ShyaRuwa
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,895
- 13,643
Kila mtu ana interests zake kwenye haya maisha.Mkuu CHARMILTON naona kuna kitu huenda unakimiss hapa,
au labda uko kwenye umri ambao huishi uhalisia wa Maisha,unaishi kulingana na namna wewe unavyoyaimagine Maisha,
kuna utofauti mkuwa sana kati ya Maisha tunayojiaminisha tunaishi na uhalisia wa Maisha hali hapa ulimwenguni,
mkuu unapaswa kujua kwenye ukuzi wa mtu kuna stage nyingi sana anapitia,na ni stage hizo hizo zinazomfanya mtu eiza aje ajutie hapo baadae au ashukuru kwa stage aliyopitia na maamuzi aliyoyafanya akiwa stage hiyo,
kuna stage ambayo vijana tulio wengi huwa tunaishi Maisha ya kufikrika,yaani tuko kwa ajili ya kusatisfy our own desire na tunaishi kwenye ulimwengu ambao tumeuumba sisi vichwani mwetu,stage hii ikitumika vibaya au kwa muda mrefu sana huweza kutokeza majuto makubwa sana huko mbeleni tuendako,ila tukistuka kwenye stage hii mapema na kurekebisha mambo na kuanza kuishi kwenye ulimwengu halisi na sio ule wa kufikrika tunaweza kusave majuto mengi sana baadae huko tuendako, (laiti vijana wote tungekuwa tunastuka mapema sana kwenye hii stage na kurekebisha mambo,dunia ingekuwa mahalia salama sana pa kuishi,too bad tulio wengi hii stage huwa inatuvuruga sana,kuja kustuka its too late hata marekebisoa hayawezekani kabisa,kama yanawezekana ni kidogo sana and its a waste)
Lakini pia ndoa ni Zaidi ya yale uliyoyasema huko juu mkuu,asikwambie mtu mkuu ulimwenguni hapa hakuna kinachoweza kulinganishwa na familia nzuri yenye furaha,narudia tena hakuna,wale walio na ndoa zao na familia zao mubashara wanaweza kuwa mashahidi wa hili
aina ya Maisha uliyochagua kuishi kwa kujiaminisha kwamba inakupa uhuru na ndio unaoutaka haiwezi kukupa hiyo satisfication ambayo wenye ndoa au familia nzuri wanayo
Hope some days utaiona ndoa katika angle tofauti kabisa na angel unayoiona kwa sasa Mkuu, All the best.
Unachokiona wewe kuwa cha muhimu hakiwezi kuwa vilevile kwa mwingine.
Mimi kudili na mambo niliyoyachagua haimaniishi kwamba hayana faida.
Hivi kwanini umeelezea ndoa kwa upande mmoja tu? Binafsi natambua umuhimu wa ndoa ni kwa faida ya malezi ya watoto basi! Hayo mengine ni maigizo.....ukianza kuorodhesha changamoto za ndoa utamaliza leo?