Wanaume tuelimishane ulinzi, ni silaha gani nje ya bunduki ni nzuri kuimiliki sehemu unayoishi?

Wanaume tuelimishane ulinzi, ni silaha gani nje ya bunduki ni nzuri kuimiliki sehemu unayoishi?

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Hasa kwa wale wanaoishi na mke ama / na watoto wadogo.

SILAHA ZANGU

1. FIRIMBI
firimbi zile za walinzi na sungusungu, zinasaidia kumpa wenge mvamiaji kudhani kwamba pana ulinzi shirikishi, filimbi hizi hazizidi elf 2 kwa machinga.

2. MANATI
Kwa mashambulizi ya mbali nina manati na golori za chuma, sio ya kuyachukulia poa hata kidogo, nikivuta hadi mwisho nikiachia, lazima ukae ama ubebwe.

3. RUNGU
nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.

Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
 
Mimi kwangu naona Upinde na kipodo cha mishale! Uzuri wa silaha hii siyo lazima upambane na adui uso kwa uso. Hata adui akiwa mbali unammaliza tu.

Ni tofauti na Kisu au Upanga ambavyo ni lazima upambane na adui uso kwa uso naye, sasa ukikuta adui ana nguvu kuliko wewe anaweza kukunyanganya silaha hiyo na kuitumia kukumaliza.
 
silaha gani nzuri kuimiliki chumbani kwajili ya ulinzi wako na familia kwa ujumla kama unayo ?

mfano umevamiwa na vibaka kama wawili hivi, inabidi ukae mkao wa ku attack maana ni aidha iwe wewe ama wao..
Mkuu.
Kwann usiwape mali waondoke badala ya kuanza vita!

Labda kama.unajua kilichowaleta ni kutoa uhai wako hapo itabidi upambane.
WEZI NA WAVAMIZI HAWANAGA CHAKUPOTEZA MKUU wameshauza nafsi zao zipo rehani hawana chakupoteza.

Silaha nzuri hapo ni muwe na panic room ambayo ina mlango mgumu
 
silaha gani nzuri kuimiliki chumbani kwajili ya ulinzi wako na familia kwa ujumla kama unayo ?

mfano umevamiwa na vibaka kama wawili hivi, inabidi ukae mkao wa ku attack maana ni aidha iwe wewe ama wao.

Binafsi nina manati na mawe ya mtoni kwajili ya mashambulizi ya mbali

Mashambulizi ya ana kwa ana nina rungu kama la komredi kipepe, nilitoka nalo kijijin, hili hata kwa paka hakuna mambo ya roho saba.
Hivi nauliza watanzania wenzangu kweli tutawahi kuendelea?

Usiku huu saa nne bado huko macho tu jamvin hujalala unaposti uzi na wengine kuchangia tutafika kweli?

Huu ni muda wa kulala bana siyo wa kuwa jamvin.

Kammoon kalaleni.

Sauh'waah?!
 
silaha gani nzuri kuimiliki chumbani kwajili ya ulinzi wako na familia kwa ujumla kama unayo ?

mfano umevamiwa na vibaka kama wawili hivi, inabidi ukae mkao wa ku attack maana ni aidha iwe wewe ama wao.

Binafsi nina manati na mawe ya mtoni kwajili ya mashambulizi ya mbali

Mashambulizi ya ana kwa ana nina rungu kama la komredi kipepe, nilitoka nalo kijijin, hili hata kwa paka hakuna mambo ya roho saba.
Well umeongelea manati ni sawa yanaweza kukusaidia kwa mbali,lakini chukua mfano wameishafanikiwa kuingiza sebuleni wewe uko chumbani, kwenye situation kama hiyo bastola ni muafaka haswa kama umejificha kwenye Kona fulani unawadondosha mmoja mmoja, lakini swali je ni Kila mmoja wetu ana sifa ya kumiliki bastola jibu ni hapana,

trick inayoweza kukusaidia ni kuwa na switch inayoweza kuzima umeme nyumba nzima, halafu unavaa miwani Yako ya night vision, huku umeshika chupa ya plastic ya nusu Lita, zile za maji ya kunywa, ikiwa imejaa maji yaliyochaganywa na pilipili ya unga Kali kabisa kifuniko kikiwa kimetobolewa tundu dogo unene wa njiti mbili za kiberiti, kwa sababu hawakuoni wewe unawaona unawaminyia maji ya pilipili kwenye macho, wakati wanafikicha macho unamaliza game na silaha za jadi halafu unawasachi mifukoni kama walitembea na hela'then unaripoti tukio kwa vyombo vya usalama.
 
Well umeongelea manati ni sawa yanaweza kukusaidia kwa mbali,lakini chukua mfano wameishafanikiwa kuingiza sebuleni wewe uko chumbani, kwenye situation kama hiyo bastola ni muafaka haswa kama umejificha kwenye Kona fulani unawadondosha mmoja mmoja...
Kwamba watavamia kiboya bila kuwa na tochi kweli!
 
Kwamba watavamia kiboya bila kuwa na tochi kweli !
Umenena hapo, maana sikuhizi hata simu za mifukoni zina tochi.

Ila kuna mdau kachangia kwamba silaha yake mojawapo ni tochi yenye mwanga mkali, nadhani kwa tuliowahi kusoma shule za boarding tunajua zilivyotumika, usiku taa zikizimwa mtu akipigwa mwanga mkali anakula mikanda bila kujua inatoka wapi
 
Back
Top Bottom