ahahhaha aisee!! Mkuu
Duke Tachez umeongelea mada moja yenye kuhitaji mjadala wa kina sana, na ndio maana ndoa nyingi hazidumu kwa sababu huwa tunauziwa mbuzi kwenye gunia, mtoto mnaonana kazini tu anakuja anawaka kama jua la jangwani unashusha nondo kali kama za Controller Audit General (CAG) unakubaliwa kidogo harusi..... hapo unakuja kugundua the true color ya mama kijacho, aiseeee!!! aisee!! mfanyakazi mwenzangu alioa harusi ikafana sana kula kunywa hadi kusaza wazee wanateremsha maji ya mende wanamsifia bi harusi kwamba jamaa kajua kuchagua mwanzo mwisho, fungate limeisha siku ya kwanza jamaa anakuja na mamsapu wake job kumuonyesha kibaruani kwake, walivyoondoka huku nyuma ukazuka mjadala mkubwa sana ndie yeye ama sie? aiseee kaka
Duke Tachez.....