Wanaume wanaoweza kuoa Mwanamke mwenye watoto/single mothers wanaroho nzuri na ya kipekee sana, Mungu awabariki

Wanaume wanaoweza kuoa Mwanamke mwenye watoto/single mothers wanaroho nzuri na ya kipekee sana, Mungu awabariki

Bigbootylover

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
2,847
Reaction score
1,828
Popote ulipo ikiwa uliweza au umeweza kuoa mwanamke ambaye ulimkuta na mtoto au watoto tayari, basi una roho ya nzuri sana na Mungu akubariki sana.

Binafsi mwanamke nispomkuta na usichana wake tu inakuwa tabu sana kumuwazia ndoa, naona kabisa napita tu hapa haolewi mtu, lakini kuna wanaume wengine anamkuta mtu ana watoto na baba yao yupo hai, anamuoa huyo mwanamke aliyezalishwa na anawahudumia watoto wake bila shida.

Na wakati mwingine kama jamaa mwenye watoto yupo hai, huyo mwanaume anaweza mruhusu kabisa jamaa aje kuwaona watoto au huyo mama awapeleke watoto "kwao". Au anaweza simuliwa na mkewe, baba fulani alipiga kuomba kuongea na wanae na mwanaume anaruhusu bila shida. Mnawezaje? Binafsi nikiwa na mahusiano na mwanamke tu halafu ikatokea akaongelea habari za ex wake tu roho inaniuma sana. Sasa najiuliza hawa wanaume wanawezaje?

Yaani uko na evidence kabisa mpaka watoto wa mwanaume Mwenzako? Unawahudumia, unamruhusu kuja kuwaona, unaruhusu mkeo aongee nae na saa zingine mpaka anakusimulia.....aaaah mbarikiwe sana ndugu zetu maana mnaroho za kipekee.

MUNGU AWABARIKI.
 
Maisha ukiyafahamu hayakusumbui....wanaume tu ndo wanayaweza haya mambo I mean wanaume.Ndoa ni mume na mke,watoto ni kama ndugu wengine home kwako utawahudumia tu kama unavyohudumia wengine.Kama una roho ya uchoyo na ubinafsi si watoto tu hata nduguzo hutopenda huwaone kwako.Haya ni maisha tu🙏
 
Maisha ukiyafahamu hayakusumbui....wanaume tu ndo wanayaweza haya mambo I mean wanaume.Ndoa ni mume na mke,watoto ni kama ndugu wengine home kwako utawahudumia tu kama unavyohudumia wengine.Kama una roho ya uchoyo na ubinafsi si watoto tu hata nduguzo hutopenda huwaone kwako.Haya ni maisha tu[emoji120]
"Maisha ukiyafahamu hayakusumbui"... asante mkuu
 
Maisha ukiyafahamu hayakusumbui....wanaume tu ndo wanayaweza haya mambo I mean wanaume.Ndoa ni mume na mke,watoto ni kama ndugu wengine home kwako utawahudumia tu kama unavyohudumia wengine.Kama una roho ya uchoyo na ubinafsi si watoto tu hata nduguzo hutopenda huwaone kwako.Haya ni maisha tu[emoji120]
Uzi ufungwe mwamba kaelezea kwa undani
 
Popote ulipo ikiwa uliweza au umeweza kuoa mwanamke ambaye ulimkuta na mtoto au watoto tayari, basi una roho ya nzuri sana na Mungu akubariki sana.
Kuna siku utalea watoto wa wenzako ukiwa huko huko kwenye ndoa, unajikuta tu vitoto viizi, vina kiburi unatafuta hata mfanano kwenye familia yenu huoni, so kuanza 0-0 sio kigezo cha wewe kutokuoea watoto wa watu
 
Kumbe nina roho mbaya. Sikujua before.

I hate single mothers
 
Ni rahisi mwanaume asiye na mtoto kuoa single mother kuliko mwanamke asiye na mtoto kuolewa na single father USINIULIZE KWA NINI MAANA HATA MIMI SIJUI
And vice versa is true! Wanaume wengi tu sana watt kabla hawajaoa,na wameoa vzr tu!
 
Back
Top Bottom