Hakuna mwanamke asiyependa raha hapa duniani
Na tunaamini ukiwa kwenye mahusiano na boy mwenye usafiri wa gari uta-enjoy mapenzi kuliko ambaye hana usafiri wake
Huwa tunafurahi na kujihisi peponi wakati mpo na boy wako kwenye mkoko halafu mpo wawili mnapiga stories huku anadrive mdogo mdogo
Pia tunapenda sana tour au kuzurura,hatupendi maisha ya kukaa viwanja au maeneo hayo hayo kila wakati,tunapenda leo Zanzibar,kesho Moshi weekend ijayo Arusha au Serengeti,na hapo usafiri wake pia unahusika maeneo mbalimbali ndani ya jiji
Halafu wanaume wenye usafiri huwa wanapenda kuwa smart sana,kwa hiyo tunajihisi kweli hapa nina bonge la HB
Hasara zake kwa wanaume wenye magari yao huwa upo roho juu,gari lake likipita tu unatamani ujue amembeba nani,kama hujakariri plate no unakuwa unatembea mjini likipita kama lake unataka uchungulie kama ni yeye au siye
Ila sasa hawa wanaume Mungu anawaona wakishajua kuwa wenye magari yao wanapendwa na kila mwanamke atakutesa sana,wanakuwa na wanawake wengi wa kila aina
Na usiombe mahali mlipo kuna chuo,wanafunzi wa kike wote ni wake ,wanafunzi wa day lift za kutosha na anavipitia sana,mabaa made wote ni wake na wadada wauza mafuta Shell za mafuta
Nakushangaa wewe mdada unayehangaika na wanaume wenye magari ,bora uwe na huyu asiye na gari maana yeye ni rahisi kupokea sim hana utetezi kuwa alkuwa ana drive,na huku umewahi kumuona anaongea na sim huku anadrive iweje leo
Na kama unataka kudate na mkaka mwenye gari lake mpime ngoma na uwe tayari kuumia
Sent using
Jamii Forums mobile app