Wanawake wanasema kuolewa ni BAHATI, na sisi wanaume tunasema kuoa ni Maamuzi.
Kwa sasa idadi ya manaume wenye mpango wa kufanya maamuzi ya kuoa ni wachache sana, hii inatokana na ndoa kuwa na usaliti mwingi, ukizingatia wanandoa siku hizi wanachepuka hadharani, hii husababisha ambao hawajaoa wafikirie mara 3 kabla ya kuoa.
Pia wanawake siku hizi wamekuwa na ufahamu mkubwa, hii husababisha wanaume wengi kuwagwaya (kuwaogopa) kuwaoa, kwani kiasili mwanaume hupenda kuwa juu ya mwanamke kwa kila kitu.
Kwa kifupi wanaume tunapenda mwanamke asiyejua sana vitu, asiyechepuka, mpole, msafi, anayejua wajibu wa mke na mwenye upendo.