Sisi wanaume ambao hatuchagui mpaka povu la sabuni ya unga tunaogea mnatuweka kundi gani, kuna kuna kina sisi tunaooga chukuchuku kama hakuna sabuni, ama tunaita kujimwagia maji.
Ila kiukweli kabisa, mambo ya kupaka lotion ama mafuta kumenikalia kushoto mnooo, siwezi kabisa, na sijawahi kutoa hela yangu nikanunua lotion,
Mke wangu alijaribu jaribu mwanzoni, akaona huu mti mkavu kwenye suala la kupaka mafuta ama lotion nimemshindwa.
Labada niende mkoa wenye baridi sana, na huko sipaki mafuta mwilini, ni mdomo tu sababu huwa unachanika chanika.