Wanaume tuna siri sana ila siri hii, hapana

Wanaume tuna siri sana ila siri hii, hapana

Mkanganyiko kukanganya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,204
Reaction score
5,053
Tukiendelea kungoja makarani wafike

Wakuu kuna suala nalitafakari nakosa jibu nisaidieni!

Iko hivi wengi wetu tunachangamoto za ndoa hasa kutokumwamini mwenza kwa matokeo ya mbeleni kwa ndoa kuvunjika kwa dalili unazoziona.

Wanaume nafikiri tunaweka usiri ambao mwishowe ni hasara za mali kupotea kwa kutojulikana na mwenza wa ndoa, watoto au mwanafamilia yeyote ikiwa msiri huyo akafariki ghafla na siri zake mbavuni.

Unakuta mtu ananunua kiwanja, nyumba, mradi n.k alafu anafanya kwa siri mara ghafla kafariki. Mwishoe mali hupotea kwa kutowafaidisha jamii ya marehemu kwa wao kutokuwa na ufahamu wowote.

Nafikiri hata kama ni kutomwamini mke/mme kwa sababu za usaliti, chuki, ubinafsi, tamaa au choyo basi mali hiyo mtonye kijana wako au ndugu unaemwamini ili ukifa isipotee kwa kuwa tupo ili tufe muda wowote kuanzia saa hii.

Mfano, kuna jamaa fundi magari aliachiwa noah kitambo kauza kifaa kimoja to kingine mpk likaisha (wanadai muhusika alifariki na fundi kwa tamaa au kutojua sijui)

Nilitaka kusema kwamba kuna kiwanja jirani yangu hapa kina zaidi ya miaka mingi kilijengwa msingi tu kimetelekezwa miaka sasa ni pori na kipo kona nzuri mnoo na hakunaga mtu anakuja hata kulima au kusalimia majirani.

Nasubiria sensa wapite kunihesabu then najitoa ufahamu napandisha jengo mimi naona nimeokota kiwanja

Memba kuna mtu alishawahi okota kiwanja?? Vp je nikiendeleza jengo kitanuka nini

NB: picha siweki usijesema ni chako.
Asante
 
Tukiendelea kungoja makarani wafike
Wakuu kuna swala nalitafakari nakosa jibu nisaidieni!!

Iko hivi wengi wetu tunachangamoto za ndoa hasa pia swala kutokumwamini mwenza kwa matokeo ya mbeleni kwa ndoa kuvunjika kwa dalili unazoziona.

Wanaume nafikiri tunaweka usiri ambao mwishowe ni hasara za mali kupotea kwa kutojulikana na mwenza wa ndoa, watoto au mwanafamilia yeyote ikiwa msiri huyo akafariki gafla na siri zake mbavuni.

Unakuta mtu ananunua kiwanja, nyumba, mradi n.k alafu anafanya kwa siri mara gafla kafariki. Mwishoe mali hupotea kwa kutowafaidisha jamii ya marehemu kwa wao kutokuwa na ufahamu wowote.

Nafikiri hata kama ni kutomwamini mke/mme kwa sababu za usaliti,chuki,ubinafsi,tamaa au choyo basi mali hiyo mtonye kijana wako au ndugu unaemwamini ili ukifa isipotee kwa kuwa tupo ili tufe muda wowote kuanzia saa hii.
Mfano, kuna jamaa fundi magari aliachiwa noah kitambo kauza kifaa kimoja to kingine mpk likaisha(wanadai muhusika alifariki na fundi kwa tamaa au kutojua sijui)

Nilitaka kusema kwamba kuna kiwanja jirani yangu hapa kina zaidi ya miaka mingi kilijengwa msingi tu kimetelekezwa miaka sasa ni pori na kipo kona nzuri mnoo na hakunaga mtu anakuja hata kulima au kusalimia majirani.

Nasubiria sensa wapite kunihesabu then najitoa ufahamu napandisha jengo mimi naona nimeokota kiwanja
Memba kuna mtu alishawahi okota kiwanja?? Vp je nikiendeleza jengo kitanuka nini
NB: picha siweki usijesema ni chako.
Asante
Nyumba na kiwanja haviokotwi ,akili mtu wangu [emoji848]
 
Unakuta mtu ananunua kiwanja, nyumba, mradi n.k alafu anafanya kwa siri mara gafla kafariki. Mwishoe mali hupotea kwa kutowafaidisha jamii ya marehemu kwa wao kutokuwa na ufahamu wowote.

Nafikiri hata kama ni kutomwamini mke/mme kwa sababu za usaliti,chuki,ubinafsi,tamaa au choyo basi mali hiyo mtonye kijana wako au ndugu unaemwamini ili ukifa isipotee kwa kuwa tupo ili tufe muda wowote kuanzia saa hii.
Kuna wanawake wana siri bora wanaume, kuna akina mama wanajenga nyumba na wengine wanajengewa na wanaume wa pembeni kwa kisingizio cha wadogo zao
 
Mnhh!! Kwahiyo unafikiri hicho kiwanja mwenye Mali kafa na alifanya siri. !? Hakuna serikali ya mtaa au ya kijiji hapo!??Balozi au kitongoji!??
 
Umenikumbusha ule Uzi jamaa amepewa kazi ya kulinda nyumba ya mnene mmoja pande za ununio lkn imepita miaka zaidi ya 5 jamaa hajarudi,hajapiga simu wala kutuma meseji,pia wala hakuna ndugu yoyoyte aliyepiga simu wala kuja kwenye ule mjengo..kuna uwezekano akawa amefariki Yule jamaa Mwenye nyumba

Jamaa kwenye Uzi alipewa ushauri aweke wapangaji kwenye like ghorofa,endapo mwenyewe atatokea mwaka wowote atamwambia alikuwa anautafuta hela ya Kula..wengine walishauri upuuzi

Kuna Siri zingine hazifai kuwa Siri Kwa watu wote maana siku tukifa tulivyovitafuta vinatoweka bila taarifa
 
Kila mwanaume atafute Hela zake period!

Mtu akitafuta Hela zake akajenga nyumba asiwashirikishe ndugu akafa ikapotea ni shida yenu? Mlikuwa mnaijua kwani hadi muumie. Yeye mwenyewe aliwaona hamfai akatafuta mtu wa mbali basi pigeni kimya tu. Bro tafuta Hela zako acha kuumia Kwa Mali za watu hata kama ni ndugu zako
 
Kiwanja kitakaa hata miaka 20 siku unapandisha jengo ndio mwenyewe anatokea 😂🤣

Kiukweli si vema kuficha vitu, ukiona inafikia hatua unafanya jambo la maendeleo unamficha mkeo, basi kubali ulikosea kuoa toka awali.
 
Kila mwanaume atafute Hela zake period!

Mtu akitafuta Hela zake akajenga nyumba asiwashirikishe ndugu akafa ikapotea ni shida yenu? Mlikuwa mnaijua kwani hadi muumie. Yeye mwenyewe aliwaona hamfai akatafuta mtu wa mbali basi pigeni kimya tu. Bro tafuta Hela zako acha kuumia Kwa Mali za watu hata kama ni ndugu zako
Hii ni fact 100% watu tusiumie kwa mali zisizokuwa zetu

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza juwa kuwa sio mwanaume pekee ndio anafanya hizo siri,hata wanawake pia wanafanya,ila vyovyote iwavyo ukishona hiyo hali kwenye mahusiano juwa kuwa tayari hali ya mahusiano sio nzuri,mkiwa vizuri kwenye ndoa na hakuna misuguano yoyote huwezi kukuta hilo jambo...
 
Viwanja vya namna hyo ambavyo vipo tu havijaendelezwa vipo vingi sana ila ukitaka kuanza kujenga tu mwenyewe anakuja.
 
Back
Top Bottom