Wanaume wanaovaa cheni na hereni wanataka nini?


mzee umegonga penyewe!!!
 
Basi kama kila mtu anaongelea mtazamo wake na sio mtazamo wa jamii inayotuzunguka hapa tunapoteza muda tu
 

Naona baadhi ya wachangiaji wanajaribu kujibu swali rahisi kwa kutumia jibu gumu…..na lengo lao hasa ni kutaka kuvuruga mada ili hatimaye mjadala ufike tamati bila jibu kupatikana. Kwanini yasitolewe majibu rahisi kama hoja ilivyo? Mtu unaulizwa 3×2 ni ngapi badala useme ni 6, unaanza ku-complicate jibu kama hivi: 3×2 = 2×3 = 3+3 =2+2+2 =6. Kwa nini usiseme tu kwamba jibu ni 6 badala ya kuleta blaa blaa nyiiiiiiingi? Au mtu unaulizwa ukokotoe eneo la pembetatu, unaanza ku-prove Pythagoras theorem kwanza, halafu ndio unakuja kutoa jawabu. Mzunguko huo wote wa nini?

Sio maana ya mtoa hoja kuanza kutafuta chimbuko au historia ya ukengeufu huu wa kuvaa hereni na mikufu kwa wanaume. Naona baadhi ya wachangiaji mmeanza kuchanganya madesa. Kufananisha usukaji nywele na uvaaji hereni wa wamasai na uvaaji hereni wa wanaume wa makabila mengine ni kutafuta flimsy and cheap excuses za kutaka kukwepa hoja ya msingi. Kwanza hamuwatendei haki wamasai kwa kufananisha uvaaji wao na uvaaji wa makabila mengine. Tangu jadi inajulikana aina ya mavazi ya kimasai na hakuna mtu anayewashangaa kwa kuvaa jinsi wanavyovaa. Ndio maana hawaoni soo kuvaa lubega zao na kutembea na sime na rungu kila bila kujali kama wapo mjini au kijijini.

Huwezi kuhoji kwanini kabila la wamsai wanapenda kuvaa lubega wakati suruali na mashati yapo na wanaweza kuyanunua na kuyavaa. Mtu yeyote akihoji hivyo au akafananisha uvaaji huu na wa raia wengine, basi ujue hayuko vizuri kichwani mwake. Kamwe huwezi kufananisha usukukaji wa wamasai na ule wa kina Diamond & Co. Utakuwa unajaribu kufananisha usiku na giza!

Pia hakuna mtu anayewalaumu wanaume wavaa hereni na mikufu. Tunachokijadili na kujiuliza hapa ni: KWA NINI wavae maurembo kama hayo ambayo, kwa saili yake, ni MAVAZI YA KIKE? Je, wanatamani kuwa wanawake? Na je, wasipovaa hayo makorokoro watapungukiwa nini? Kisingizio kwamba wanakwenda na wakati, na kwamba wana uhuru wa kufanya watakavyo bila kushurutishwa na mtu yeyote, ni sawa na kukubali ukengeufu huu uzoleke kwenye jamii bila kukemewa. Mnataka kuwaziba watu midomo wasiusemee ufirauni huu.

Naomba tuelewane vizuri hapa. Tukitaka hii mada ifikie tamati, tusije na majawabu rahisi kwamba wavaa hereni wanaiga kutokana na utanadawazi au kwamba wanataka kuonekana SEXY! These are lame and bogus excuses that cannot be accepted by anyone, whether frenzy or normal. Sasa tujiulize: Wanaume wanaovaa cheni, shanga, bangili na hereni wanafanya hivyo ili iweje? Na wasipovaa watapungukiwa nini? Je, huu si sawa na uhayawani mwingine wowote ule?

CC: Ablessed , sokwe , siafu dume
 
Last edited by a moderator:

Oooonh you have your background assumptions already!!!!!!!
Basing on what,you know better!!!!!!!
Much as all explanations doesnt ring any of your senses then why not study! !!!!!!?????
Indepth interviews and focus group discussions wont let you down, narrations as well may serve a purpose!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nashukuru na wewe umenote kitu...nmejaribu kuuliza maswali yanayoonesha mfano kwenye jamii yetu badala watu kujibu..wanauliza jamii yetu ni akina nani..as if ukisema jamii ya watanzania watu hawaijui..?! imenisikitisha kidogo kwenye huu mjadala..kwani kuna vitu vipo wazi lkn watu wanatengeneza base za ajabu ajabu za kuvipinga...sishangai baada ya miaka 10 ijayo watu..wanatotea mambo kama haya wakiita ni mabadiliko kwenye jamii.. wakajakutetea ushoga kwa kutumia base kama hizi...kama mtu unamuuliza je anaona kwenda kwa mkwe umevaa hereni ni sawa au sio sawa anashidwa kutoa jibu...anaanza kuuliza mkwe ni nani..mmasai au mzaramo..ili aweze tu kutetea hereni basi baada ya miaka kumi itatumika base hiyo hiyo kuhalalisha ushoga usagaji kwenye jamii
 
Kuiga mambo mabaya harusiwi kwenye jamii..basi tuige na ushoga basi kama kuiga kila kitu ni poa...siongelei moral code zangu naongea za jamii yangu ambayo mm na wewe tumo(zipo set na utamaduni ukichanganya na dini zetu )...naona unakomaa moral code zangu mm naongelea jamii..
 

Labelling haijawahi kuwa dawa ya matatizo ya kijamii! !!!!!!!
Wako mashoga hawavai hereni wala mikufu! !!!!!!
Zeroing in mikufu na hereni towards ushoga ni kukwepa jukumu la kufanya tafiti ili kubaini mzizi wa linaloongelewa!!!!
Nimekupa vitabu na theories, methods of enquiry na kila lihusulo mjadala wa aina hii sasa ni jukumu lako kusoma au kuendelea kuamini unayoamini na.kudhani ndio uhalisia!!!!!!

Nimekuomba jaoo jina la kitabu au mtunzi ili nikasome "mental window" unayojengea hoja mpaka sasa hujataja!!!!!!!!

Maisha ya kudhani na kutaka wengine wadhani unavyodhani wewe ndio yanaishia hivyo!!!!!!
 
Kwa nini unaudhika na maisha ya watu wengine? Ya wengine yanakuhusuje wewe?

Huna yako ya kukushughulisha vya kutosha hadi uanze kuudhika na ya wengine?
 
Kwa nini unaudhika na maisha ya watu wengine? Ya wengine yanakuhusuje wewe?

Huna yako ya kukushughulisha vya kutosha hadi uanze kuudhika na ya wengine?

Kwa msimamo wako huu umekula hasara na si ndogo.
Imagine; Mwanao wa kiume(kama unae ama ukijaaliwa baadae)
Siku anakukuta umetulia sebuleni na mkeo pamoja na wageni wenu wengine,
Kisha anakumbia Baba nina sapraizi nataka niwajulishe nyie pamoja na wageni waliopo.
Wewe, Unakaa mkao wakupata habari mpya tena njema pengine,
Kisha Dume lako la mbegu linakuhabarisha "Nimeamua kuwa Shoga na hivi ninavyosema bwana (Basha wangu)
Yuko njiani anakuja kuwajulia hali wazazi wangu.

Nategemea Upige miruzi ya furaha hapo ama? Si ni Maisha yake?
 
Kwa msimamo wako huu umekula hasara na si ndogo.

Hakuna hasara yoyote niliyokula.

Imagine; Mwanao wa kiume(kama unae ama ukijaaliwa baadae)

Well, huwa sipendi sana kujadili hypotheticals....but oh well.....

Siku anakukuta umetulia sebuleni na mkeo pamoja na wageni wenu wengine,

Okay......

Kisha anakumbia Baba nina sapraizi nataka niwajulishe nyie pamoja na wageni waliopo.

Alrighhhht.........

Wewe, Unakaa mkao wakupata habari mpya tena njema pengine,

Naam.........

Kisha Dume lako la mbegu linakuhabarisha "Nimeamua kuwa Shoga na hivi ninavyosema bwana (Basha wangu)
Yuko njiani anakuja kuwajulia hali wazazi wangu.

Right back at ya! Hivi, mpaka mwanao anaamua kukupasulia mbarika tena mbele ya kadamnasi ya wengine inamaanisha nini? Je, haina maana kwamba tayari atakuwa anaujua msimamo wako kuhusu hayo mambo? Manake kama hajui, kwa nini afanye hivyo mbele ya wote hao? Karukwa na akili?

Okay, tuseme anakwambia hivyo, wewe utamfanya nini? Utampiga? Utamuua? Utachimba ardhi ujifukie? Utachukua kamba ujinyonge? Utasaga sumu unywe?

Utafanya nini wewe kama mwanao wa kiume, aliye mtu mzima mwenye kujitegemea mwenyewe, endapo ataamua kuwa na mwelekeo huo?

Mimi najua nitakachofanya nacho ni sitamfanya chochote. Nitamwacha aishi apendavyo. Si kataka mwenyewe kuwa hivyo.....sasa kama kataka mwenyewe mimi nimfanye nini?

Nategemea Upige miruzi ya furaha hapo ama? Si ni Maisha yake?

Ndiyo, ni maisha yake na wala sitapiga miruzi, nderemo, hoihoi, wala vifijo. Nitasikitika tu, basi.

Wewe utafanya nini? Utampiga ngumi? Makonzi? Mtama au frankiki?
 
Siafu dume,kama kuna mtu ameshindwa kuelewa comments zako ni tabia za uboishi na kutafuta kuhalalisha visivyo halali.

Nimefanya ~"job interviews" nyingi sana sijawahi ona mtu wa kiume kaja na pete,cheni,hereni,na utumbo mwingine.Hata hao wamasai hawavai lubega,wote wanakuwa smart kwani ndivyo jamii inataka hata kama malezi na makuzi yako wazazi wako walikuruhusu kuvaa hayo makitu.

ILA KUPAMBANA NA USHOGA KAZI KWELI KWELI.
 


Tatizo la wasomi wetu wa kiafrika ni kusoma bila kuelimika! Sasa huyu naye na medical school aliyosoma tunamwita msomi katika jamii yetu ila je ameelimika au elimu aliyoenda kupata ni ya kukariri tu na kucopy and paste.
Au mpaka msomi wewe uone wazungu wamekubali kanahapo chini ndio nawewe utakubali na kutambua utamaduni wako nasikitika sana. Nimeamua kutumia picha ili hata wenye uelewa mdogo waelewe.
 

Hehehe majibu unayo sema huyataki tu. Sasa kama usukaji wa Diamond ni tofauti na wa mmasai sijui naanzeje kujadiliana na wewe hapo!? Style hio hio akisuka mmasai ni poa lakini mwingine ni ushoga!! Aisee.
Kama mkufu na bangili anazovaa mmasai wa kiume nikichukua halafu nivae mimi basi zinakua ni urembo wa kike, sijui hio metamorphis imetokeaje hapo! Hehehehe! Elimu za kukariri zina kazi sana.
Cultural norms are very dynamic and relative tpaul, hio jamii unayoitetea hapa kuwa inaona kuvaa bangili, hereni, kusuka na kadhalika kuwa ni UKIKE nafikiri ni jamii ya kichwani kwako! Hapa hapa bongo kuna ma director wa kampuni za maana tu wamesuka rasta, mwingine namfahamu ana hereni. Sasa sijui ni jamii gani hio ambayo ni abnormal.
 

Umefanya interview za kada gani!!!!????
Unajua group norms and subcultures!!!?????
Hawaji kwenye interviews zako sababu wanajua their norms are not in line with what your vacancies require!!!!!Period, au ulitaka waje tu ili uwakatae roho yako ikupe ushujaa wa kuwa strict!!!!!???????

Kupambana na ushoga ni kazi kubwa kwa watu wa aina yako mnaotaka superficial treatments ya observables while there are underlying mechanisms and other unobservable influences that sums up in what you think it is a mere observation if not a coincidence!!!!!! !!!!!!!
 
Eti unakutana na mwanaume njian kavaa shanga kiunoni,naam naye anasema ni kwenda na wakati na /au yeye huko huru kuishi atakavyo!
 
itatumika base hiyo hiyo kuhalalisha ushoga usagaji kwenye jamii
Mkuu ukiwa mwaminifu kwa nafsi yako je ushoga na usagaji hapa kwetu haupo kweli. Hao waliohalalisha kwenye nchi zao haina maana kwamba wao wana mashoga wengi kuliko sisi, je huoni kuwa vitendo hivi hapa kwetu vimeshamiri hadi mwanaume akimfumania mkewe basi hawara wa mwanamke huingiliwa kinyume na maumbile. Uliwahi kuona wanajamii wakipinga ufirauni huu badala yake wameuita mchezo huu tigo, tujiulize je hao huwa wamevaa hereni. Kumbuka kuna kijana aliuawa kwa kuliwa na mbwa maeneo ya bichi wakati wanatigoana , kijana yule alikua havai hereni lkn alikua si riziki.

Unajua mjadala huu ni ngumu kufikia muafaka kwa sababu tayari tulisha fikia hukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…