magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 11,075
- 24,634
Mababu namna gani tena?!Yaan nisivae pensi kisa nn kwaiyo unaenda Beach na suruali za mashineni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mababu namna gani tena?!Yaan nisivae pensi kisa nn kwaiyo unaenda Beach na suruali za mashineni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna mmoja nilimuona kavaa kichupi kabisa halafu anahangaika kukashusha..aibu niliona mimi
Ni katika kushindana na Wazee wa Haki Sawa.Vpochi imekuw fashion san , vjan wanavbena hadi unajiulz wamewek nn zaid ya smartphone na kitambaa cha mafua , mwingine anawek na pyfyum asee kizaz kinaisha
Watu mnachekesha hatarii. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwanza kama hujazoea hata pensi ya kawaida huwezi kuvaa na kutoka nayo... Kuna hivi wanavaa skuizi ni kama viutumbo fulani, vinabana ngozi chini wanapiga na viraba vyao hawana habari[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Kuna haja ya jando kurudishwa, maana kuna watu wanashindwa kutambua mipaka ya jinsia zao kwasababu hawakuambiwa kiume zaidi.
Mwanaume kunikia ni vyema, ila kuna tupafyumu twa bei rahis tunanukia mpaka inaumiza kichwa😂Hahahaaa hamna mkuu, labda hiyo kunukia mara moja moja huwa nanukiaga ingawa sidhani kama huwa inafika kwenye kiwango alichosema jamaa hapo juu.
Sasa nani anajali? Em acha kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu.Mwanaume yeyote ukivaa kibukta ambacho kipo juu ya magoti
Marufuku kufika nyumbani kwangu au kuniongelesha [emoji848]
Waambie hao watu, hawana wanalojua.Umewahi fika katavi na usukumani? Wale jamaa wanavaa sketi za kanga au vitenge, banging etc . Na jamaa hawana habari kabisa, na jamii inaona kawaida tu. Fiji wanaume wanavaa sketi.
Hapo sasa.Kwa joto la Dar mnataka kaka zetu wavae majeans na makadeti baadae mnakuja kuwasema wananuka korodani, waacheni wapigwe na upepo jamani joto kali
Ni kweli, perfume ambazo hazina majina ya kueleweka huwa zinakera sana😂Mwanaume kunikia ni vyema, ila kuna tupafyumu twa bei rahis tunanukia mpaka inaumiza kichwa😂
Mkuu naona umeshindwa kumuelewa mtoa hoja. Yeye amewazuia kutokanyaga nyumbani kwake tu sio mtaani. Shida iko wapi mkuu?Sasa nani anajali? Em acha kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu.
Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Karibu umalizie story yako ili tuweze kubalance mzani mkuu.Ukifanya upekuzi na utafiti kwenye mitandao mikubwa(search engines) kama yandex gugu etc na ukatafuta kwa maneno haya machache ya kidhungu
"Scantly dressed African"
[jaribu kutafuta in antiquty] ama hata before colonization ama
kutoka kwenye journals na barua n.k kutoka kwa baadhi ya Wakoloni waliowahi kufika Africa, utagundua hakuna jipya hapa.
Wazungu wametuiga kuvaa vipensi vifupi, kuchora tatoo n.k, kutoboa pua, kuvaa vito vya thamani ikiwa ni pamoja na kuvaa bangiri na hereni kadha wa kadha Wazungu hata kuonyesha matiti kwa wanawake ilikuwa ni kama unatenda dhambi(tambua mpaka kunyonyesha mtoto hadharani walipiga marufuku huko kwao).
Tukija kwa wanaume ndio vile tena, muonekano wa mtu mweusi, hakika, unawasumbua. Mtu ana misuli, yuko cut, six pack natural na ngozi ipo glossy! Sasa hata wale wanaoshindana kwenye mashindano ya kunyanyua vyuma kama the Arnolds, unawakuta wazungu wamejipaka rangi(sun tan) ili waonekane kana wana ngozi nyeusi-which accentuates-ili waonekane kama ni 'wagumu'😅
======nitaendelea====
Yeah, mtoto nitamfanya awe na msimamo na kuwa na tabia ya kutokuiga vitu bila kuvipima kwanza.Hamna unachofanya hapo sasa unakemea wewe akiwa uko mtaani anakutana navyo kwenye TV na n.k
Aisee Dunia ina mambo, kuna hawa awanaotoboa masikio na pua na mbaya zaidi hii inafanywa na watu wanaotambulika kama kioo cha Jamii, katika Dunia hii ukifanikiwa kutambua nafasi yako inatosha mengi yanakanganya katika uhalisia wa maisha.Siku hizi imekuwa desturi kwa baadhi ya wanaume kuvamia fasheni na tabia za kike hadi inaleta wasiwasi. Unamkuta mwanaume kipande cha baba amevaa kipochi cha kike anazurura nacho mtaani hadi unashangaa huyu jamaa vipi? Amerogwa, ni shoga au amezidiwa na homoni za kike?
Hivi hawa wanaume wanaovaa vipochi, tena wanamechisha kabisa, na kutoka navyo mitaani wana nini lakini jamani? Kwanini mtu uvae vitu vya kike? Wengine wanafikia hatua ya kuvaa bangili mikononi mwao. Lakini kuna wanaoenda mbali zaidi hadi kutoga masikio na pua na kuvaa hereni na vipini, mtawalia. Au unamkuta mwanaume kajichafua tatoo mwili mzima utadhani mwali kajipamba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa ndoa. Je, tukisema kwamba hawa wanaume wana homoni za kike au ushoga tutakuwa tumekosea?
View attachment 3264764
Inashangaza na kusikitisha unakutana na mwanaume kajipaka marashi yananuka mtaa mzima. Yaani unapishana naye unakwenda hatua zaidi ya 100 bado unasikia harufu ya marashi? Ukiwabana watu wa aina hii watakuambia eti wamejipaka marashi ya kiume. Ebo!
Kana kwamba haya yote hayatoshi, kuna wimbi kubwa la wanaume wanaotaka kuhalalisha uvaaji wa bukta na boxer na kuingia nazo mitaani. Hivi mwanaume mzima unavaaje bukta unaenda nayo hadi sokoni na kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu na bado unajiona uko sawa? Kama kawaida yao, ukiwauliza kwanini wanafanya hivi watakuambia wanavaa bukta za kiume sio pensi za kike. Kama vipi basi watengenezewe papuchi za kiume wawe wanagawa uroda, isiwe taabu.
View attachment 3264765
Nchi hii ina baadhi ya wanaume wa ovyo na wenye tabia na akili za kike na kishoga kuliko kawaida. Serikali isipoingilia kati na kupiga marufuku huu ushenzi, miaka michache ijayo tutakuwa na taifa la ovyo sana.
Akina Diamond na genge lake wao wanapaka hadi lipu shaina na lipu sitiki!Aisee Dunia ina mambo, kuna hawa awanaotoboa masikio na pua na mbaya zaidi hii inafanywa na watu wanaotambulika kama kioo cha Jamii, katika Dunia hii ukifanikiwa kutambua nafasi yako inatosha mengi yanakanganya katika uhalisia wa maisha.