Wanaume tunaopenda kuwa smart tusikose package hii

Wanaume tunaopenda kuwa smart tusikose package hii

Mtu anayefanya kazi za mikono, inachafuka. Au mwalimu na Chaki. Anafanyaje kuweka mikono yake smart?
Hawawezi kukuelewa, unakuta mtu amevaa vizuri ila vidole vya mikono vinatoa harufu ajabu. Mtu anayejitambua hawezi kukubali mikono iwe na hali hiyo.

NB: Hayo uliyoyaita mafuta huwa yanatumika sehemu gani ya mwili?.
 
Kwa wale wanaume tunaopenda kuwa smart, nashauri tutumie hizi package zitakuweka smart sana bila kujali unafanya kazi gani na eneo gani.

Dove Gel Body Wash
View attachment 3207110
Hakikisha ni Secret, ujue pia kutofautisha fake na OG. Chupa ndogo inauzwa Sh.12,000 mpaka 15,000. Kubwa inauzwa Sh.20,000.

Jergens Utra Healing.
Haya mafuta ndio ninatumia mimi, nimeona matokeo mazuri sana. Usichukue Jergens yeyote tu bali chuku Utra Healing yenye Vitamin C, E na B5.
Bei yake sio kivile ni Sh.45,000 mpaka Sh.50,000

View attachment 3207079

Nivea Men Breathable
Haya mafuta ni ya ukweli sana wakuu, jaribu kuyatumia utayakubali
View attachment 3207094

Kwa body lotion napendekeza hayo mafuta

Dove Hand Cream
View attachment 3207100
Pamoja na kutumia body oil bado hutakiwi kukosa Hand Lotion kwa ajili ya kuiweka mikono yako vizuri. Hasa kwa wale wa maofisini usikose hii kitu kwenye kibeg au kwenye gari. Labda umefanya kazi ngumu ya kutumia mikono,au vyovyote vile umeona mikono yako haiko sawa, tumia hiyo hand lotion.
Kwa mimi napendekeza Dove hand cream. Inauzwa Sh.10,000 mpaka Sh.12,000
Mwasibu CPA uchwara SUNZU BOBAN OKW umehamia huku tena?
 
Sisi wanaume ambao hatuchagui mpaka povu la sabuni ya unga tunaogea mnatuweka kundi gani, kuna kuna kina sisi tunaooga chukuchuku kama hakuna sabuni, ama tunaita kujimwagia maji.

Ila kiukweli kabisa, mambo ya kupaka lotion ama mafuta kumenikalia kushoto mnooo, siwezi kabisa, na sijawahi kutoa hela yangu nikanunua lotion,
Mke wangu alijaribu jaribu mwanzoni, akaona huu mti mkavu kwenye suala la kupaka mafuta ama lotion nimemshindwa.
Mie ni body spray tu baasi.

Labada niende mkoa wenye baridi sana, na huko sipaki mafuta mwilini, ni mdomo tu sababu huwa unachanika chanika.
 
Nikioga nikapaka duodorant yangu kwapani, futa la nazi juu ya ngozi, saa mkononi, nguo zimepigwa pasi, mkanda kiunoni, kiatu mguuni, nmechana kipilipili changu kichwani na uchebe plus kaunyunyu kidogo cha savage nimemaliza.

Hizo dove nikinunua zitaexpire nitasahau kutumia.
Kuna sabuni zinaitwa MEGA zina maandishi ya kiarabu, ni buku tu hazina harufu kali binafsi tangu nizijue nazipendelea sana.
Hivi kwa joto hili watu mnapaka lotion kweli
 
Mikono inaoshwa mara kwa mara ndio maana ina moisturizer yake ambayo ndio hiyo hand cream...
Zipo hand cream kwa ajili ya wanaume, kwa ajili ya ngozi ngumu za kiume...

Hakuna uwiano unapotumia moisturizer usoni halafu mikono imekakamaa kama ngozi ya kenge...

Kama una moist mwili mzima basi fanya mwili mzima tu..
Yani kabisa Mkuu unatumia muda wako kunifafanulia kuhusu vipodozi mimi? Umenichekesha sana, mie ni jabali hakuna utakachoniambia kwenye hii sekta.

Huyo niliyemuita anatumia products nyingine bora zaidi ya hata hiyo Dove, na tulishazungumza kwa alipo na nikamwambia vya kutumia.

Good day.
 
Kwa wale wanaume tunaopenda kuwa smart, nashauri tutumie hizi package zitakuweka smart sana bila kujali unafanya kazi gani na eneo gani.

Dove Gel Body Wash
View attachment 3207110
Hakikisha ni Secret, ujue pia kutofautisha fake na OG. Chupa ndogo inauzwa Sh.12,000 mpaka 15,000. Kubwa inauzwa Sh.20,000.

Jergens Utra Healing.
Haya mafuta ndio ninatumia mimi, nimeona matokeo mazuri sana. Usichukue Jergens yeyote tu bali chuku Utra Healing yenye Vitamin C, E na B5.
Bei yake sio kivile ni Sh.45,000 mpaka Sh.50,000

View attachment 3207079

Nivea Men Breathable
Haya mafuta ni ya ukweli sana wakuu, jaribu kuyatumia utayakubali
View attachment 3207094

Kwa body lotion napendekeza hayo mafuta

Dove Hand Cream
View attachment 3207100
Pamoja na kutumia body oil bado hutakiwi kukosa Hand Lotion kwa ajili ya kuiweka mikono yako vizuri. Hasa kwa wale wa maofisini usikose hii kitu kwenye kibeg au kwenye gari. Labda umefanya kazi ngumu ya kutumia mikono,au vyovyote vile umeona mikono yako haiko sawa, tumia hiyo hand lotion.
Kwa mimi napendekeza Dove hand cream. Inauzwa Sh.10,000 mpaka Sh.12,000
Nipe packages ya pamba.

Sabuni natumia ya Unga/Kipande ya kufulia.
 
Bora useme wewe! Mimi wameniita mshamba
Mwanaume na hand cream loooh🙌
Hand cream ni hapana na nimemwambia mtu hapa loud & clear, huo mstari asiuvuke.

Kuna products naweza kumuelewa, face wash, showe gel, moisturizer za kiume zipo kibao, deodorant & perfumes zote awezavyo.

Ila serum, toner, hand cream, sunscreen, lip balm, face mask zimpite mbali.
 
Hadi sunscreen mbona unamuonea😂
Mimi sijawahi kununua sunscreen hua nategea ya babe wangu.
 
Back
Top Bottom