakika,
Mayatima tunataka yatima wenzetuMtajua hamjui, kituo cha kwanza "Msimbazi Centre"