Mada nzuri sana lakini umeipapasa papasa tu bila kuzingatia misingi ya kisaikolojia na kijamii utafikiri cheaters hawa ni mawe na wanaishi katika ombwe.
Kijamii (hasa katika jamii za Kiafrika) mfumo dume ndiyo unatawala. Mfumo huu, kwa kiasi kikubwa, unamtegemea mwanaume acheat. Na katika makabila mengi, kuwa na wanawake zaidi ya mmoja ilikuwa ni ishara ya urijali na ukwasi. Ndiyo maana jamii inamhukumu mwanamke anayecheat kwa ukali zaidi kuliko mwanaume (slut vs stud, malaya vs. rijali...)
Kisaikolojia-mwanamke anajulikana kuwa ni kiumbe wa hisia zaidi kuliko mwanaume. Mwanaume yeye anaongozwa na tamaa ya anavyoona (visual stimuli). Na wanawake (subconsciously) wanalijua hili ndiyo maana wanashinda saluni wakijipodoa na hata kujishindilia matako ya bandia ili tu kumvutia mwanaume.
Implication ya mtanziko huu wa hisia vs. visual stimuli ni kwamba mwanaume anaweza kulala na mwanamke na akaondoka bila hisia zo zote akarudi kwa mkewe; na mambo yakawa sawa tu. Kwa mwanamke hali ni tofauti. Akikanyagwa huko nje sawasawa ni lazima ataacha hisia zake huko; na mwanaume kama uko observant utagundua tu hata ajifanye vipi. Dharau za rejareja, kiburi, mabadiliko katika tendo, kutojali na mengineyo yataanza. Ndiyo maana wanasema kuwa ogopa sana mke wako akianza kuchapwa nje. Anahamishia hisia zake huko polepole na akikolezwa huko basi wewe huna chako labda uamue kuwa boya uvumilie.
Kibayolojia - Homo Sapiens ni mnyama na ana instincts zile zile za kinyama. Ukienda Serengeti ukakuta madume ya simba yanapigana kwa kawaida visababishi ni viwili tu - mademu na chakula. Kuna instinct kwa kila kiumbe cha kiume kulala na +ke wengi ili kuhakikisha kwamba DNA yake inarithishwa katika vizazi vijavyo. Ndiyo maana kuna viumbe wachache sana ambao ni pure monogamous. Penguin na mnyoo gani sijui ndiyo hutajwa tajwa sana. Kwa hivyo kibayolojia men are wired to cheat; na huu ni ukweli uliosimikwa katika EvolutionaryBiology. Ndiyo maana ni shughuli pevu kubakia pure monogamous japo inawezekana hasa baada ya kuvuka kipindi cha ujana mtu akijitambua.
Kwa hivyo inasaidia kidogo tukiliweka suala hili katika muktadha sahihi na kulijadili katika mitazamo wezeshi. Kuna sababu za kijamii, kisaikolojia na hata kimaumbile (kibayolojia).
Na hii siyo justification ya kucheat maana kuwa loyal kabisa kabisa kwa mwenzi mmoja inawezekana. Ni suala la kuamua tu!
Na siyo ukweli wa jumla kwamba uki-cheat basi na mwanamke wako naye ata-cheat. Wapo wanawake wanaojitambua na kujiheshimu sana kiasi kwamba hawako tayari kwenda kujidhalilisha na miili yao huko kisa tu eti kulipiza kisasi maana kusema kweli hakuna anayelipizwa kisasi pale. Ila nakubaliana na wewe kwamba mwanaume uki-cheat basi huna uhalali wala moral authority ya kumkataza na kumhukumu mwenza wako pale anapocheat japo cheaters wengi ndiyo wakali kweli kweli kwa wenza wao na huumia mno wenza wao waki-cheat. Mbombo ngafu!