Wanaume wa JF, single mothers waliwafanyia nini?

Wanaume wa JF, single mothers waliwafanyia nini?

Kuna single mom wengine walitegeshea mimba makusudi kabisa n wakapigwa chin afu wanataka tuoe ili tuanze ndoa na majukumu ambayo c ya kwetu.
 
Hellow JF,

Naomba kuwauliza wanaume mliopo humu JF, hivi single mothers waliwafanyia nini mlio wengi, mbona mnawaandama sana kila kukicha?

Naombeni mnijibu sababu thread zenu zinaumiza sana pia zinachosha as long as sio wote walipenda kuwa single mothers wengine iliwabidi tu, au mlitaka wafanye abortion kuepuka kuwa single mothers?

Single mothers =Single fathers.
 
Hellow JF,

Kuna baadhi ya wanaume humu wanapenda sana kuwadis single mother. Jamani usimhukumu mtu eti kwa vile tu ana mtoto na hajaolewa sawa japo yatakiwa mtoto azaliwe katika ndoa but inapotokea kazaliwa pasipo ndoa haitakiwi kumlaumu mtu wala kumuongelea vibaya kwa kitu kama hicho.

Everything happens for a reason na ni bora anayezaa hata kama hayupo ndani ya ndoa kuliko anayefanya abortion kisa tu kapata mimba then bado hajaolewa au mwanaume kamkimbia.

Kuna watu wanaongea maneno makali sana kuhusu single mother, kweli hakuna anaependa kuwa single mother but Mungu akikubariki mtoto ni kushukuru sana sababu mtoto ni baraka kubwa sana haijalishi umempata katika mazingira gani. Kuna watu wapo kwenye ndoa but hawana furaha kwa kukosa watoto.

Pia hata ukizaa kama kuolewa kupo utaolewa tu, mtoto sio kikwazo. Wangapi wamezaa na wameolewa tena na vijana ambao hawana hata mtoto? Mtu akikupenda hatajali kusema una mtoto. Upendo wa kweli hauchagui.

Msiwaongelee vibaya single mothers, Mungu anawaona
[HASHTAG]#kigodoro[/HASHTAG].
 
Hao hawaongelewi vibaya isipokuwa watu wanataadharishwa kuwa ukiamua kuoa single mother basi jiandae na changamoto zake nyingi.
 
Ila haya maneno makali yanakuja baada ya hao single mothers kuja na very defensive argument zenye maneno makali. Wakati mwingine thread zina lengo la kuwaweka sawa mabinti wasije wakajikuta kwenye hali ambayo hawakutegemea.
 
Nakubaliana na wewe,, 100% kuna watu hawafikirii mbali badala yake mnawadis hawa dada's hawana makosa maana tunawadanganya sisi,, bora kuza na kulea katika mazingira magumu kuliko kutupa mtoto au kuchoropoa mimba!!! Tuwaache ama tuwape surpot Dada zetu. Obama ni zao LA single mother!
 
tunawongea hivo ili kuwataadharisha mabinti mabinti kuwa ukiwa single mother ushaloose battle tayari hivo wabane miguu mpaka watakapoolewa
 
Jamani kuwa single mom iwe ni kwa bahati mbaya msitake kuuhalalisha.

Kuna wale wenye uwezo wa kiuchumi hupendelea kuwa ma single mother, na hawa ndio wabaya, wanajivuna na kuwalea watoto vibaya. Lakini wale waliopata kuwa single mom kwa bahati mbaya, na bado wakipata wachumba wanatulia na kuolewa wako poa kabisa.
 
Ila haya maneno makali yanakuja baada ya hao single mothers kuja na very defensive argument zenye maneno makali. Wakati mwingine thread zina lengo la kuwaweka sawa mabinti wasije wakajikuta kwenye hali ambayo hawakutegemea.
Wanakuja na maneno makali baada ya kuchokonolewa,na kama lengo ni kuwaweka mabinti kwanini mnaanza kuwadis single mother why mabinti wasiwekwe sawa bila kuumiza wengine?
 
Waulize hao wanaoponda kwenye ukoo wao dada zao wote wamezalia ndoani?au kujisifu mtandaoni tu
Tena wengine unakuta kwenye ukoo walioolewa na kuzalia kwenye ndoa hata watatu hawafiki wengi ni single mother ila akija hapa anawadisi sana single mother utafikiri kwenye ukoo wake hawapo kumbe wamejaa tele.
 
Back
Top Bottom