Wanaume walioko humu ambao ningependa kuonana nao face to face

Wanaume walioko humu ambao ningependa kuonana nao face to face

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Nimecheka kwa sauti,
tbh, hakuna mtu nilikuwa natamani kuona anafananaje kama Zero IQ kipindi kile anaandika ujinga mwingi, sahii amepoa na interest imepotea pyuuuh'...!!
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Me nasubiri tu mzee mweusi mwenye kitambi chake aje online
Me naetamani kumuona ni mzabzab nione anayoyaandika yanafanana na yeye au ni nini
 
Mmoja huyu apo
FB_IMG_1674239545095.jpg
 
Kuna mmoja hapo ukitaka kumwona nenda kwenye maduka ya kubeti. Ukiona mtu anafika kavaa tai na suti anaenda kwenye fixture, dakika 2 kashachukua timu 3 anaenda kwa cashier anatoa kibunda ili kufyatua mkeka kisha anaondoka, basi ujue huyo ndio mwana JF unayemtafuta sasa.
 
1. Bill Lugano
2. GENTAMYCINE
3. Chizi Maarifa
4. Deep Pond
5. Viatu vya samaki

Kuna watu huwa nawasoma halafu nawaza watakuwa na sura gani? Umbo gani? Wanavaaje? Wanatembeaje? Wanaishije.

Huyu chizi maarifa nahisi atakuwa ni yale maanaume makorofi yenye sura mbaya mababe, hayana sana akili yanajua kutiana tu labda. Halina mvuto lipo lipo tu ila labda limepata vijicent kidogo so linakuwa na ujeuri sana.

Bill Lugano anaonekana mkaka mstaarabu sana. Msafi anajipenda. Hana ugomvi na very romantic kwa kweli. Sijawahi soma akimtukana mtu au akijibishana na mtu vibaya. Hata kuwatukana wanawake. Siyo kama lichizi maarifa lilivyo.

Gentamycine anaonekana atakuwa mweusi, mfupi, anakitambi kikubwa. Mnene anajipenda sana. Anapenda kuonekana kwenye kundi la watu. Mbishi hapendi kuambiwa kitu amekosea. Akiwa na demu wake ana wivu sana.

Deepond naye mstaarabu ila tu ana michepuko sana. But si mgomvi ana utulivu anaweza kuwa maji ya kunde na kimo cha wastani. Anavaa vizuri pia.

Hao ni wanaume ambao binafsi natamani niwaone nione ufanano wanachoandika na mwonekano wao. Maana kuna mambo mtu anaandika mpaka unawaza atakuaje huyu mtu? Nimeangalia wanaume sababu mimi ni jinsia ya tofauti nao

Ooooh .... Na kuna mwingine Komeo Lachuma huyu anaishi kwa shemeji yake. Nadhani kamaliza form six ila alifail kijijini so hakuendelea na chuo. Kisha akaona maisha ya kule kijijini magumu akaja kuishi kwa dada yake mjini. Anataka kuchukua mademu kupitia hali nzuri ya shemeji na dada yake. Atakuwa mweusi , mrefu wa wastani. Mwembamba nyangema. Ila ana ushamba kiasi flani. Ana ujinga mwingi pia. Maana anaishi na kulishwa na dada yake. Hafikirii kuanzisha maisha yake.

Kuna wakati nawasoma watu sana kisha naanza kujenga picha watakuaje hao watu katika maisha halisi. Najiwazia tu kutokana na wanachoandika
Aisee 🀣
 
Back
Top Bottom