wanaume wanao ni-approach hawafanani na mimi nisaidieni jamani!

cacico nani anataka mambo ya kupimana status,mwache akae benchi kwanza, akigusa thirty atapunguza vigezo na masharti lolest!!

Kuja bi dada mmoja anakaribia 40 sasa. Bado anaweka vigezo na mashart utafikiri kigoli wa miaka 24 minus. Cha ajabu wenzie hapa ofisini wakiolewa analia hadi kamasi na kwenye harusi haendi kwa uchungu.
 

Hebu anika hapa sifa zako zote tuone kama kweli hakuna wa kufanana na wewe humu!! Naamini tupo wengi tu.
 

Mbona sikuelewi wewe una rank gani? mhh unaanza kunitisha kuwa huelewi unachotaka wewe bibie... hivi unaweza hata kuainisha sifa zako na za mwanaume unayemtaka kwa ufasaha? Manake kwa unavyojidai unataka eliyesoma unanitisha ikiwa huwezi hata kusema wewe ukoje na unayemtaka aweje.
 

Mie sijaandika hii thread kwaajili ya kutafuta mpenzi hapa JF nimeomba ushauri nimepata so ntautumia ushauri huo huku nilipo , thanks
 

Umekiri kuwa kuna wanaume ambao unadhani ni wa status yako lakini hawaji kukutokea, ushauri wangu-'Just make a move towards them' its the time to fight for your love! Unaweza ukawa na qualities ambazo hao wanaume wa status yako hawawezi kuziona kwa mbali. Just make a move for friendship, then over time I hope atatokea ambaye amekuwa interested na wewe na atakutokea. Ukijifanya matawi ya juu, ukajitenga na kusubiri utokewe utadoda!
 
Kuja bi dada mmoja anakaribia 40 sasa. Bado anaweka vigezo na mashart utafikiri kigoli wa miaka 24 minus. Cha ajabu wenzie hapa ofisini wakiolewa analia hadi kamasi na kwenye harusi haendi kwa uchungu.
ha!ha! umenichekesha eti haendi ktk haruc.
 
emu simamia hivyo kama kwel unaona vina tija kwako na lazima uwe na mtazamo wa kuthamini na kiilewa jamii inavyobadilika
 
Ngoja mimi muuza madafu nikae kimyaaaa manake inaonekana huyu mwanadada ana phd ya kusongea ugali ,
 
wanaume wengi wa siku hizi shule matatizo, ambayo inadhuru hata thinking.....
eboo kama ni hivii mimi muuza madafu ngoja nikamtafute demu muuza hoteli manake nilikuwa nataka nioe mwanamke msomi ila mimi muuza madafu stdseven
 
Hana lolote huyo ni nunganyembe tu anajifanya kutaka ushauri kumbe ndo anatafva mwanaume ungekuwa m'ke wa maana ungekuwa ushapana bwana subiri w'me wasiojua kutongoza wataku pm

Chinga boy, mbona umewaka ivo!?
na wewe ni mmojawapo wa wasio level yake nini
maana mmmh! umewakaje?

itakua Soledad alikutema:tongue:
 
u

Ulichosema hapa ni kweli kwamba Mungu umpa mtu mke/mme wa kufanana nae,
Tatizo la Soledad akipewa huyo wa kufanana nae,ye anadai huyo sio wa status yake
What i believe is kinachotoka kwa Mungu kwa maana ya kufananishwa na mwenzi wake
sio hizo sifa anazozitaja bi shost,
bali ni utu,ucha Mungu,kiasi,na mambo yanayofanana na hayo
sio material km status,i don know uhandsome, utajiri n.k

Mungu hawezi mpa mtu alietulia au mcha Mungu akampa mzinzi,mlevi n.k
Bali atamchagulia wa kufanana nae katika hayo....

viangalieni hivi vitu kwa umakini sana
Mtu asijeona ana Elimu, kazi, ni mzuri wa sura na umbo zen akamforce Mungu ampe mtu wa hivyo km atakavyo
Utaishia kusubiri na kujiona una mkosi milele..

ntarudi tenaa!
 
Kuna dada mmoja alisema yeye anataka mwanaume handsome, tall, famous hapa mjini, mwenye masters, nyumba mbezi beach na mkwanja wa maana hhahahaha mpaka leo anaendelea kugawa one night stand tu akiendelea kuchagua huyo handsome! sasa na wewe naona unaelekea huko huko kila la kheri na status yako!!!
 
Sasa, mbona mnamsema vibaya badala ya kumpa ushauri.....?
 
Tatzo vgezo mingi, things kama eliimu na umri ww poteza tu coz life cyo hayo tu ni akili ya kawaida...xory 4dat..
 
Samahani kwa ku-interrupt.
Ukitaka kupata mnaefanana sanaaa ki-fikra n.k. kuanzia sasa anza kutafuta mwanamke mwenzako.
 
Hao wanaokufata wanakuona wewe ni sawa yao na ni wa status yao kabisaaaa! Ila wewe ndio hujitambui kama status yako inafanana nao! Jiangalie na ujipange upya!

huyu anaweza akawa kama huyu paka kwenye avatar yangu, akijiangalia kwenye kioo anajiona yeye ni simba.(hajitambui yeye ni nani)
 
samahani kama nitakuudhi unasema hujapata mnaoendana na wao ujue wenye status kama yako wameona huwafai tatizo umekuwa mchaguaji sana ata ukitongoza wewe inaonyesha hamtadumu miaka 27 hujaona mtu alafu ukute elimu yenyewe degree tu sifa nyingi kwa ushauri tafuta mwanaume ambaye sio tegemezi yani mchapakazi angalia na umri tu vingine sio issue utazeekea home wenzio siku izi umri uo ndo wakuwa na familia yako unazaa unapumzika subiri sana shosti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…