Nawaheshimu sana single mother honestly . Kulea mtoto peke yako si kazi rahisi. Malezi ni zaidi ya kuwa na hela aisee. Mtoto kazidiwa usiku unakimbizana naye peke yako, how you wish angekuwepo baba yake akaku-hug tu na kukwambia tu "our kid is going to be ok". Let alone mtoto anavyoanza kukuuliza, mama mbona mimi baba yangu simjui au hatukai naye kama wenzangu". Bado socila rejection hapo. And honestly kuna part ya malezi ambayo baba anaiwezea zaidi kuliko mimi. Wawili sio sawa na mmoja. But all is well, yakitokea unajipanga tu unakuwa both mama na baba
Kuna single mothers ambao waliamua kuacha ndoa zao, wakajibebea watoto wao na kuwalea vyema. Hongereni strong women, sio wanawake wote wana guts za kutoka kwenye toxic relationships, wengine wanabaki tu kisa akiachika eti hakuna mwanaume atayemkubali na wanae,... woman, know your worth. Tutawaita majina yote, but nyie ndo mnajua vyema nini kiliwatoa, na mnajua ni kipi mnachokitaka kwa ajili ya maisha yenu. But mabinti pia, jamani huyo ni boyfriend wako sio mumeo, ooh sijui nampenda sana namzalia, zaa tu mama ila usije kulia jamani. Mtu una boyfriend anawachanganya wanawake watatu, ila unahisi ukijibebesha mimba ndo atastick na wewe pyeee. Na mwingine anakwambia kabisa hana future na wewe, ila bado tu unajiachia naye kama mumeo mmh. Ataenda kuoa mwenzako pamoja na kuwa single faza na wanawake watamgombania tu, subiria wewe sasa .
Tabia ya kupasha viporo, wanayo tu watu wengi, ila single mum akipasha kiporo au akichepuka, hatutomjudge kuwa ni Tabia tu ya wanawake wasio waaaminifu, ila tutajudge tu kuwa single mazas ndivyo walivyo. Wote tunakosea, ila ukishakosea jifunze kosa lako, usirudi tena ulipotoka na usiruhusu past yako iwe inakumbushiwa kila mara. S/O kwa single mazas wote mnaojitambua na msiokubali past zenu zisiwakatishe tamaa. You are already good enough, Mtu/jamii isiwafanye mkajiona hamna thamani. Mkijithamini na kujiheshimu nyinyi wenyewe kwanza, then kila mtu atawathamini, na hata tusipowathamini inahuuu kwani. Makosa yalishatokea, hayawezi kufutika but mna uwezo wa kutengeneza present na future yenu vizuri sana