Mkuu, hivyo vyote ni vifaa vya kike tu. Pete ukishafanyia shoo siku ya kufungua ndoa, ukifika nyumbani ivue na kuihifadhi kwenye sanduku kwa ajili ya kumbukumbu, sio kutwa kucha umevaa mipete hadi vidole vinachimbika wewe umengangania mipete ya kike! umeona eeh?
Wanaume kama mabinti. Micheni, mihereni, poda, kutinda nyusi yote haya nimeyaona yanafanywa na baadhi ya wanaume wa siku hizi... basi mkafanye surgery mjiwekee na matiti ili mvae hadi brazia...mfyuuuuuuuu
Wewe kama huna pesa za kununulia cheni na saa za maana kaa kule, tuachie sisi wenye pesa zetu tuvae, usilete umasikini wako hapa!
Ila hata viongozi wa dini zote kubwa yaani waislam na wakristo wanasisitiza wanandoa hata baada ya ndoa zao wazivae ili kuondoa/kupunguza usumbufu na maswali maswali mkuu.
Hivi una umri gani wewe? Samahani lakini nataka nijue ili ninapokujibu nijue namjibu mtu wa aina gani.
Bila samahani Mkuu,ila ukinisaidia kwanza nipate muafaka ktk hili ni vizuri zaidi coz its so confusing,kuhusu umri it doesnt matter alot kwa issue hii as long as tunaelewana mkuu.
mleta mada sijui unaishi wapi dunia hii ya sasa,kuvaa cheni unaona dhambi?bora hata hereni cheni!enzi hizi za insta na fcbk we bado uko enzi za ujima aisee,yaani kwakweli nyie ndio watu ambao mnatakiwa kurudishwa kwenu huko vijijini mlikotoroka mkaendelea kulima viazi.
maana kwa mtu kama wewe huna faida ya kuishi mjini kama sio duniani kabisa.kha
Mbona wamasai mwanaume ndo naeongoza kwa kuweka urembo mwln mwake? Tuwaitaje sasa,,,, acha wivu mkuu dunia inasonga we endelea kukaa
Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
Siku hizi ni kawaida kumkuta mwanaume amevaa cheni shingoni au hereni masikioni. Tena utamkuta mwanaume mwenye akili zilizotimia (achilia mbali mateja) amevaa hereni na cheni kubwa huku akijiona mjanja! Huu ni ujanja au ni dalili za kukengeuka?
Tangu dunia hii ilipoumbwa, inajulikana kwamba urembo ni kwa ajili ya wanawake. Mwanaume hata ukiwa rafu ni pouwa tu--hakuna mtu atakayekushangaa, tofauti na ilivyo kwa wanawake. Mwanamke ni kiumbe anayejisikia kuonekana nadhifu na mrembo nyakati zote. Hivyo hupenda kuvaa vifaa vya urembo kama vile hereni, mikufu, pete, vidani, bangili, nk. Sasa wale wanaume wanaovaa vifaa hivi vya KIKE tuwaweke fungu gani? Si wavae na sketi kabisa ili tujue moja?
Kwa kweli wanaume wenzangu wanaovaa pete, hereni na mikufu wananiudhi sana. Mimi siwezi hata kuvaa saa kwa kuwa inanifanya nijihisi nimevaa bangili! Sasa iweje wanaume na ndevu zao watamani kuvaa urembo wa kike?
Naomba tujadiliane BILA JAZBA hadi jibu lipatikane. Samahani sana, najua hata humu JF wavaa hereni wamo.
mi navaa cheni na saa labda ungeniambia heleni tu ningekuelewa... cheni na saa vina tatizo gani, na nani alikuja akasema hivi ni vya mwanamke? designer wenyewe wanaandika "for men" sasa sijui wewe hayo yako umetoa wapi
Wengine na "lipshine" juu....ni upungufu wa kisaikolojia hivyo hutaka kufidia na vitu kama hivyo. utanashati kwa mwanaume ni muhimu lakini isiwe too much! unamkuta mtu kavaa cheap jewerls kibao, cheap perfumes mpaka anakera na vikolombwezo kibao
Sidhan kama cheni ina shida..mkuu labda huna hela ya kununua silver useme!!
Micheni mikubwa kama ile wanayovalishwa mbwa au?
Eti bana! Nyie mitoto ya siku hizi... wacha tu!!Mwanaume aonekane sex ili iweje? Atongozwe?