Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,208
- 20,517
Miaka hii miwili nilikuwa maeneo ya vijijini basi katika zunguka yangu huko nilikutana na wazee kadhaa huko wakiugulia huu ugonjwa uitwao Tezi dume.
Baadhi ya wazee niliongea nao Waliniambia ya kuwa wana tatizo Hilo Kwa muda mrefu ila ni kuwa hawana fedha Kwa ajili ya kwenda kufanya upasuaji. Na waliniuliza kuwa kama serikali Inatoa msaada wa kimatibabu Kwa watu kama wao ambao hawana uwezo wa kujitibia.
Ukweli ni kuwa umaskini umesababisha wananchi wengi sana katika hizi nchi zetu kufariki Dunia huku wakijiona na hata wanafamilia wakishuhudia.