Wanaume watatu zaidi wamemshutumu Sean "Diddy" Combs kwa ubakaji na unyanyasaji wa kingono katika kundi la kesi mpya zinazodai mwanamuziki huyo wa rap aliwapatia dawa za kulevya na kuwanyanyasa.
Malalamiko hayo, yaliyowasilishwa kando katika Mahakama Kuu ya New York siku ya Alhamisi, yanahusisha matukio ambayo yanadaiwa kutokea kati ya mwaka 2019 hadi 2022.
Wanaume wawili kati yao wanadai kuwa walienda kwenye tafrija na Bw. Combs, ambapo "binafsi aliwapa" vinywaji vya pombe vilivyowafanya kupoteza fahamu, kabla ya kuwabaka.
Mawakili wa rapa huyo walitupilia mbali kesi hizo na kuzitaja kuwa "zimejaa uongo". Diddy anaendelea kuzuiliwa katika jela ya Brooklyn.