Wanaume tukatae kufa mapema kwa sababu ya wanawake

Kwenye misiba siku hizi wala hata kulia hawalii tena 👌👌
Sababu ya chuki.
 
Wakati mwanamke mwaminifu mbele za Mungu kabisa katika regular prayer items Mojawapo inapaswa kuwa ni ya kukataa Roho ya ujane.
Kujiombea na mumeo mfike wote uzee mwema mshibe siku za Neema kama Ayub kwa rehema za Mwenyezi Mungu.
Hata mume akienda kwa mchepuko unambea iwe salama siku zote asipate HIV,
Mungu mfungue akili yake iwapo mchepuke amemroga kumpumbaza n.k
 
Hata Mwanaume akianza kuumwa utakuta mke hamuuguzi vizuri mumewe,
Labda kama watoto ni wakubwa wamhurumie baba yao,
Au awepo ndugu waloshibana amiuguze lakini mke thubutuuu!
Wengine siku hizi ufanye kumtafuta mtu baki umlipe akusitiri.
Na kwa bahati mbaya wanaume huwa hawasemi wanapofanyiwa mabaya na wake zao
 
wanaume tunakufa haraka kwa sababu zifuatazo:-

1. Uzinzi(hatujali afya zetu) mwanaume kuwa na wanawake wengi ni ufahari, si unaona wanaojisifia kutembea na wake za watu, wanaume wanajisifia kufanya ngono kinyume na maumbile, hapa utakuwaje na maisha marefu? kaswende, kisonono, UTI na Fangasi vyote tunakumbana navyo utaponaje?

2. Ulevi wa kupindukia,wanaume tunaongeza kwa kutumia vilevi tena vikali, huko Rombo wanaume wanalalamikiwa kwa ulevi na kushindwa kuwatimizia wanawake haja zao kiasi kwamba wanawake wanakodi wanaume wa kenya, hapa mwanaume unaponaje na magonjwa ya mapafu?

3. Kuendesha vyombo vya moto pasipo uangalifu, ukifanya ulinganifu wanakufa kwa ajali kati ya mwanamke na mwanaume, wanaume ni wengi sana wanaokufa, wanakimbizana barabarani, hawajali yaani tuko careless tunajifanya kuonyesha, ujuzi kumbe ndio kufa kwetu.

4. Tunalogwa sana, kila eneo mwanaume ni target, ni kiumbe kinachowindwa sana.

Hata tukisema wanaume waache kuoa bado kufa kuko pale pale, kupanga ni kuchagua ufeje
 
Ndio mimi nasema mzazi wa mtoto wa kiume mwanao hata akiwa mkubwa usiache kuwa na mawasiliano nae ya karibu na awe huru kukweleza mambo ya ndani ili umtie
Moyo na umsaidie.
Wanaume wanabeba mambo mengi kifuani wanayofanyiwa na wake zao na Hawana jinsi ya ku-vent out.
Wanaume wengi wanaumwa presha na visikari sababu ya shida toka kwa wake zao.
 
Mimi sitakubali Mwanangu aje kuteswa na mkewe.
Na Mwenyezi Mungu anisaidie.
Kama vipi waachane kwa amani tu kuliko kutaka mtu akuulie mwanao weee !

Kama wapendana waishi kwa wema na upendo na kuchukuliana madhaifu ya kawaida .
Mkitofautiana zungumzeni malizeni tofauti zenu maisha yaendelee kwa Furaha na mke asiwe na tabia ya kukumbushia mambo yalopita kila mara.
Mwanamke unataka mume akugope?!
badala ya mume kukutawala wewe mke ndio unataka kuwa na sauti ?!
Hapana aisee!
 
Michepuko inakuja kutokana na stress tunazopata kutoka kwa wenza wetu. Ni jitihada za mwanaume kutafuta mahali ambapo atapata amani ya moyo. Sisemi kama ni sahihi au la maana yote yanaweza kukurudisha kule kule tu kwenye kiwanda cha stress.
mzuri pesa tu! kwanini usijinywee bia zako ukaenda kulala?!
 
Shogq yake uko kwenye vikoba/salon akimwambia muwekee simu ya Panya kama anakusumbua naweka. We uoni wamejaa wajane tu.
 
Asante sana, naomba kuishi na neno hilo, kujisamehe.
I think one of the best hraling process is to be able to laugh at yourself. Cheka sana, jiambie jinsi ulivyoingizwa mjini, ulivyodogoshwa na ukawa mdogo kama piriton. Yaani jinsi ulivyofanywa kama mtu alikuja mjini na gari ya maparachichi. Yaani ukishacheka hivyo endelea mbele! Na ufanye makosa mengine mapya usirudie ya zamani 😄
 
Asante sana mkuu, unaweza kuwa mleta habari njema kwangu

Sikuwahi kudhani kama kuna kujicheka!
Always najua kujilaumu, kujikosoa, kujilaani.
Kumbe ninanaweza kujicheka kwa some error issues nilizokutana nazo then nikapona!!
I will try my friend.
 
Asante sana mkuu, unaweza kuwa mleta habari njema kwangu

Sikuwahi kudhani kama kuna kujicheka!
Always najua kujilaumu, kujikosoa, kujilaani.
Kumbe ninanaweza kujicheka kwa some error issues nilizokutana nazo then nikapona!!
I will try my friend.
Karibu mkuu. Tena tafuta mtu wa karibu wa kujicheka nae. Yaani unampigia unamuambia sikujua mimi ni kenge namna hii! Yaani leo nimechemsha tope kabisa! Yaani wakati unamsimulia yeye anacheka na wewe unacheka! Usijipe nafasi ya kukasirika, ukutoka hapo mweupeee! Life is short jamani, make mistakes and learn from them; then find new mistakes to make 🤣🤣
 
Ukisha zaa nae watoto 2-3,Jitahidi kuwa mtu wa safari nyingi sana, maana yeye by nature huwa hakuhitaji sana, na hupenda vijana wadogo zaidi, safiri sana kumkwepa na uwe bize huko mbali, lakini udumia family kama kawaida. Utaepuka mengi.
Uzi ufungwe sasa, wewe unawajua vizuri sana wanawake "maana yeye by nature huwa hakuhitaji sana, na hupenda vijana wadogo zaidi"
 
Find new mistakes and learn
That's best quote kwa kweli.
Umahiri na umadhubiti unapatika kwa kujifunza kwingi.

Bado naendelea kushukuru , i wish ningekuwa na rafiki wa kuweza kuongea nae hivyo
Hata hivyo nimeichukua jinsi ilivyo , nitajiongelesha mwenyewe na kujicheka kwa vile nilivyo ingia king kizembe 😂
 
kataa ndoa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…