Wanaume wambea wanazidi kuongezeka kwa kasi ya 5G

Wanaume wambea wanazidi kuongezeka kwa kasi ya 5G

Pamoja na kwamba umbea wameumbiwa wanawake kwakuwa inasemwa hawana vifua vya kuhifadhi mambo na makoromea na kuzuia vitu visitoke nje ya mdomo lakini hiyo dhana inatoweka kwa kasi ya ajabu.. Wanaume wa kileo (sio wote) ni wambea mpaka inakera kama sio kutia aibu ama kinyaa

Case studies ni mitandao ya kijamii, online TVs na blogs ambazo nyingi wamiliki na waandishi wake ni vijana wa kiume.. Ukiingia huko utagundua kuna tatizo kubwa na linakuwa kwa kasi ya ajabu
Tumetoka kwenye zama za kujipodoa vijana wa kiume hili sasa limeshazoeleka sio ajabu tena!
Tumetoka kwenye zama za vijana wa kiume kuvaa kike, kutoka masikio, pua, midomo, ndimi na vitovu hili nalo limeshazoeleka si ajabu tena!
Kuna hii enzi ya ushoga pamoja na ukakasi mkubwa wa hili jambo lakini taratibu jamii inaanza kulipokea na kulizoea japo kwa shingo upande na kwa kificho
Hata mapenzi ya siku hizi yana maajabu yake.. Zile dirdo hazitumiwi na wanawake tuu wale wanaosagana bali hutumiwa na wanawake kwa wapenzi wao wa kiume[emoji35]
Kuna mabadiliko makubwa sana ya vinasaba, na haya yanajitokeza zaidi kwa vijana wetu wa kike na wa kiume! Wanaume wa kike siku hizi ni wengi kuliko wanaume wa kiume!

Uvumilivu wa jamii kwenye hayo mambo hapo juu ndio umezaa haya matokeo ya wanaume kuwa wambea..
Mtu anayebadili dini huwa mkali zaidi ya wenye dini yao! Ogopa sana mwanaume akiwa mmbea!

Makuzi na utandawazi, elimu ya jinsia( jando na unyago) iliyopewa kisogo, elimu ya utambuzi isiyopewa umuhimu, kuiga na kutamani kujaribu vyaweza kuwa sababu kuu ya haya matokeo
Pamoja na uhuru tulionao wa kuandika chochote alimradi tu usivunje taratibu na kanuni za jukwaa lakini kuna post nyingi sana zimeandikwa na vijana wa kiume mtu ukiziona unaona hata aibu kuzisoma! Na nyingine zinatia kinyaa kwakweli

Sisi kama wazazi na wazazi tarajiwa natoa rai tuwajenge vijana wetu katika njia sahihi za kimaisha kulingana na jinsia zao
Tuwakemee waziwazi na kuwaonya kwamba hilo halipaswi kufanywa na wewe kutokana na jinsia yako! Lakini tusiishie hapo tu bali tuwajenge kulingana na jinsia zao ili wasije kujuta tukiwa hai uzeeni tukajuta nao ama tukiwa hatupo tena!

Riep warumi View attachment 2768189

Sent using Jamii Forums mobile app
Unayosema ni kweli kabisa mkuu 😀
 
Attachments

  • VID-20230808-WA0009.mp4
    14.7 MB
Hili tatizo ni kubwa mno,ukiona wanaume wako kijiwenu asubuhi mpk jioni mara kwa mara tambua hapo masengenyo yanayopigwa sio ya kitoto...kuna mahali niliwahi ishi,jioni moja nikasema ngoja nikapate elimu mpya ya maisha kwenye kijiwe kimoja cha vijana mchanganyiko wa umri(watu wazima na vijana),..mada nilizokuta pale na kusema watu..tangu ile siku nili azimia nikitoka kwenye majukumu yangu ni nyumbani...bora nikae hapo kutwa nicheki TV...kibaya huyu anayemsengenya mwenzie kazidiwa mbali kimaisha...ukiwa na changamoto ya kimaisha Muombe Mungu wako akusaidie...kinyume na hapo utakua bango la matangazo either ofisini au mtaani kwako.
ukiwa na changamoto ya kimaisha Muombe Mungu wako akusaidie...kinyume na hapo utakua bango la matangazo either ofisini au mtaani kwako.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Innalillahi waiina illahi rajiun
Bro huu ni mtihani sana
Mume wa shamsa alikiri kabisa yeye ni mbea pamoja na mkewe na akasema hapa waalikwa mkitoka tu tunawateta
Mume wa shamsa alikiri kabisa yeye ni mbea pamoja na mkewe na akasema hapa waalikwa mkitoka tu tunawateta[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naunga mkono hoja, ila hata wale wasiofanya hayo wanayafuatilia kisirisiri.
Mfano wewe hii screenshot umeitoa wapi? Bila shaka ulikuwa unafuatilia umbea.
Ila ukweli umeuandika jamii yetu sasa hivi haieleweki watoto wa kiumr wanavaa mavazi kama wanawake.
Imetumwa kwenye kundi sogozi la kitaa lakini pia kuweka ushahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi kama wazazi na wazazi tarajiwa natoa rai tuwajenge vijana wetu katika njia sahihi za kimaisha kulingana na jinsia zao
Tuwakemee waziwazi na kuwaonya kwamba hilo halipaswi kufanywa na wewe kutokana na jinsia yako! Lakini tusiishie hapo tu bali tuwajenge kulingana na jinsia zao ili wasije kujuta tukiwa hai uzeeni tukajuta nao ama tukiwa hatupo tena!

Sent using Jamii Forums mobile app
True mkuu lakini hilo silioni.
Washasema the future is female na dunia imeleta teknolojia ambayo imerahisisha almost kila kitu kiasi kwamba ni ngumu kumlea mtoto wa kiume kwa uanaume wake.

Ila nimefurahi pia kuwa siku hizi kuna kampeni zimeanza kuhusu boy child maana alisahaulika. Natumai kila mmoja kwa nafasi zetu tutafanya kitu
 
Imetumwa kwenye kundi sogozi la kitaa lakini pia kuweka ushahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu. Na jamii ime entertain haya mambo kiasi kwamba karibia kila chombo cha habari kina segement ya umbea na watamgazaji wanalipwa pesa nyingi.
Mimi kwangu walikuwa wapenzi wa ICU ila niliwashawishi wameacha kutazama unless kama wanafanya hivyiw nikiwa sipo.
 
Kwa nini msijisakame wazazi wa siku hizi kwa kushindwa malezi na si kuwatupia lawama zote vijana wa siku hizi[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Makuzi na utandawazi, elimu ya jinsia( jando na unyago) iliyopewa kisogo, elimu ya utambuzi isiyopewa umuhimu, kuiga na kutamani kujaribu vyaweza kuwa sababu kuu ya haya matokeo

Sent using Jamii Forums mobile app

Exactly lakini nadhani pia mafaza wapunguze vikao vya bar ili wapate muda wa kuwafundisha watoto wa kiume kuwa wanaume. Zile zama za tamaduni na jamii kukulelea mtoto zimekwisha
 
True mkuu lakini hilo silioni.
Washasema the future is female na dunia imeleta teknolojia ambayo imerahisisha almost kila kitu kiasi kwamba ni ngumu kumlea mtoto wa kiume kwa uanaume wake.

Ila nimefurahi pia kuwa siku hizi kuna kampeni zimeanza kuhusu boy child maana alisahaulika. Natumai kila mmoja kwa nafasi zetu tutafanya kitu
Aisee teknolojia imefanya malezi ya watoto kuwa magumu.
Mimi nashangaa kuna information watoto wanakuwa nazo hadi unashangaa.
Haya ma insta yanafanya watoto hawataki shule kisa vitu wanavyoona mtandaoni
 
Mkuu zamani tulifungiwa tusione vitu vya kikubwa ili tusipevuke akili kabla ya muda Ila siku hizi watoto wanajua vitu vingi mapema. Kheri uweke ukaribu na mtoto ili umpe elimu sahihi kuliko akaja kupata ya mtaa na ya mitandaoni ambayo itamuharibu. Hakuna njia nyingine salama
 
Malezi yamekuwa shida mkuu. Mimi mwanangu kuna nyimbo sipend azisikilize ila kuna muda nasikia anaimba nyimbo fulani ambazo nikawa najiuliza amezisikia wapi. Kumuuliza ananiambia kwenye school bus na huko shuleni kwenye talents
 
Watu hawataki kwenda kulima, wanataka hela ndio ibadilike iwe chakula, kwa hiyo wanatumia nguvu nyingi kupata hela bila kuangalia madhara ya njia wanazotumia kupata hela.

Suluhisho ni kila mmoja aanzishe ata bustani ya mchina ili aweze kuokoa hizo mia tano mia tano.​
 
Malezi yamekuwa shida mkuu. Mimi mwanangu kuna nyimbo sipend azisikilize ila kuna muda nasikia anaimba nyimbo fulani ambazo nikawa najiuliza amezisikia wapi. Kumuuliza ananiambia kwenye school bus na huko shuleni kwenye talents
Za zuchu hizo 😁😁😁
Ndio anthem za watoto

Mkuu usijiwazishe sana, hakikisha tu unawapa watoto taarifa sahihi ili wawe na uwezo wa kuchambua mambo mwenyewe lakini pia kufanya maamuzi kwa kukushirikisha bila hofu.
 
Mimi nawazaga sana huenda kwenye taulo za kike hizi za kisasa kutakua wanaweka kemikali inayomuingia mwanamke na kujificha kweye homoni zake ili siku akija kuzaa mtoto wa kiume awe na chembe chembe za ukike ndani yake.

Wewe angalia watoto wengi walio zaliwa kipindi cha hapa kati cha matumizi ya taulo nyingi za kisasa na P- 2 utaona kabisa kunautofauti mkubwa. Unakuta mtoto ni wakiume ila amekaa kike kike kabisa sasa umbea utaishaje.

Wanaume wa kike ni wengi sana siku hizi ,wanawake kuweni makini mnapo taka kuolewa angalia kabisa huyo ni mwanaume mwenye uanaume au ni mwanaume mweye ukike ndani yake.

Msiseme hamjaambiwa
 
Umeflow vzr ila hapo mwisho umeharibu kulikuwa na haja gani ya kuweka picha ya mshabiki wa yanga, tofauti ya ww na hao wanaume wa kike itakua ni ID tu Mr mshana
 
Hii ya umbeya nadhani kimtaa imekuwepo siku zote maana ukifuatilia vijiwe vya kahawa au mabar, zinazoongelewa nyingi ni habari za watu.

Tofauti na wanawake, wanaume hakuna kawaida ya kufitinishana na kuzungukana lakini pia dhima ya story huwa ni kwenye kujenga Ila kwa wanawake mfano masaloon, huwa wanasengenya kama sehemu ya kujifurahisha lakini pia kubomoana ndio maana kuzushiana na kuzungukana huwa kwingi.

Mwisho wa yote badala ya kusakama hiki kizazi kipya, lazma mjiulize nyie vizazi vilivyopita, je, mlivyokuzwa ndivyo mlivyowakuza hawa mnaowasema leo hii. Kama mlishindwa, hamuoni kuwa mnapaswa kuona aibu kwa kushuhudia kufeli kwa malezi yenu kama mababa na makaka kuliko kujificha kwenye kichaka cha lawama..

Kwa nini msijisakame wazazi wa siku hizi kwa kushindwa malezi na si kuwatupia lawama zote vijana wa siku hizi
Hongera sana kwa kuwaza nje ya box
 
Mimi nawazaga sana huenda kwenye taulo za kike hizi za kisasa kutakua wanaweka kemikali inayomuingia mwanamke na kujificha kweye homoni zake ili siku akija kuzaa mtoto wa kiume awe na chembe chembe za ukike ndani yake.

Wewe angalia watoto wengi walio zaliwa kipindi cha hapa kati cha matumizi ya taulo nyingi za kisasa na P- 2 utaona kabisa kunautofauti mkubwa. Unakuta mtoto ni wakiume ila amekaa kike kike kabisa sasa umbea utaishaje.

Wanaume wa kike ni wengi sana siku hizi ,wanawake kuweni makini mnapo taka kuolewa angalia kabisa huyo ni mwanaume mwenye uanaume au ni mwanaume mweye ukike ndani yake.

Msiseme hamjaambiwa
Usisingizie taulo hebu waza malezi mwanaume umemzalisha mwanamke huko halafu umekimbia mtoto wako wa kiume analelewaje na mama yake huko?
 
Back
Top Bottom