Naona baadhi ya wachangiaji wanajaribu kujibu swali rahisi kwa kutumia jibu gumu…..na lengo lao hasa ni kutaka kuvuruga mada ili hatimaye mjadala ufike tamati bila jibu kupatikana. Kwanini yasitolewe majibu rahisi kama hoja ilivyo? Mtu unaulizwa 3×2 ni ngapi badala useme ni 6, unaanza ku-complicate jibu kama hivi: 3×2 = 2×3 = 3+3 =2+2+2 =6. Kwa nini usiseme tu kwamba jibu ni 6 badala ya kuleta blaa blaa nyiiiiiiingi? Au mtu unaulizwa ukokotoe eneo la pembetatu, unaanza ku-prove Pythagoras theorem kwanza, halafu ndio unakuja kutoa jawabu. Mzunguko huo wote wa nini?
Sio maana ya mtoa hoja kuanza kutafuta chimbuko au historia ya ukengeufu huu wa kuvaa hereni na mikufu kwa wanaume. Naona baadhi ya wachangiaji mmeanza kuchanganya madesa. Kufananisha usukaji nywele na uvaaji hereni wa wamasai na uvaaji hereni wa wanaume wa makabila mengine ni kutafuta flimsy and cheap excuses za kutaka kukwepa hoja ya msingi. Kwanza hamuwatendei haki wamasai kwa kufananisha uvaaji wao na uvaaji wa makabila mengine. Tangu jadi inajulikana aina ya mavazi ya kimasai na hakuna mtu anayewashangaa kwa kuvaa jinsi wanavyovaa. Ndio maana hawaoni soo kuvaa lubega zao na kutembea na sime na rungu kila bila kujali kama wapo mjini au kijijini.
Huwezi kuhoji kwanini kabila la wamsai wanapenda kuvaa lubega wakati suruali na mashati yapo na wanaweza kuyanunua na kuyavaa. Mtu yeyote akihoji hivyo au akafananisha uvaaji huu na wa raia wengine, basi ujue hayuko vizuri kichwani mwake. Kamwe huwezi kufananisha usukukaji wa wamasai na ule wa kina Diamond & Co. Utakuwa unajaribu kufananisha usiku na giza!
Pia hakuna mtu anayewalaumu wanaume wavaa hereni na mikufu. Tunachokijadili na kujiuliza hapa ni: KWA NINI wavae maurembo kama hayo ambayo, kwa saili yake, ni MAVAZI YA KIKE? Je, wanatamani kuwa wanawake? Na je, wasipovaa hayo makorokoro watapungukiwa nini? Kisingizio kwamba wanakwenda na wakati, na kwamba wana uhuru wa kufanya watakavyo bila kushurutishwa na mtu yeyote, ni sawa na kukubali ukengeufu huu uzoleke kwenye jamii bila kukemewa. Mnataka kuwaziba watu midomo wasiusemee ufirauni huu.
Naomba tuelewane vizuri hapa. Tukitaka hii mada ifikie tamati, tusije na majawabu rahisi kwamba wavaa hereni wanaiga kutokana na utanadawazi au kwamba wanataka kuonekana SEXY! These are lame and bogus excuses that cannot be accepted by anyone, whether frenzy or normal. Sasa tujiulize: Wanaume wanaovaa cheni, shanga, bangili na hereni wanafanya hivyo ili iweje? Na wasipovaa watapungukiwa nini? Je, huu si sawa na uhayawani mwingine wowote ule?
CC:
Ablessed ,
sokwe ,
siafu dume