Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
Mwanaume aliyeoa ni sawa na Greda linalojenga barabara lakini Barabara ikikamilika linaletwa Gari kubwa la kubeba Greda lisipite ktk barabara kwa sababu ya kusema litaharibu barabara.
Mfano huo ni sawa na wanaume waliooa ambao hujinyima Nguo nzuri, Simu nzuri, Gari zuri, hujinyima Chakula cha mchana na kujituma kupambana kwenye utafutaji ili kutunza familia zao na kusomesha watoto wao.
Lakini watoto wakiwa wakubwa na wanapopata kazi, ktk hali ya kushangaza humjali zaidi mama yao na kumtelekeza Mzee aliyefanya kazi kubwa kwa kujituma kama punda akihangaika peke yake kijijini. Utakuta hakuna mtu anayejali kuona hali ya mzee huyu mstaafu au kujua kama amekula au anapata sitara ya baridi.
Ipo mifano iliyo ya kawaida siku hizi kuona watoto wakimchukua na kumpeleka mama mjini ili kufurahia faida za kuwalea.
Mwanaume, hebu liangalie hilo suala kwa jicho la pili na kuzingatia Malengo na Mpango wako wa maisha yako ya baadaye mapema kabla nguvu hazijapungua. Nakuhakikishia kama hujastuka mapema utakuja wakati huu wa bahati mbaya ambapo hakutakuwepo na mtu anayekujali hata watoto wako mwenyewe.
ANGALIZO: ujumbe huu hauna maana kwamba tusihudumie familia zetu ambalo ni jukumu lisilokwepeka, bali kutafuta balance usijiache nyuma kwa kutaraji kulipwa fadhira na watoto hapo baadaye. Wapo waliobahatika kutunzwa na watoto lakini bahati ya mwenzio.
Inaweza isiwe yako. Kumbuka mwanamke ana ushawishi mkubwa sana kwa wototo stuka chukua hatua mapema.