Wanaume wa JF, single mothers waliwafanyia nini?

Wanaume wa JF, single mothers waliwafanyia nini?

Kuna watu walio wahi kuwadate single mothers wakaenda poa, ila wengi mambo hayawi mazuri, halafu baba wa mtoto anaweza piga mzigo muda wowote.
Hata wewe single mother mwenyewe sidhani kama ungependa mtoto wako wa kiume aje alee mtoto asiye wake.
Pia uki date na single mothers unafanya double work, umfurahishe mama na mwanae.
*kuna wale ambao walio zaa nao walifariki wana la kujitetea, zaidi ya hapo wanawake kuweni makini siyo kila mwanaume wa kuzaa naye tu.

Mjomba hakuna jambo nisilopenda kama kufuga mateka
 
Hellow JF,

Naomba kuwauliza wanaume mliopo humu JF, hivi single mothers waliwafanyia nini mlio wengi, mbona mnawaandama sana kila kukicha?

Naombeni mnijibu sababu thread zenu zinaumiza sana pia zinachosha as long as sio wote walipenda kuwa single mothers wengine iliwabidi tu, au mlitaka wafanye abortion kuepuka kuwa single mothers?
Ngoja wahucka hao unaowalalamikia waje wakujibu .... sie wengne twakosa majibu coz hatujawah rusha hivo vjembe japo ni wanaume pia wa JF ....
 
Siku zote mwanamke mtu mzima huzaa na mwanaume aliyempenda ila mambo hutuendea kombo tu na hatupendi itokee hivyo, ila Dunia ni uwanja wa mapambano na Mwanamke jasiri huendelea kupambana hata mkiwakosoa muwakosoavyo hatupi mtoto wake
iwe leo iwe kesho nikiwa single mother sitakatishwa tamaa na wanaume wenye akili hasi
Amen.
 
Kwani walishikiwa kisu ili watiwe mimba

Si waliachia mzigo wenyewe[emoji2]

Tema mate chini kijana, haya maisha hayana formula hakuna aijuae kesho isipokuwa Mungu peke yake, mshukuru sana Mungu kama umepata malezi ya baba na mama, lakini si hiyo kauli uliyoiandika hapo.... hakuna mtoto anaependa kulelewa na mama peke yake wala hakuna mama anaependa kulea watoto peke yake, dunia hii ni mapito ati, Mungu akusaidie sana
 
Achana nao wasikuumize kichwa Bora Mimi single mother najitambua na jamii inajua hivyo kuliko wao wanalea watoto wa wanaume wenzeo bila kujua, na wamelelewa na ma Baba ambao si wao

hahahahahahahahahaaha baelezee
 
Tema mate chini kijana, haya maisha hayana formula hakuna aijuae kesho isipokuwa Mungu peke yake, mshukuru sana Mungu kama umepata malezi ya baba na mama, lakini si hiyo kauli uliyoiandika hapo.... hakuna mtoto anaependa kulelewa na mama peke yake wala hakuna mama anaependa kulea watoto peke yake, dunia hii ni mapito ati, Mungu akusaidie sana

thumbs up
 
Hakuna haja ya kuwachukulia vibaya, wanaume wengi tuna watoto njeee. MTU kuwa na tabia mbovu ni yeye siyo kwamba wote wako hivyo. Pia kuna wengi wamelelewa na single mothers hao hao.
 
Back
Top Bottom