Wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya Wanawake

Wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya Wanawake

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Mi nimeleta maada hapo tujifunze wewe unaanza mambo ya copy na paste umekuwa computer?@sonnita
Hahahaha,hapanaa,kama hujui nikuambie tuu siku ingine usirudie kosa.
Content unayoweka publicly especially kwa maandishi kama sio kazi yako ni vizuri kum-acknowledge owner(ulipoitoa).
Usifanye kavile wewe ndo mhusika mkuu. Ni hayo tuu.
 
Mke wangu mimi elimu yake ni darasa la saba, mimi nimemaliza chuo kikuu ni mhasibu nafanya kazi benki na nina mshahara mkubwa tu. Nilikutana na mke wangu kipindi kaja kuchukua mkopo wa Biashara yake, wakati huo nilikua afisa mikopo. Alinielezea kuhusu Biashara yake, plan zake na namna alivyoanza Biashara nilimuambia ondoka uje kesho.

Lakini alipokua anaondoka nilimuita dada mmoja rafiki yangu na kumuambia nitamuoa yule dada, yule ndiyo mke wangu. Hakuamini lakini nilimtongoza nikampata na sasa hivi ni mke wangu.

Ana akili sana huyu mwanamke, kabla ya kumuoa nilikua nishafanya kazi miaka tisa, nilikua na Gari tena ya mkopo na kiwanja tu. Nilijua sina akili kama yeye hivyo nilimuongezea mtaji kwenye Biashara yake na kumuacha afanye "miujiza" yake maana mimi naiita miujiza. Sasa hivi ndoa yangu ina miaka sita, tuna nyumba mbili, viwanja vitatu maduka mawili makubwa ambayo tunasimamia wote na vitu vingine vingi. Ingawa majina katika hati ni yetu wote wawili lakini ndani ya nafsi yangu nakiri hakuna chakwangu hapo.

Mwaka jana mke wangu aliniambia kuwa anatamani kuwajengea nyumba wazazi wake, nikaridhia ombi lake. Kwetu kuna nyumba kubwa tu ambayo tulijenga na ndugu zangu na nahudumia kama kawaida. Alipoanza kujenga nikaona ndugu zangu kama nyuki, wanavamia na maneno, kunijaza kuwa nimetekwa sijui na maujinga ujinga mengi. Mama naye alianza kumchukia mke wangu mara aniambie kamuongelesha vibaya, mara aniambie hivi mara vile, mara ghafla kabila eti kisa wachaga ataniua sijui nini alikuja hana kitu huku anapendeza.

Baada ya kelele nyingi niliona hii itakuja kuniletea shida. Siku moja nilienda nyumbani, nikaomba kuongea na Mama, alianza kuniambia maneno mengi nikamsikiliza sana nikamuambia....

“Mama hivi kabla ya kuoa nilikua na nini?” Alinyamaza kisha akaniambia Gari, nikamuuliza na sasa hivi? Akataja vile vichache anavyovijua, nilimtajia na vingine vingi ambavyo havijui akabaki kushangaa. Akaniambia tatizo hushirikishi ndugu zako nikamuambia kwani walishiriki kuzichuma?

“Mama nakupenda sana, ila jua kuwa sina akili kama mke wangu nikimuacha yule mwanamke kesho,keshokutwa nitakua kama fala flani hivi sina kitu na yule mwanamke hata nikimuacha na laki moja tu mwakani yeye atakua milionea.

Nauchukuia sana umasikini hivyo kawaambie wanao kuwa wakiendelea kumsumbua mke wangu basi hata kwangu hawatakanyaga.Kujifanya wananiheshimu halafu wanamdharau mke wangu ni unafiki.Mke wangu simuachi, kwao haachi kujenga kama unataka nyumba Mama nilishakujengea hao ndugu watafute vya kwao na wenza wao!”

Mama aliongea sana akilalamika kuwa nimetekwa akili nikamuambia wewe ni Mama yangu hata ukinitukana siwezi kuacha kukuhudumia kwani ni kazi yangu lakini siwezi kumuacha mke wangu, ila waambie wanao kuwa wakimsumbua mke wangu nitasahau kuwa tumezaliwa tumbo moja. Mama aliongea, akaongea lakini niliondoka. Walijua kama natania wakidhani kama nimelishwa limbwata, ile nafika nyumbani mke wangu nakuta hajachangamka, nilimuuliza tatizo ni nini hakuniambia alisema yuko sawa.

Nilihisi kitu nikachukua simu yake, nikaangalia meseji mdogo wangu wa kike alikua akimtukana mke wangu kuwa amenilisha limbwata mpaka imefikia hatua namtukana Mama yangu, mara ataondoka tu laana itamshika na mambo kibao. Nilichukua simu ya mke wangu na kumpigia, alipokea hata kabla ya salamu alianza kutukana na vitisho kibao. Nilimuambia kuwa “Inaelekea Mama hakukupa ujumbe wangu vizuri ukauelewa, nilisema atakayeendelea kumsumbua mke wangu nitasahau kama ni ndugu yangu, basi wewe kuanzia sasa nimekwisha kusahau!”

Nilikata simu na sikumtafuta, ilikua mwaka jana, yeye yuko chuo nilikua namlipia mimi kila kitu nikakata kabisa, nikamuambia sitatoa. Mama akapiga simu akalia lakini nikakataa, mke wangu alinibembeleza sana kumsamehe lakini wapi nilimuambia sitaki. Nilifanya makusudi ili wajue kuwa namaanisha kuhusu msimamo wangu.
Mwaka huu wote ada ya chuo ya mdogo wangu aliyelipa ni mke wangu, hawakuniambia lakini najua kwani Mama ndiyo alikua anapiga anamuomba na pia sasa hivi akitaka matumizi anaomba kupitia mgongo wa Mama ili Mama aniombe nimpe.Najua zinaenda wapi nabaki nacheka tu moyoni.

Mdogo wangu nimemsamehe ila natamani ajue kuwa mke wangu ni jembe,ana akili ya Biashara ambayo mimi sina, akili yangu ni ya darasani tu ila kwa Biashara huyu mwanamke hapana.

Wakati mimi nikiiangalia Tsh 100,000 naona raundi kadhaa za bia Baa,yeye anaiona kama mtaji wa Biashara itakayozalisha mamilioni.

Nimuambie tu mdogo wangu najua bado yeye na Mama wanaamini nimelogwa, Si kweli,mimi sitaki tu umasikini nikimuacha huyu mke wangu ataondoka na mali zake.Biashara tunazomiliki sasa sitaweza kuziendeleza na hata nikiwapa ndugu zangu hawataweza kuziendeleza!


Funzo : Wanaume wengi wanafanikiwa kupitia migongo ya Wanawake
Story yako inafanana sana na yangu, kawaida napambana sana , ila nilikuwa nina matumizi mengi ya kijinga , until nilipokutana na huyu darasa la saba !!
Maisha yalibadilika the day ameingia ghetto , tukaanza kununua jiko la mchina sufuria na vijiko, baada ya hapo ilifata miujiza mingi sana ya maendeleo , yeye akiwa mama tu wa nyumbani ,sasa hivi anafanya biashara zake kwa usimamizi wake ,naamini nisingeweza bila yeye na mara kadhaa nimempab credit kwa hilo.
 
Alafu kesho mtu huyo huyo unamkuta anaparamia nyuzi za ajira[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na anakifuata hadi pm kuuliza connection kama panya aliemeza sumu akitafuta maji[emoji38][emoji38][emoji38]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]acha kabisa,ndo walimwengu sie tulivyo.
 
Hahahaha,hapanaa,kama hujui nikuambie tuu siku ingine usirudie kosa.
Content unayoweka publicly especially kwa maandishi kama sio kazi yako ni vizuri kum-acknowledge owner(ulipoitoa).
Usifanye kavile wewe ndo mhusika mkuu. Ni hayo tuu.
Poa usijali
 
Story yako inafanana sana na yangu, kawaida napambana sana , ila nilikuwa nina matumizi mengi ya kijinga , until nilipokutana na huyu darasa la saba !!
Maisha yalibadilika the day ameingia ghetto , tukaanza kununua jiko la mchina sufuria na vijiko, baada ya hapo ilifata miujiza mingi sana ya maendeleo , yeye akiwa mama tu wa nyumbani ,sasa hivi anafanya biashara zake kwa usimamizi wake ,naamini nisingeweza bila yeye na mara kadhaa nimempab credit kwa hilo.
Darasa la saba wengi wanaakili natural ambazo hazijachakachuliwa na theories nyingi za kijinga za wazungu na kunyonya nguvu asilia ya Mungu ndani ya mtu!!

Elimu zetu hizi ni toxic sana kwa minds zetu na zimefifiza uwezo asilia tuliopewa na muumba!

We fikiria kwa miaka 17 unafyonza elimu ya uwazungu akili ya utafutaji itatoka wapi!!?

Ni rahis sana darasa la saba kuwa tajiri kuliko msomi coz usomi ni ulemavu wa akili kuu yaani Brain stem ya asili imechoshwa na ujinga wa kusoma vitu vya kufikirika vya wageni!!

Nina bachelor lakini haina uwezo wa kunifanya niwe tajiri zaidi ya kuwa mtumwa wa kuajiriwa!!!

Ndio maana hata huyo muhasibu kasema yeye hana akili bali mkewe anajua huo uhasibu uliua kipaji chake cha asili ambacho Mungu alimpa!!!

Tujipe pole wasomi ndio maana kina profesa kabudi,mhongo, na wengineo wakakimbia usomi wao wakaenda siasani!!!
 
Back
Top Bottom