Mkuu unakuta mwanaume kaoa binti mbichi kabisa,hana mambo mengi kabisaa!ila akishaanza kumzalisha tu ataanza kumuona hana jipya tena,hamjali wala kumtunza na hapo anataka huyo mwanamke asifanye kazi ya kujiingizia kipato hata cha kujitunza kidogo eti kisa atakuwa jeuri.Mwanamke ule uzuri wa muonekano wote unaondoka kwa manyanyaso ya kihisia,Mwanaume anafanya chochote kibaya anacho jisikia akijua bibie hana pakwenda na vile wanawake wengi huwa wanavumilia kwaajili ya watoto basi anaishia kugumia tu ili mradi siku ziende.Ubaya wanaume wengi wakimpata mwanamke mtulivu na anayewapenda kwa dhati huwa wanamuona km mjinga.
Nimeshudia hata kwa ndugu zangu wa kiume,ni wachache sana wanajua kuthamini walichonacho.Yan mwanaume anaenda kumpendezesha kahaba na kumuacha mkewe aliyemkuta mbichi kabisa achakae kwa mawazo na majuto.
Kwa mimi huwa inaniumiza sana hata kama hayajanikuta ila hii hali inakatisha tamaa.Huwa nanaki najiuliza..."Sasa neema ya kuolewa kwa huyu dada maskini ni ipi?"