Wanaume tunaokwenda kujitambulisha ukweni hivi karibuni njooni tupeane mbinu za kurahisisha jambo

Wanaume tunaokwenda kujitambulisha ukweni hivi karibuni njooni tupeane mbinu za kurahisisha jambo

Nacheka ninaposoma huu Uzi...

Naona utoto mwingi...

NB: Ndoa ni zaidi ya kuchomeka na kuchomoa...
 
Binafsi mwezi ujao naelekea Tanga maeneo ya Muheza kujitambulisha. Nimejipanga kwa haya yafuatayo.
1. Sitolala ukweni.
2. Ikitokea kula ukweni ntakula mlo mmoja tu.
3. Ntavaa simple sana( shati yangu ya mikono mirefu, suruali na balaghashehe kichwani) na kiatu changu cheusi
4. Nitaongea kwa vituo vingi sana.
5. Ntaomba nafasi ya kukaa ni binti yao kwa dakika 15 , nimsikilize utayari wake na jambo la ndoa, na kumsoma mawazo na akili yake kwa ujumla.
6. Katika maongezi yetu( mimi na binti yao) nimepanga niwe msikilizaji muda mwingi(ntaongea kidogo ).
7. Kwenye Barua ya posa sitoweka zaidi ya elfu 30.
8. Mahari sitolipa zaidi ya laki 5 ( Na hapo ntalipa kidogo kidogo) nyingine tutamalizia kwenye ndoa mbele ya safari.
9. Mama mkwe akiwa muongeaji sanaa kuliko baba mkwe basi huenda nikaghairisha kumuoa binti yao (elewa neno huenda).
.
.
.

Endelezeni madini mengine mkuu.
Tupeane tips hizo tusinyimane.
Hapo namba 2,kwani ulitaka ule milo mingapi mkuu?
 
Nacheka ninaposoma huu Uzi...

Naona utoto mwingi...

NB: Ndoa ni zaidi ya kuchomeka na kuchomoa...
Akamkaze mtoto wa watu kwa laki 5 miaka yote Afu alipe kidogo kidogo.

Anapanga kulala ukweni.
Barua anapeleka mwenyewe.

Hataki mama mkwe aongee
Au kachaguliwa mchumba huyu.
 
Akamkaze mtoto wa watu kwa laki 5 miaka yote Afu alipe kidogo kidogo.

Anapanga kulala ukweni.
Barua anapeleka mwenyewe.

Hataki mama mkwe aongee
Au kachaguliwa mchumba huyu.
Huyu jamaa anafurahisha genge, hamna muoaji hapo...
 
Huyo mke umechaguliwa au imekuwaje?
Nilitegemea uwe umemfaham vizuri kabla ya kuwa na maamuzi kwenda kwao kutoa barua.

Barua hupeleki wewe anapeleka mshenga ndugu,wew ukakaa kusubiri majibu yao baada ya kuzungumza na bint yao ambae ameridhia wewe upeleke posa kwao.
Mwenyewe nimeshangaa, et anaenda kumsikiliza utayari wake kuhusu ndoa, 😂 ina mana hajawasiliana nae kama yupo tayari ?
 
Mkuu hongera Kwa kupata mbususu ya kitanga,ila Kwa mwandiko huu naona kabisa unaenda kuharibu hiyo ndoa
 
Namba 5 kwann mpk ufike ukweni ulitakiwa kuwa ushafanya
 
unajipanga nini wewe nenda katika hali ya kawaida

wasikilize msipoelewana basi kila mtu akubali kutokubaliana na mwenzake basi
 
Back
Top Bottom