Wanaume Wanapendana Kuliko Wanavyowapenda Wanawake | Kainetics

Wanaume Wanapendana Kuliko Wanavyowapenda Wanawake | Kainetics

Kainetics

Senior Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
135
Reaction score
276
Picsart_22-08-08_06-55-26-750.jpg

Habari wana JamiiForums, kwa wanaume wenzangu ambao watakuwa offended na title ya thread, mtanisamehe kwa muda ila nadhani kufikia mwisho wa kusoma yote nitakayoandika; tutakubaliana kuwa hii ni kweli.

Kama wewe ni mwanamama, nadhani observations kadhaa wa kadhaa nitakazoorodhesha zitakuwa sio ngeni kwako pia, na tunaweza kubaliana kuwa ni moja ya mahusiano yenye nguvu kuliko mahusiano mengine yaliyopo baina ya binadamu nikimaanisha yana nguvu kuliko ndoa, mahusiano baina ya wanawake kwa wanawake, japo sina uhakika kama yanazidi mahusiano kati ya mama na mwanae.

Bila kupoteza muda, hii ni 'Kwanini Wanaume Wanapendana Kuliko Wanavyowapenda Wanawake.' Hata kama wengi wao Hawafahamu.

Disclaimer: Thread hii haihusiani na Ushoga.

Utangulizi

Kwanza kabisa, nianze kwa kutanguliza kuwa mimi ni mwanaume, nna mke ambae tunapendana sana na tumebahatika kuwa na watoto wawili. Kwa mara ya kwanza nilipokutana na hii concept nzima ilinichanganya kidogo na kunistua, ila baada ya muda ilibidi nikubali kuwa ni kitu ambacho kipo ndani ya nature yetu moja kwa moja, na kiliacha nipa shida as long as hakikuwa kinaingilia maisha yangu au kubadili hisia zangu kiujumla.

Concept husika ni kitu ambacho kwa lugha ya wenzetu kinaitwa Bromance ambacho kwa tafsiri isiyo rasmi tunaweza kitambua kuwa zile hisia tu zisizo na madhara ambazo mwanaume anakuwa nazo kwa wenzie, yaani marafiki. Au Washikaji. (Sijui kama naitafsiri kwa usahihi)

Huu urafiki baina ya wanaume ndio unaenda kuwa point ya thread hii na kwanini kuna muafaka kama huo (kuwa wanaume wanapendana kuliko wanawake wanavyopendana, na kuliko wanavyowapenda wanaume pia.)

Tuongelee Urafiki.

Mtoto huanza kujenga tabia ya kujitengeneza marafiki akifikisha umri wa miaka mitano hadi saba, hii haijalishi kama ni mvulana au msichana. Pale anapokaribia au anapoingia katika balehe, yeye na hisia zake kiujumla huanza vutiwa na jinsia tofauti.
Kama ni mvulana, ataanza wataka wasichana na vivyo hivyo mschana hujaribu anza vuta attention ya wavulana. Ila hii haimaanishi jinsia hizi mbili hupoteza marafiki zao.

Japo kuwa watakuwa wakivutiwa na jinsia tofauti, marafiki zao wa karibu bado hubaki kuwa wa jinsia yao ile ile. Wavulana watabaki na washkaji zao kadri watakvyokuwa na hata wasichana watakuwa na marafiki wa kike kwenye inner circle zao huku wakiwa na marafiki wachache wa jinsia tofauti.

Ni kwenye tofauti ya aina hizi mbili za Urafiki; Ushkaji wa wavulana na Ubest wa Wasichana, ambapo tunakiona kile nlichojaribu kukiongelea kwenye title ya thread.

Urafiki Aina A: Wanaume na Wanaume

Kwanza kabisa, urafiki wa kiume hauhitaji sababu kibao kutokea. Tunaweza kubaliana kuwa unatokea tu. Na ukitokea, yapo mambo machache mno ambayo yanaweza yakauvunja.

Na hata ukivunjika, wanaume sio rahisi kutunziana vinyongo, au chuki. Ni aidha watakuwa marafiki , watakosana na watakuwa tena marafiki. Ikiwa ni kosa ambalo halisemeheki, basi kila mtu ataendelea na maisha yake, na salamu za hapa na pale, hata kusaidiana, kutakuwepo. Kitu ambacho hatuwezi kukiona kwenye urafiki wa watoto wa kike.

Kwenye urafiki wa kike, wasichana au wanawake huitaji sababu kadhaa wa kadhaa ili kuweza kupatana. Hobbies, interests, ideologies na beliefs lazima ziwe zinafanana kwa asilimia zadi ya themanini ili huo urafiki uweze kudumu kwa muda, mbali na hapo watachokana ndani ya wiki kadhaa.

Pia,wakikosana sio rahisi kusamehana , na wanaweza tunziana visa na chuki hata kwa miaka kumi. Naongelea kufikia hatua ya kutosemeshana au kufanyiana vituko miaka nenda rudi.

Mbili ni swala zima la Faragha, Uaminifu na Loyalty. Ukisikia wanaume ni marafiki, tayari bila hata kuambizana, watakuwa na code ambayo hawawezi vuka likija swala la uaminifu au loyalty.

Hutokuja sikia wanaume wanakaa sehemu wanaanza ongelea mambo ya chumbani/ au mapungufu ya wake zao. Hio ni code ambayo ipo . Tunaweza kaa tukaongelea wanawake na mambo kibao lakini hilo swala haliwezi ingia kwenye convo.

Kwenye uaminifu, shida kubwa utakayokutana nayo ambayo inaweza ata vunja uaminifu ni ukileta habari za hela, kuazimishana, nk. Na hii ni fact amayo inajulikana. Ila bado ni ngumu kumkuta mwanaume anaazima hela kwa mwanamke.

Hio kitu ni mara chache sana kuwepo. Tunaweza sema wako tayari kuaminiana japo kuwa wanajua uaminifu unaweza ukavunjwa. Pia mambo za usnitch ni mara chache kuzikuta kwa marafiki ambao wamekuwepo kwa muda.

Tukija kwenye loyalty, naweza kupa statement simple ambayo inaweza kuwa hivi; Ni rahisi kukuta kwenye harusi yoyote ile, Bestman wa mwanaume huwa mtu ambae amekuwepo almost zaidi ya miaka mitano na kuendelea.

Anaweza hata kuwa rafiki wa toka utotoni, ila ma maid wengi kwa upande wa mwanamke, huwa marafiki wa hivi karibuni. Na baada ya ndoa hata huo urafiki huweza pungua kama ma bridesmaids wenyewe hawajaolewa.

Urafiki Aina B: Wanawake Kwa Wanawake

Kwenye mambo kama faragha, usiri na uaminifu, kwa kama asilimia tisini, ni kinyume tukija kwa wanawake. Wengi wao swala la Privacy hawana, utakuta wanaweza kaa wakaongelea sex life yao bila shida. Unaweza kuwa mwanaume huna hili wala lile na rafiki wa mkeo anafahamu hadi unavyofanana ukiwa uchi, kutokana na convo zao.

Pia ,wao kwa wao hawaaminiani, japo kuwa wanaambizana mambo nyeti kama hayo. Ni rahisi mambo kusambazwa baina ya wao kwa wao kuliko ilivyo kwetu maana mara nyingi utakuwa best friend wa mwanamke mmoja wapo, nae ana best friend wake so cycle huendelea. So kukuta wanawake wanaofichiana siri ni ngumu mno. Kama unae, na uko mwanamke, mtunze.

Urafiki Aina C: Wanaume na Wanawake

Kuna urafiki ambao sijaongelea, ule wa baina ya mvulana na msichana/mwanaume kwa mwanamke usio wa kimapenzi na hata wa kimapenzi. Bila kujali kuwa mmejuana toka utotoni au mmejuana jana, kama wewe ni mwanamke fahamu kuwa huyo rafiki yako wa kiume ameshawaza kukukula, at one point in hi head. Hata kama haoneshi any interest na hata kama anafahamu umeolewa au uma boyfriend. Ni nature.

Nadhani hakuna kitu kama urafiki baina ya mwanaume na mwanamke. Attraction hufanya kazi kwa subconscious level, na by nature lazima hizo homones atapambana nazo tu labda kuwa gentleman au tu kwa kuwa kuna kule kujiheshimu, na maadili ya kutovunja nk. Ila mbali na hapo, ukimpea chance yoyote hata kimatani... Utaona.

Huu urafiki ninaweza uita aina ya Interest, na interest za mwanume kwa mwanamke ambae sio ndugu lazima kwa hapa na pale zita involve hichi sex. Mwanamke anaweza kuwa tu rafiki na wewe na asiweze kukuweka kichwani sexually kwa kuwa ni kwao ni kawaida ia kwa wanaume ni ngumu.

Na kama anakutaka, bado haimaanishi mahusiano yenu yatakuja yazidi mahusiano yake na washikaji zake. Iko hivi; Mwanaume anaweza angaika miezi kadhaa kukupata, lakini ikiwa hamtopatana utaondoka na atabakia na marafiki wale wale. Kama wewe ni mwanaume utakuta ushawahi kuwa na girlfriends nane ila cycle yako ya marafiki ambao hata muda mwingi huna time nao, hubaki wale wale.

Kwa msichana au mwanamke, unaweza jiuliza umeachana na marafiki zako wa kike wa ngapi kulinganisha maboyfriends. Utakuta idadi ya wenzio ni nyingi, kitu ambacho ni vice versa kwa wanaume .

Tuongelee Motisha na Inspiration Kiujumla.

Karibia kila binadamu ana watu wanao mu inspire kwenye maisha, ana favourite celebrities wake, wanamuziki pendwa, michezo aayopenda fuatilia, nk.

Kwa wanaume, utakuta role model, mtu anae mu inspire ku hustle, au kuwa fit, au idea yake ya maisha yenye furaha, huwa mwanaume mwenzie. Na kwa asilimia karibia tisini huona mazuri yake peke ake. Sio rahisi kukuta mwanume anakuwa inspired na umaarufu au maisha ya kifahafi ya Uwoya au Nick Minaj.

Unaweza kuta pia hata kimuziki, favourite artists ni wakiume na hata kama ana nyimbo iliyoimbwa na msanii wa kike anayopenda, hutomkuta anaiimba publically, japo siku hizi hii inaenda kuwa norm. Sema bado idea ya kukuta mwanaume ana confess ni fan wa Zuchu haijakaa sawa kwa wengi hata kama haina shida. Kwa wasichana, idea yao ya maisha mazuri, fitness au utajiri sio lazima iwe ya wanawake wenzio...na hata kama role models wao ni wa kike, huona mazuri na mapungufu ya hao role models pia. Ni rahisi msichana au mwanamke kupenda nymbo ya msanii wa kiume kuiimba freely pia.

Kwenye mpira wa miguu wa kiume jinsia zote mbili huwa fans wa damu, nk. Ila ni ngumu kumkuta mwanume ansfuatilia ligi ya mpira sa miguu wa wanawake, au netball. Hio haipo, na iko kwenye nature.

Itimisho.

Mifano inaweza endelea mingi tu, na tunaweza kubaliana kuwa mahusiano haya ya kshakaji yana tendency ya kuwa strong kuliko hayo mahusiano mengine. Ni kama kuna written rule ndani ya DNA inayomfanya mwanaume avalue mahusiano/urafiki wake na wanaume wenzie. Na mwanmke anapoingia kwenye picha, most of the time ni kwa malngo ya kujamiiana au kutengeneza familia au tamaa. Mwaaume atake kwambia tofauti na hapo, atakuwa anadanganya.

Kwa wanawake, sense yao ya attraction kwa jinsia yetu iko strong na inavuka mipaka ya interests walizo nazo baina yao wao kwa wao. I mean, nafaham wanawake wachachd ambao wanafuatilia huo mpira wa miguu wa kike kwa mfano 🙂

Nakaribisha maoni yenu kuhusu hili. Kwako imekaeje? Ulikua uliwahi lifanyia observation au ndo mara ya kwanza unaliweka kichwani?

Nawasilisha.
Kainetics

🏷 Telegram Channel : Kainetics Blog 🇹🇿
🏷 Blog : Kainetics
 
Wanaume wengi wanapendana, upendo wao siyo wa kinafiki, hata kusaidiana wanasaidiana.

Hata ndoa nyingi wenye shida ni wanawake.

Tabia za kuzaliwa nazo, wakiongeza na vitabia vya shule/vyuo na tabia za mashosti, wanawake wanakua na roho mbaya ever.

Miaka ijayo hope after this karne, ndoa zitabakia chache sana, watu hawatavumiliana, wanawake hawakunjiki.

Anyway ngoja tuone
 
Wanaume wengi wanapendana, upendo wao siyo wa kinafiki, hata kusaidiana wanasaidiana.

Hata ndoa nyingi wenye shida ni wanawake.

Tabia za kuzaliwa nazo, wakiongeza na vitabia vya shule/vyuo na tabia za mashosti, wanawake wanakua na roho mbaya ever.

Miaka ijayo hope after this karne, ndoa zitabakia chache sana, watu hawatavumiliana, wanawake hawakunjiki.

Anyway ngoja tuone
Hio ya ndoa kutokuwepo kabisa kwa siku za ivi karibuni ni kama vile naiona
 
Kwenye relationship ya wanaume, wote wakiwa single kiaina....kunakuwa na uelewano mkubwa sana. Kuanzia kuchill, mazoezi, kupanga mbinu za kutafta shilingi n.k.

Ngori inaanzia pale mmoja wao kapata mwanamke..... Yani...pale mwanamke anapoingilia kati. Dynamic inabadilika. Kama kulikuwa na progress inakuwa slow sana.
 
Kwenye relationship ya wanaume, wote wakiwa single kiaina....kunakuwa na uelewano mkubwa sana. Kuanzia kuchill, mazoezi, kupanga mbinu za kutafta shilingi n.k.

Ngori inaanzia pale mmoja wao kapata mwanamke..... Yani...pale mwanamke anapoingilia kati. Dynamic inabadilika. Kama kulikuwa na progress inakuwa slow sana.
Hii sijui nini inaielezea... Au ndo tuiite break up ya kimya kimya
 
Hii sijui nini inaielezea... Au ndo tuiite break up ya kimya kimya
Wanaume huwa hawa break up... ni kila mtu anaanza kujipa shughuli kivyake. Kama mlikuwa mnasupportiana...inakuwa hakuna tena iyo. Mara mchizi aanze kujazwa maneno na demu wake "hao rafiki zako hawakusaidii" mara "its just me and you against the world"...upuuzi mtupu. Inaitwa kuendeshwa na mbususu.
 
Wanaume huwa hawa break up... ni kila mtu anaanza kujipa shughuli kivyake. Kama mlikuwa mnasupportiana...inakuwa hakuna tena iyo. Mara mchizi aanze kujazwa maneno na demu wake "hao rafiki zako hawakusaidii" mara "its just me and you against the world"...upuuzi mtupu. Inaitwa kuendeshwa na mbususu.
Haha kuendeshwa na mbususu... Nimekupata mkuu
 
Back
Top Bottom