Hehehe. . .
Well nashindwa kukubaliana na wewe kwasababu hao wanaume wanaodeka sio kama wanadeka kila mahali, kila wakati na kwa kila mtu. Wakiwa nje, kwenye shughuli zao wanafanya kazi wanayotakiwa kufanya nasio wanakaa nyuma ya dawati na kudeka.Then akirudi kwa mkewe anadeka kwasababu ni haki yake, hana haja ya kua firm na mkewe 24/7. . .unless he has control issues.
Hata wewe unaeonyesha kukataa hii hali sidhani kama unapokuaga na bibi nyumbani hua unamkoromea tu muda wote au uso umekunja kama vile unameza klorokwini.Sidhani mnapokua chumbani unamwagiza tu bila kumpa nafasi ya yeye kukufanyia atakavyo.
All in all kuna aina nyingi za kudeka.
Hata kukaa mezani na kusubiria mpaka mikono unawishwe ni kudeka kwa aina yake. Kinachotofautiana ni kiasi tu na namna.